Ni pamoja na Hifadhi za Taifa (National parks): Tanzania ina jumla ya Hifadhi za Taifa 21 kwa upande wa Tanzania bara na 1 iliyo pekee visiwani Zanzibar inayofahamika kama ‘’Jozani Chwaka Bay National Park’. Hifadhi za Taifa kwa upande wa Tanzania bara ni pamoja na Arusha, Tarangire, Ziwa Manyara, Saadani, Mkomazi, Mikumi, Ruaha, Kitulo, Katavi, Udzungwa, Burigi – Chato, Saanane, Nyerere, Gombe, Kisiwa cha Rubondo, Mahale, Ibanda – Kyerwa, Rumanyika – Karagwe, Serengeti,Ugalla,pamoja na Mlima Kilimanjaro. Hata hivyo, kusini mwa Tanzania unaweza kutembelea Hifadhi za Taifa ambapo katika kila Hifadhi utakutana na upekee wa aina yake kama vile Maporomoko ya Maji ya Sanje katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa mkoani Iringa na Morogoro, wanyamapori swala aina ya kudu wakubwa na kudu wadogo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa. Ndege wazuri wenye kupendeza na kuvutia na pia maua maarufu kama vile bustani ya Mungu katika Hifadhi ya Taifa ya Kitulo, pamoja na Mabwawa na Mito mizuri ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Nyerere na bila kusahau makundi makubwa ya wanyamapori Nyati au Mbogo katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi mkoani Morogoro. Viboko, Mamba na Mto mkubwa wa Rufiji ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Nyerere mkoani Pwani, Morogoro, pamoja na Lindi.