TALII NA TEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA RUAHA (RUAHA NATIONAL PARK)
Mkoani Iringa Katika Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini (Southern Highlands Zone) Mwa Jamhuri ya muungano ya Tanzania (The united Republic of Tanzania)
Chanzo Cha Chimbuko Halisia Kimaelezo (Mwalimu Edgardo Kabulwa Welelo)
Ukweli Wa Mambo Kuhusiana Na Hifadhi Ya TaifaYa Ruaha (Ruaha National Park) Mkoani Iringa Katika Ukanda Wa Nyanda Za Juu Kusini(Southern Highlands Zone); Hii ndio Hifadhi ya Taifa (National Park) iliyo ya pili kwa ukubwa wa eneo la bardhi yenye kuwa na takribani kilomita za mraba 20,226 (au sawa na takribani maili za mraba 7,809) mpaka hivi sasa nchini kwetu Tanzania baada ya Hifadhi ya Taifa ya Nyerere (Nyerere National Park). Ukubwa wa eneo la ardhi katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (Ruaha National Park) umepatikana baada ya kuongezwa kwa ukubwa wa eneo lake wa maeneo ya ardhi ya uhifadhi ya ‘’Mapori ya Akiba ya Wanyamapori’’ (Game Reserve) ya ‘’USANGU’’ pamoja na ‘’Ardhi Oevu’’ (wetlands) mnamo mwaka wa 2008, na kuifanya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (Ruaha National Park) kuwa mojawapo ya ‘’Hifadhi Za Taifa Kubwa Barani Afrika’’. Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (RuahaNational Park) ina utajiri wa kiwango cha hali ya juu sana na kilicho cha upekee wa uoto wa asili pamoja na wanyamapori kama vileTembo/Ndovu (African/Bush/Savanna Elephant), Nyati/Mbogo (African/Savanna/Cape Buffalo), Swala (Antelopes) wa aina mbalimbali ambapo baadhi yao ni adimu na pia waliopo hatarini kutoweka kama vile ‘’Mbwa Mwitu’’ (Wild dogs).Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (Ruaha National Park) ni maarufu sana barani Afrika na Duniani kwa ujumla wake kama mojawapo ya maeneo ya uhifadhi yaliyo bora sana katika utalii wa utazamaji wa wanyamapori (Game viewing) sambamba na taswira au sura yake ya kijiografia na mandhari nzuri yenye kupendeza na kuvutia. Jina la Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (Ruaha National Park) limetokana na ‘’Mto Ruaha Mkuu’’ (The Great Ruaha River) ambapo kimsingi nakihalisia neno ‘’RUAHA’’ limetoholewa kutoka katika matamshi ya lugha ya jamii ya kabila la ‘’WAHEHE’’ (LUVAHA) ikimaanisha ‘’kitu kilicho kikuu au kikubwa’’ (GREAT) na kitu hicho kikuu kilikuwa ni ‘’Mto Wenyewe’’ na hatimaye kupatikana maana halisi iliyokamilika ‘’Mto Ruaha Mkuu’’(The Great Ruaha River) na vilevile ni vema na busara ikakumbukwa na kueleweka ya Kwamba umeme unaozalishwa kwa njia ya maji na ulio mwingi nchini kwetu Tanzania pia unatokea katika ‘’Mto Ruaha Mkuu’’(The Great Ruaha River) ambapo umeme wake unatengenezwa na
kuzalishwa Kidatu.
Ushauri kwa watalii raia wa Tanzania katika kujiandaa na kujipanga kimaandalizi na kikamilifu kwa Safari utalii
Utafiti ni lazima ufanyike wa kupata maelezo ya taarifa za hifadhi yenyewe sambamba na wadau wa sekta ya utalii wanaotoa huduma ya matembezi katika hifadhi hii ili kupata gharama husika jinsi zilivyo na mambo mengineyo muhimu katika maandalizi ya usafiri. Muda wa maandalizi katika kujiandaa ni muhimu sana katika kufahamu ya kwamba haya yote yanahitaji fedha na bajeti ya matumizi ya fedha zenyewe mwanzo mpaka tamati ya safari utalii.
