Nchi Ya Visiwa Vya Zanzibar

Nchi ya ‘’Visiwa Vya Zanzibar’’ vilijipatia uhuru wake mnamo tarehe 10 Desemba ya mwaka wa 1963 kutoka katika ‘’ Milki na Utawala wa Mkoloni Muingereza’’, chini ya utawala wa kimla wa ‘’Sultan Jamshid bin Abdullah’’, ambapo uhuru rasmi wa kujitawala na kujiongoza wao wenyewe ulipatikana kwa njia ya ‘’Mapinduzi’’ katika umwagaji wa damu kwa kumng’oa kutoka madarakani ‘’Sultan Jamshid bin Abdullah’’ mnamo tarehe 12 Januari ya mwaka wa 1964, na baadaye ‘’Nchi ya Visiwa Vya Zanzibar’’ ikaungana rasmi na ‘’Nchi Ya Tanganyika’’ (Tanzania Bara) na kupelekea kupatikana na kuzaliwa kwa ‘’Jamhuri Ya Muungano Ya Tanzania’’ (The
United Republic of Tanzania) mnamo tarehe 26 Aprili ya mwaka wa 1964. Ikumbukwe na ifahamike ya kwamba jina “TANZANIA” – limetokana na muunganisho wa maneno au majina ya awali ya ‘’Tanganyika’’ na ‘’Zanzibar’’ (“Tan”na “Zan”). Maandishi tamati yaliyobakia yaliongezwa katika kukamilisha ladha nzuri ya jina “Tanzania” ili kuleta maana sahihi, ingawa pia kuna neno ‘Azania’ likuhusishwa katika kuchangia na kukamilisha maana halisia ya chimbuko la jina ‘Tanzania’. Na maana ya neno au jina ‘Azania’ ina maanisha ‘’PWANI YA AFRIKA MASHARIKI’’
(EAST AFRICAN COAST).

Maelezo ya huduma za habari utalii wa ndani.

MAWASILIANO MENGINEYO MAKAO MAKUU (TANAPA)

+255 272508216

info@domestictourismsafaris.c  info@domestictourismsafaris.co.tz