Dondoo

Utambulisho

Tazama Ramani Utalii Tanzania ni Tovuti huru ya kielimu, kizalendo, kitaifa na kijamii nchini Tanzania ambayo ni binafsi na isiyo ya kiserikali inayoendeshwa, kuratibiwa na kisimamiwa na chuo cha Utalii Udzungwa (www.umctotz.org) kinachopatikana Mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro, kazkazini mashariki mwa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba Tovuti hii ni sehemu ya mchango wetu kama taasisi ya kielemu nchini kwetu Tanzania katika kuiunga mkono wizara ya maliasili na utalii na taasisi zake kama vile Bodi ya Utalii Tanzania, TAWA, TANAPA, NGORONGORO, na serikali yetu kwa ujumla wake ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, sambamba na wadau wengineo kwa ujumla wao katika sekta ya utalii nchini Tanzania kama vile wamiliki wa kampuni za utalii, hoteli na malazi, taasisi na umoja wa vyama mbalimbali vya sekta ya utalii katika jitihada zao katika uelimishaji, uhamasishaji, na uwezeshaji utalii wa ndani na mazingira yake kwa raia watanzania wazalendo watalii wa ndani. Uanzishwaji wa tovuti hii umetokana na tathmini ya chuo chenyewe kwa miaka mingi katika eneo hili la utalii wa ndani na uzoefu wake kwa kivitendo katika uhamasishaji, uelimishaji, na uwezeshaji wa utalii wa ndani kwa umma wa watanzania tangu mnamo mwaka wa 2008 katika kutumia lugha yetu aushi ya Kiswahili kama lugha ya Taifa katika kufikisha ujumbe kwa mammillioni ya raia wetu nchini Tanzania. Ni Imani yetu kama taasisi ya kielimu ya kwamba kila raia mtanzania mzalendo nchini Tanzania anayo nafasi na anawajibika katika nafasi yake katika jamii yetu popote pale alipo katika kutangaza utalii wa nchi yetu kwa wananchi wenzake na wageni watalii kutoka nje ya nchi yetu. Safari za matembezi ya utalii wa ndani yanayoratibiwa, kusimamiwa, kuendeshwa, na kuwezeshwa na Chuo cha Utalii Udzungwa cha Mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro (www.umctotz.org) zilianzishwa na kuzinduliwa tangu mnamo mwaka wa 2008 na kupelekea kuwepo kwa uanzishwaji wa kampuni ya utalii wa ndani katika uelimishaji, uhamasishaji,na uwezeshaji utalii wa ndani (www.domestictourismsafaris.com/www.domestictourismsafaris.co.tz) na hatimaye hivi sasa Tovuti ya Kiswahili , Jarida la Tazama Ramani Utalii Tanzania na vitabu vya viongozi katka lugha yetu ya Taifa ya Kiswahili. Katika kutoa fursa kwa Watanzania watalii wa ndani, safari zetu za matembezi hifadhini katika maeneo tofauti ya hifadhi za Taifa na maeneo mengineyo ndio yanayokamilisha dhamira yetu ya kuwaelimisha na kuwahamasisha watanzania wote wa umri wowote ule na wa tabaka zote kuwa wapenda mazingira na kutangaza vivutio vyetu asilia vya utalii pamoja na kiutamaduni nchini Tanzania.

DHAMIRA YA MTANDAO WA TAZAMA RAMANI UTALII TANZANIA

Kufikia mamilioni ya raia watanzania watalii wa ndani kupitia jarida lake la utalii wa ndani la Tazama Ramani Utalii Tanzania, vipindi maalumu katika redio na televisheni, makala katika televisheni, vitabu vya viongozi vya utalii (Guide books), kanda za video na Dvds, Ramani pamoja na vyombo vya habari mbalimbali nchini Tanzania.

TIMU YETU YA TAZAMA RAMANI UTALII TANZANIA

Timu yetu ya Tazama Ramani Utalii Tanzania inaundwa na idara mbalimbali za vijana wa kitanzania waliobobea katika taaluma zao za kazi kama vile timu ya watafiti, wavumbuzi na wachokonozi, waandishi wa vitengo mbalimbali katika taaluma husika kama vile wanajoolojia, wanahistoria, wanamazingira, pamoja na wanabayolojia na wananchi kwa ujumla wake. Timu yetu ya safari utalii na matembezi hifadhini hutoa ushirikiano wa hali ya juu kwa kila mtalii wa ndani kutika matembezi yetu hifadhini. Ushirikiano huu ni kama vile kubadilishana mawazo na maarifa ya mambo husika na mengineyo.