Hifadhi ya Taifa ya Ruaha’’ (Ruaha National Park) ilianzishwa rasmi kama ‘’Hifadhi ya Taifa’’ (National Park) mnamo mwaka wa 1964. Eneo la ardhi ya ‘’Hifadhi ya Taifa ya Ruaha’’ (Ruaha National Park) ni tajiri sana kihistoria ambapo kabla ya uhifadhi wa eneo hili ni ya kwamba hapo zamani miaka mingi sana kupita zilikuwepo ndani ya hifadhi njia za mwanzo kuweza kufahamika za kibishara zikipita maeneo ya katikati ya hifadhi hii.Njia za msafara wa biashara ya ‘’Watumwa Za Wakoloni Waarabu’’ (The Arab Trading Caravans) walitumia njia hizi zilizopita ‘’Hifadhini Ruaha’’ kabla ya uhifadhi kuchukuav nafasi yake mwanzoni kabisa mwa kipindi cha karne ya 19. Ilipofikia mnamo mwaka wa 1830 wakoloni waarabu wafanyabiashara ya watumwa kutoka ‘’Ukanda Wa Mwambao Wa Pwani Ya Afrika Mashariki’’(East African Coast) walianza kusafiri kuelekea uelekeo wa njia zilizokuwa zinaelekea upande wa kaskazini mwa eneo la leo hii ya ‘’Hifadhi ya Ruaha’’, wakiendelea na njia iliyokuwa inawapeleka katika eneo linalofahamika leo hii kama ‘’Mkoa wa Dodoma’’.Hatimaye njia hizi za msafara wa biashara za watumwa (Slave Trade Caravan Routes) zilikuja kutumika na wavumbuzi (Explorers) kama vile BURTON pamoja na SPEKE baina ya mwaka 1857 mpaka 1858, bila kusahau pia na wavumbuzi wengineo wa mwanzoni waliopita. Mnamo mwaka wa 1886] ‘’TANGANYIKA’’ (Leo hii ikifahamika kama Tanzania Bara) ikawa chini ya uthibiti na mamlaka ya utawala wa ‘’Wakoloni Wajerumani’’ ikifahamika katika kipindi cha nyakati hizo kama ‘’Ujerumani ya Afrika Mashariki’’ (German East Africa). Jamii ya kabila la ‘’Wahehe’’ wakiongozwa na ‘’Chifu Mkwawa’’ walikuwa ni mojawapo ya kabila lililotawala eneo hili linalofahamika leo hii kama ‘’Hifadhi ya Taifa ya Ruaha’’ (Ruaha National Park).Chifu Mkwawa wa kabila la ‘’Wahehe’’ pia aliongoza na kutawala eneo muhimu kuanzia kutokea eneo la leo hii linalojulikana kama ‘’Mkoa wa Njombe’’ katika upande wake wa kusini kuelekea ‘’KILOSA’’ mojawawapo ya wilaya katika ‘’Mkoa wa Morogoro’’ pamoja na ‘’MPWAPWA’’ pia nayo mojawapo ya wilaya katika ‘’Mkoa wa Dodoma’’ katika upande wake wa kaskazini na vilevile kutokea ‘’Mto Ruaha Mkuu’’(The Great Ruaha River) kuelekea ‘’KILOMBERO’’ nayo vilevile mojawapo ya wilaya katika ‘’Mkoa wa Morogoro’’ Ni vema na busara ikaeleweka na kukumbukwa ya kwamba ‘’Njombe’’ hapo awali ilikuwa ni mojawapo ya wilaya katika ‘’Mkoa wa Iringa’’ kabla ya ‘’Mkoa wa Iringa’’ kumegwa na kutenganishwa na hatimaye kupatikana kwa ‘’Mkoa Mpya Wa Njombe’’ mnamo mwaka wa 2012.Jamii ya kabila la ‘’Wahehe’’ walitambulika na kufahamika kama mojawapo ya jamii ya watu ‘’Shupavu, jasiri na mashujaa’’ katika kupigana na kushinda vita vyao walivyopambana na jamii nyinginezo za makabila nchini kwetu Tanzania na vilevile wakoloni watawala ‘’Wajerumani’’ chini ya uongozi na utawala wa kiongozi wao maarufu ‘’Chifu Mkwawa’’.Hata hivyo, baada ya kupigana vita vingi na pia kuvishinda, ilipofikia mnamo mwaka wa 1894, ‘’Chifu Mkwawa’’ alilazimika kutoroka na kukimbilia katika maficho baada ya vikosi vyake vya upiganaji katika vita kuanza kuishiwa nguvu na kuanza kuzorota.Baada ya ‘’Chifu Mkwawa’’ kukimbilia katika maficho aliweza kuendeleza vita vya msituni (Guerrila Warfare) katika kupigana na kupambana na ‘’Wakoloni Wajerumani’’ katika kipindi kingine cha takribani miaka 4. Mengi ya haya maficho yaliyotumika na ‘’Chifu Mkwawa’’ katika kujificha wakati wa vita vyake vya msituni (Guerrila Warfare) dhidi ya majeshi ya ‘’Wakoloni Wajerumani’’ yanasemekana pia yamo ndani ya ‘’Hifadhi ya Taifa ya Ruaha’’ (Ruaha National Park).Hatimaye ilipofikia mnamo mwaka wa 1898, majeshi ya ‘’Wakoloni Wajerumani’’ yalifanikiwa katika kushinda vita hivyo dhidi ya ‘’Chifu Mkwawa’’ na kuuangusha kabisa utawala wake, lakini siri ya kiongozi huyu wa kabila la ‘’Wahehe’’ aliyepata kutokea kuwa mashuhuri na shupavu nchini kwetu Tanzania na barani Afrika kwa ujumla wake itabakia kuwa iliyofichika katika ardhi ya eneo la ‘’Hifadhi ya Taifa ya Ruaha’’ (Ruaha National Park).Ilikuwa ni katika nyakati hizo za utawala wa ‘’Wakoloni Wajerumani’’ mnamo mwaka wa 1910 pale ambapo eneo la ardhi ya leo hii ya ‘’Hifadhi ya Taifa ya Ruaha’’ (Ruaha National Park) ilipoanzishwa rasmi kama ‘’Pori la Akiba la Wanyamapori’’ lililofahamika kama ‘’SABA’’(SABA GAME RESERVE).Hatimaye ilipofikia mnamo mwaka wa 1946 ‘’wakati wa kipindi cha nyakati za utawala wa (Wakoloni Waingereza)’’ wakatangaza eneo hili la pori la akiba ya wanyamapori la ‘’SABA’’(SABA GAME RESERVE) kuongezwa na kupanuliwa kwa ukubwa wa eneo lake la ardhi na kupelekea kufahamika kama ‘’Pori la Akiba la Wanyamapori la Rungwe’’(Rungwe Game Reserve).Hatimaye ilipofikia mnano mwaka wa 1964 baada ya nchi yetu ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania (The United Republic of Tanzania) kujipatia uhuru wetu wenyewe wa kujiongoza na kujitawala kupitia viongozi wetu ndipo ambapo sehemu ya ardhi ya upande wa kusini mwa ‘’Hifadhi ya Taifa ya Ruaha’’ (Ruaha National Park ) ilipotangazwa na Serikali na kuanzishwa rasmi.Mnamo mwaka wa 1974 kipande cha sehemu ya ardhi ya uhifadhi katika upande wa kusini mashariki mwa ‘’Mto Ruaha Mkuu’’(The Great Ruaha River) uliongezwa kama mojawapo ya eneo la ‘’Hifadhi ya Taifa ya Ruaha’’ (Ruaha National Park).Lakini pia vilevile tena ilipofikia mnamo mwaka wa 2008, ‘’Hifadhi ya Taifa ya Ruaha’’ (Ruaha National Park) ikaongezwa na kutanuliwa ukubwa wa eneo lake la ardhi ambapo ilihusisha maeneo ya ‘’Ardhi Oevu ya Usangu’’(Usangu Wetland) ambayo ilikamilisha mipaka ya eneo la hifadhi leo hii.Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba ‘’Hifadhi ya Taifa ya Ruaha’’ (Ruaha National Park) ni mojawapo ya ‘’Hifadhi za Taifa Tanzania’’ (Tanzania National Parks) ambayo ina upekee na utofauti wa aina yake wa kuweza kubahatika katika kuzungukwa na ‘’Mapori ya Akiba ya Wanyamapori’’ (Game Reserves), ‘’Hifadhi za Kijumuiya za Wanyamapori’’ (Wildlife Management Areas) pamoja na Hifadhi za Misitu ya Asili (Forest Nature Reserves).Kwa mfano hai ni pamoja na eneo la ardhi la uhifadhi wa mazingira wenye kuwa na ukubwa wa takribani kilometa za mraba 45,000 (au sawa na takribani maili za mraba 17,000) wa maeneo ya ardhi ya ‘’Rungwa – Kizigo – Muhesi’’( Rungwa – Kizigo – Muhesi ecosystem) ambayo huhusisha maeneo ya ardhi kama vile ‘’Mapori ya Akiba ya Wanyamapori ya ‘’Rungwa’’(Rungwa Game Reserve) pamoja na ‘’Kizigo na Muhesi’’(Kizigo and Muhesi Game Reserves) na bila kusahau ‘’Hifadhi za Kijumuiya za Wanyamapori ya ‘’Mbomipa’’( Mbomipa Wildlife Management Area).
