NYANDA ZA JUU KUSINI (SOUTHERN HIGHLANDS)

Maelezo Yote Na Ubunifu (Mwalimu Edgardo KabulwaWelelo)

Nyanda za Juu Kusini zinapatikana kijiografia Kusini Magharibi mwa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na inajumuisha mikoa 7, ambayo ni IRINGA, NJOMBE, RUKWA, KATAVI, MBEYA, SONGWE, pamoja na RUVUMA. Ukanda huu wa Nyanda za Juu Kusini (Southern Highlands) unaunda mkusanyiko wa Milima yenye kuwa na asili inayotokana na Volkano pamoja na misitu na nyasi na vilevile asilimia kubwa ya ngano na viazi vya Tanzania vinalimwa katika ukanda huu. Katika ukanda huu wa Nyanda za Juu Kusini kunapatikana hali ya hewa yenye kuwa na baridi pamoja na mvua nyingi kuliko kanda nyinginezo za Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Nyanda za utalii zikiwemo ni kama vile Milima mirefu, maziwa makubwa, mbuga za wanyama, urithi wa kiutamaduni pamoja na reli ya TAZARA.

Maelezo ya huduma za habari utalii wa ndani.

MAWASILIANO MENGINEYO MAKAO MAKUU (TANAPA)

+255 272508216

info@domestictourismsafaris.c  info@domestictourismsafaris.co.tz