’Hifadhi ya Taifa ya Ruaha’’ (Ruaha National Park) ina ukubwa wa eneo la ardhi yenye kufikia kilomita za mraba takribani 20,226 (au sawa na maili za mraba takribani 7,809). Hii ndio iliyo mojawapo ya ‘’Hifadhi ya Taifa Tanzania’’ (Tanzania National Parks) ya pili kwa ukubwa wa eneo la ardhi nchini kwetu Tanzania baada ya ‘’Hifadhi ya Taifa ya Nyerere’’ (Nyerere National Park) ambapo hapo zamani ilijulikana kama ‘’Pori la Akiba la Wanyamapori la SELOUS’’ (SELOUS GAME RESERVE). Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba hapa kuwa ‘’Pori la Akiba la Wanyamapori la SELOUS’’ (SELOUS GAME RESERVE) ni eneo la uhifadhi ambalo kimsingi lilianzishwa kihistoria toka mnamo mwaka wa 1905 ambapo ukubwa wake wa eneo la ardhi ulifikia takribani ‘’kilometa za Mraba 55,000’’, na kijiografia eneo hili la ardhi linapatikana na kutawanyika mipaka yake katika (‘’Mikoa ya RUVUMA, LINDI, MTWARA, MOROGORO na PWANI’’).Karibia kilometa za ‘’Mraba takribani 30,000’’ kutoka katika kilometa za ‘’Mraba 55,000’’ za hapo awali za eneo lote la ardhi ya ‘’SELOUS’’ zilimegwa na kuanzishwa ‘’Hifadhi ya Taifa ya Nyerere’’ (Nyerere National Park) mnamo mwaka wa 2019 katika kumuenzi ‘’Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere’’ kutokana na mchango wake mkubwa kwa nchi yetu ya Tanzania alioutoa katika harakati na mapambano ya kupigania ulinzi na uhifadhi wa mali asili zetu zilizo urithi wetu nchini kwetu Tanzania kwa ajili ya vizazi vilivyopo na vijavyo.Sehemu iliyobakia ya ardhi ya ‘’Selous’’ inabakia kuwa endelevu kama ‘’Pori la Akiba la Wanyamapori’’ (SELOUS GAME RESERVES).’’Hifadhi ya Taifa ya Nyerere’’ (Nyerere National Park) kwa hivi sasa ndio iliyo kubwa zaidi nchini kwetu Tanzania ikipatikana zaidi kijiografia katika ‘’Mikoa ya PWANI, MOROGORO na LINDI).
Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (Ruaha National Park) inafikika kwa njia ya usafiri wa barabara umbali wa takribani kilomita 120 mpaka 130 (au sawa na takribani maili 81) kutokea katika upande wa ‘’Magharibi’’ mwa ‘’Mji wa Iringa’’(Iringa City). Vilevile Hifadhi ya Ruaha pia inafikika kwa njia ya usafiri wa barabara umbali wa takribani kilomita 322 kutokea ‘’Mji wa Mikumi’’ katika nmkoa wa Morogoro. Pia ni sawa na umbali wa takribani kilomita 369 kutokea Mkoani Dodoma, yaliyo makao makuu ya ‘’Taifa Tanzania’’. Kutokea ‘’Jijini Darn es Salaam’’ (Dar es Salaam Commercial Capital) ni sawa na umbali wa takribani kilomita 615. Kutokea ‘’Jijini Mbeya’’ (Mbeya City) ni sawa na umbali wa
takribani kilomita 502. Na kutokea ‘’Jijini Arusha’’ (Arusha City) ni takribani kilomita 807. Ni sawa na umbali unaotumia muda wa takribani wa saa 2 mpaka 3 kutokea upande wa ‘’Magharibi’’ mwa ‘’Mji wa Iringa’’ (Iringa City) na vile vile ni takribani muda wa saa 9 mpaka 10 kutokea ‘’Jijini Dar – es -
Salaam’’.
Ni pamoja na ‘’Mito’’(Rivers) , ‘’Kuta za Bonde la Ufa’’(Rift Valleyb Escarpment/Rift Wall) , ‘’Chemichemi za maji’’(Springs), ‘’Vilima’’(Hills) vya hapa na pale, ‘’Uoto wa Asili wa Mimea ya Miti ya Miombo’’(Miombo Woodland) ambapo nchini kwetu Tanzania,uoto huu wa asili umechukua karibia nusu ya ukubwa wa eneo la ardhi yote ya Tanzania ambao umetawanyika na kutawala zaidi sehemu kubwa ya ‘’Magharibi na Kusini’’ mwa Tanzania. Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba ‘’Bonde Kuu la Ufa’’ (The Great Rift Valley) ni mojawapob ya sura au taswira kubwa ya maumbile ya kijiografia nchini kwetu Tanzania, Barani Afrika na Duniani kwa jumla wake na pia ‘’Bonde Kuu la Ufa’’(The Great Rift Valley) limepita katikati kabisa ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (Ruaha National Park). ‘’Ukuta wa Bonde la Ufa’’ (Rift Wall of The Great Rift Valley/Escarpment) unaofikia urefu wa kwenda juu wa takribani mita 50 mpaka 100 katika upande wa ‘’Kaskazini – Mashariki’’ mwa ‘’Hifadhi ya Ruaha’’ ni mojawapo ya kivutio cha utalii chenye kuwa na mandhari nzuri ya kuvutia na
kupendeza. Inafikiriwa na kudhaniwa na wataalamu ya elimu ya miamba ya kwamba ‘’Bonde la Mto Ruaha Mkuu (The Valley of The Great Ruaha River) ni mojawapo ya matokeo ya ‘’Bonde Kuu la Ufa’’ (The Great Rift Valley) kupita katikati ya hifadhi yenyewe. ‘’Mto Ruaha Mkuu’’ (The Great Ruaha River) hutiririsha maji yake ya mto kwa takribani umbali wa kilomita 160 kuelekea katika uelekeo wa eneo lote la mpaka wa mashariki mwa hifadhi kupitia mabonde mbalimbali pamoja na ‘’Ardhi Wazi Tambarare’’ (Open Plains). ‘’Bonde Kuu la Ufa’’ (The Great Rift Valley) kimsingi ni mpasuko wa ardhi katika ganda la dunia kutokana na kugongana na kutawanyika kwa miamba ya ganda la dunia (Blocks of Earth Crust) ambayo ni mojawapo ya sehemu inayounda sehemu ya tabaka la nje la muundo wa dunia (Earth’s Crust). Nchini kwetu Tanzani ‘’Bonde Kuu la Ufa’’ (The Great Rift Valley) limegawanyika katika ‘’Mikondo Miwili’’ ambayo ni pamoja na ‘’Mkondo wa bonde la Ufa la upande wa Mashariki’’ (Eastern Rift Valley) pamoja na ‘’Mkondo wa bonde la Ufa la upande wa Magharibi’’). Kwa maelezo zaidi pitia na soma tena ‘’Maelezo ya Hifadhi ya Ziwa Manyara (Lake Manyara National Park) ambayo kimsingi ni hifadhi ambayo imepitiwa na pia inapatikana yote ndani ya ‘’Mkondo wa bonde la Ufa la Mashariki’’. Kwa ufupi ‘’Hifadhi ya Taifa ya Ruaha’’(Ruaha National Park) ina aina mbalimbali ya upatikanaji wa maumbile asilia ya kijiolojia kuanzia ‘’Bonde Kuu la Ufa’’ (The Great Rift Valley), ‘’Mikondo ya mito’’, ‘’Chemichemi asilia za maji’’(Natural Springs), ‘’Ardhi Oevu’’(Wetlands), ‘’Chemichemi za maji moto’’(Hot Water Springs), ‘’Miamba ya Ardhini Katika Uso wa Ardhi’’(Rocky Outcrops/Kopjes), ‘’Vilima na Milima(Hills and Mountains). Mito mikuu ipatikanayo ndani ya Hifadhi ni pamoja na ‘’Mto Ruaha Mkuu’’(The Great Ruaha River), ‘’Mto Mzombe’’(The Mzombe River), ‘’Mto Jongomero’’(The Jongomero River), ‘’Mto Mdonya’’(The Mdonya River), ‘’Mto Mwagusi’’(The Mwagusi River) na kadha wa kadhalika. Chemichemi za maji asilia ni pamoja na ‘’Mkwawa’’, ‘’Mwayembe’’ na ‘’Makinde’’, na ‘’Majimoto Springs’’
Inaanzia mita ‘’750 katika ‘’Bonde la Mto Ruaha Mkuu (The Great Ruaha Valley), ‘’Mita 1700 katika kilele cha Mlima Datambulwa katika upande wa kusini, mpaka Mita 1900’’ katika kilele cha Mlima Ikingu katika upande wa Magharibi kutoka katika usawa wa bahari. Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (Ruaha National Park) ina majira ya msimu wa mvua wa ukanda wa ‘’Misitu ya Kitropiki’’. Msimu wa kipindi cha mvua fupi (Short – Rainfall Season/Short – Rainy Season) kawaida huanzia ‘’Mwezi Novemba mpaka Mwezi Februari’’, wakati ambapo msimu wa kipindi cha ‘’Mvua Ndefu Za Masika’’ (Long – Rainy Season/Wet Season) kawaida kimsingi huanzia baina ya ‘’Mwezi Machi na Mwezi Aprili’’. Kipindi cha msimu wa baridi kawaida huanzia ‘’Mwezi Julai’’ ambapo wakati mwingine kiwango cha juu cha joto cha nyuzi joto 30 hushuka na kufikia takribani nyuzi joto 15 wakati wa kipindi cha nyakati za usiku na baadaye tena huongezeka. Kiwango cha mvua hutofautiana kwa mwaka mzima kwa wastani wa takribani ‘’Milimita za Mvua’’ baina ya ‘’Milimita 520 katika ‘’Makao Makuu ya Hifadhi ya Taifa Ruaha (MSEMBE), mpaka zaidi ya Milimita 800’’ juu ya kuta za bonde la ufa na uoto wa asili wa mimea ya miti ya miombo, wakati ambapo wastani wa joto ni takribani ‘’Nyuzi Joto 28’’. Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (Ruaha National Park) kawaida msimu wake wa ‘’Kipindi Cha Kiangazi’’ (Dry – Season) ni kati ya ‘’Mwezi Juni na Mwezi Oktoba’’ ambapo katika kipindi hichi cha nyakati kawaida kiwango cha joto katika ‘’Makao Makuu ya HifadhiMSEMBE’’, hufikia nyuzi joto takribani 35.
Ni pamoja na ‘’Mto Ruaha Mkuu’ ’(The Great Ruaha River) ambao kimsingi mto huu hutoa fursa kubwa zaidi hususani wakati wa kipindi cha msimu wa kiangazi na kuweza kuvutia wanyamapori kama vile Tembo/Ndovu (African/Savanna/Bush Elephant), aina mbalimbali ya viumbe hai ndege, Tandala Wakubwa na Wadogo (Greater and Lesser Kudus), Viboko (Common/East African Hippopotamus), na bila kusahau ‘’Mamba’’ aina ya ‘’Nile’’ (Nile Crocodiles) na kadha wa kadhalika. Kivutio kinginecho ni pamoja na ‘’Ardhi Oevu Tambarare ya Usangu’’ (The Usangu Flats) eneo ambalo linapatikana takribani umbali wa maili 50 (au sawa na takribani kilometa 80) katika upande wa ‘’Kusini – Magharibi’’ mwa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (Ruaha National Park) ambapo eneo hili huwa ni chanzo cha maji ya ‘’Mto Ruaha Mkuu’’ (The Great Ruaha River). ‘’Mto Mzombe’’ (The Mzombe River) ambao kimsingi ni mto ambao unakuwa kama mpaka wa kaskazini wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ni mto ambao hutiririsha maji yake ya mto kuelekea ‘’Bwawa la Mtera’’ (Mtera Dam). Kwa pamoja ‘’Bwawa la Mtera na Bwawa la Kidatu’’ kihistoria ni mabwawa yaliyojengwa na Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania (The United Republic of Tanzania) toka mnamo miaka ya 1970 na mapema mwanzoni wa mwaka 1980 kwa ajili maalumu ya uzalishaji wa umeme unaotumia maji. Kuelekea chini zaidi ya ‘’Bwawa la Kidatu’’ ni ya kwamba ‘’Mto Ruaha Mkuu’’ (The Great Ruaha River) huungana kwa pamoja na ‘’Mto Rufiji’’ (The Rufiji River) ambao kimsingi ndio mto ulio mkubwa kuliko yote nchini Tanzania unaopatikana wilayani Rufiji katika mkoa w Pwani, mito hii miwili hutiririsha maji yake kwa pamoja kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Nyerere (Nyerere National Park) na ‘’Pori la Akiba la Wanyamapori la ‘’SELOUS’’ na hatimaye bahari ya Hindi (The Indian Ocean) na jiji la Dar es – Salaam, takribani umbali wa kilomita 150 kusini
Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (Ruaha National Park) ina utajiri wa hali ya juu sana wa upatikanaji wa aina mbalimbali za wanyamapori. Orodha ifuatayo ni miongoni mwa wachache katika orodha hiyo ya utajiri wa hifadhi hii; Impala (Swala Pala), Fisi Madoadoa (Spotted Hyenas), Duma (Cheetah), Tandala Wakubwa na Wadogo (Greater and Lesser Kudus), Palahala (Sable Antelope), Korongo (Roan Antelope), Swala Granti (Grant Gazelle), Mbwa Mwitu (Wild dog), Nyati/Mbogo (African/Savanna/Cape Buffalo), Simba (Lions), Chui (Leopards), Pofu (East African Eland/Patterson Eland), Pundamilia (Common/Plains/Burchell’s Zebra), Kuro (Common Waterbuck), Twiga (Kilimanjaro/Maasai Giraffes), Ngiri (Common Warthog) na Pongo (Bushbucks). Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba ‘’Hifadhi ya Taifa ya Ruaha’’ (Ruaha National Park) ina utajiri wa hali ya juu sana wa aina mbalimbali za viumbe hai
ndege kuweza kuripotiwa na kurekodiwa kitafiti na kisayansi zaidi ya spishi za
ndege takribani 400. Na hii inachangiwa kwa kiasi kikubwa na upatikanaji wake kijiografia ambapo hupelekea kutembelewa na ndege wahamaji (migratory birds) kutokea ‘’Uzio’’ wa ‘’Kaskazini’’ (Mstari wa IKWETA KASKAZINI/Northern Hemisphere) pamoja na ‘’Uzio’’ wa ‘’Kusini’’ (Mstari wa IKWETA KUSINI/Southern Hemisphere).
Hifadhi ya Taifa ya Ruaha’’ (Ruaha National Park) inaangukia katika ukanda wa ‘’Uoto wa Asili unaojulikana kama ‘’Zambeziani’’(Zambezian Region) au ‘’Uoto wa asili wa Miombo’’(Miombo Woodland) ambao kimsingi umechukua ukubwa wa eneo la ardhi takribani zaidi ya asilimia 40 ya ukubwa wote wa eneo la ardhi ya Tanzania. ‘’Uoto huu wa asili wa ‘’Zambeziani’’(Zambezian Region) au ‘’Uoto wa
asili wa Miti ya Miombo (Miombo Woodland) umechukua sehemu kubwa ya maeneo ya ‘’Magharibi na Kusini mwa Tanzania’’ ambapo uoto wa asili wa miti ya miombo (Miombo Woodland) umetawala na kutalamaki. Aina ya mimea ya miti ipatikanayo katika ukanda huu wa ‘’Uoto wa asili wa mimea miti ya Miombo’’ (Miombo Woodland) ni pamoja na ‘’Koo za mimea miti ya ‘’Isoberlinia’’, ‘’Julbernadia’’. Miti mingi ya mbao na chakula inatokea katika ukanda huu. Kwa ufupi Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (Ruaha National Park) imetalamaki kuwa na uoto wa asili wa maeneo ya ardhi nusu jangwa ambapo uoto wa asili wa mimea ya miti ya ‘’Mibuyu’’(Baobabs), ‘’Migunga’’(Acacias) na aina nyinginezo umetawala kwa kiasi kikubwa. Kwa ujumla wake kunapatikana zaidi ya spishi 1650 za uoto wa asili wa mimea mbalimbali ndani ya hifadhi hii. Pia ni sehemu pekee ya hifadhi ambapo wanyamapori wakubwa kama vile ‘’Tandala Wakubwa na Wadogo (Greater and Lesser Kudus), Palahala (Sable Antelopes), Korongo (Roan Antelopes) huweza kuonekana kwa urahisi katika makazi ya miti ya miombo.
Wakati mzuri na ulio bora wa kutembelea na kutalii ‘’Hifadhi ya Taifa ya Ruaha’’(Ruaha National Park) ni katika ‘’kipindi cha msimu wa kiangazi’’ cha katikati ya ‘’Mwezi Mei mpaka Mwezi Desemba’’ kwa ajili ya kuwaona ‘’Wanyamapori Wawindaji na Walao Nyama’’ (Predators) pamoja na ‘’Wanyamapori Wengineo Wakubwa’’. Kwa ‘’utazamaji wa viumbe hai ndege’’(Bird –Watching), uzuri na mandhari ya uoto wa asili wa mimea wa miti ya mapori na maua ni wakati wa kipindi cha msimu wa masika ambao ni ‘’Mwezi wa Januari mpaka Aprili’’. Vilevile kwa ‘’Wanyamapori Swala Tandala Wakubwa Madume’’ (Male Greater Kudus) wao kimsingi huonekana na hupatikana katika kipindi cha ‘’Mwezi wa Juni’’ kipindi chao maalumu kwa ajili ya kujamiana na kuzaliana (Breeding Season).
Waandaaji wa safari utalii yenu ya matembezi hifadhini ni vema na busara wakazingatia kwa umakini mkubwa mambo muhimu yanayohusiana na huduma hii iliyo ya umuhimu. Je mtabeba vyakula vyenu vya kujipikia wenyewe au hakuna ulazima na badala yake mtapata huduma hiyo ya chakula katika sehemu husika au maalumu zinazotoa huduma hiyo ya chakula?
Je ni sehemu gani mtakapofikia kwa ajili ya kulala katika safari utalii yenu ya matembezi hifadhini au kama mtalala ndani ya hifadhi, ni lazima kubeba vifaa vyenu vilivyo vya muhimu katika kupiga kambi kama vile mahema (tents) na kadha wa kadhalika. Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (Ruaha National Parks) kunapatikana huduma kadhaa za malazi kwa ajili ya wageni watalii wa ndani na wan je. Hii ni pamoja na huduma za kupiga kambi kama vile ‘’kambi za jumuiya’’ (Public Campsites) za
‘’Camp Site No 1 & Camp Site No 2/Mdonya Public Campsite’’. Vilevile ‘’kambi maalumu’’ (Special Campsites) za ‘’Ifuguru’’, ‘’Mbagi’’, na ‘’Mdonya’’. Hali kadhalika panapatikana ‘’Nyumba Maalumu ya Wageni inayomilikiwa na Shirika’’ (Park Accommodation - COTTAGES). Pia panapatikana huduma za ‘’Kampuni za watu binafsi’’ zinazomiliki wao wenyewe kambi zao na Hotel/Lodge (Private Camps & Lodges) kama vile ‘’Mwagusi Camp’’ na ‘’Ruaha River Lodge’’. Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (Ruaha National Park) pia ina huduma za maeneo ya mapumziko ya muda mfupi (Picnic Sites) ambapo maeneo haya hutoa fursa iliyo ya kipekee kwa wageni watalii wa ndani na wa nje ya nchi ya mandhari nzuri ya kuvutia na kupendeza pindi wanapokuwa wakifurahia kutalii na kutembelea hifadhi hii. Mfano hai ni pamoja na ‘’Mbuyu Wa Fence View Point’’, ‘’Mbuni Picnic Site’’, ‘’Breakfast Point Picnic Site’’, ‘’Maganga Madungu View Point & Picnic Site’’. Huduma ya kiwanja cha ‘’ Ndege Msembe’’ pia inapatikana kwa ajili ya ndege
ndogo za watalii kutua moja kwa moja.
Je, safari utalii yenu ya matembezi hifadhini inaendeka au haiendeki? Hapo ndipo penye jibu kamili litakapofahamika. Lakini ni baada ya utaratibu mzuri kukamilika unaohusiana na maandalizi ya usafiri, huduma za chakula, tozo za viingilio na kupiga kambi, malazi au kulala kukamilika pamoja na mambo mengineyo yaliyo ya muhimu.Hii ndio dira ya safari utalii yenu Ndugu Watanzania (Wabongo)
Mawasiliano ni ya umuhimu na ya ulazima kuwepo kati ya waandaaji wa safari utalii yenu ya matembezi hifadhini Ruaha (Ruaha National Park). Mambo haya muhimu ya kimsingi ya kujiuliza ni kama vile nini kifanyike na ni nini kisifanyike? Mfano hai hakuna sababu ya msingi ya kubeba vyakula vya kujipikia wenyewe na badala yake mtafanya manunuzi mkifika ‘’Mjini Iringa’’ kuepuka vyakula kuharibika kutokana na umbali wa safari mnayosafiri. Hii itafanyika baada tu ya timu yenu ya maadalizi ya safari utalii kupata na kukusanya taarifa zilizo za umuhimu za hapa na pale za kimawasiliano. Njia nyinginezo pia ni kupitia kampuni za utalii zinazotoa huduma za utalii hifadhini Ruaha, TANAPA na vilevile ‘’Makao Makuu ya HIfadhi ya Taifa Ruaha pale MSEMBE’’.Vyanzo vya taarifa ni pamoja na ‘’tovuti na mtandao wa intaneti’’
Mambo muhimu ya kufanya na kuzingatia
(kanuni na taratibu ndani ya hifadhi)
Vifaa vyote muhimu vya huduma ya kwanza katika safari utalii ya matembezi hifadhini kubebwa. Kanuni na taratibu kuzingatiwa ni kama vile; usiendeshe chombo chako cha usafiri kama vile gari uwapo ndani ya hifadhi(Mwendo kasi unaoruhusiwa ni takribani kilometa 40 kwa saa moja; usiwabuguzi wanyamapori au kuwapigia kelele au kuleta usumbufu wa aina yeyote ile; usiwalishe chakula wanyamapori au ndege; usichume majani ya mimea au kuchuma maua na kuharibu; usitupe takataka ndani ya hifadhi au kuchafua mazingira kama vile kutupa hovyo vichungi vya sigara; wanyama wafugwao majumbani ni marufuku kabisa kuingia nao ndani ya hifadhi;usitembee peke yako hovyo uwapo ndani ya hifadhi pasipokuwa chini ya ulinzi na usimamizi wa askari wa wanyamapori; daima wakati wote bakia katika njia maalumu zilizoruhusiwa kisheria uwapo ndani ya hifadhi aidha wakati wa matembezi ya mguu au utumiaji wa gari;uwindaji viumbe hai ndani ya hifadhi ni marufuku kabisa, uchumaji sampuli wa mimea sambamba na wanyama pia ni marufuku;shughuli mbalimbali za kiutalii kawaida hufanyika baina ya muda unaoanzia saa kumi na mbili asubuhi na kumalizikia saa moja kamili ya jioni isipokuwa tu kwa wageni watalii waliopo katika kambi au lodge; usiendeshe gari lako nje ya barabara maalumu zilizowekwa na kuandaliwa ndani ya hifadhi kwa ajili ya utalii wa utazamaji wanyamapori; pesa iliyofanyiwa malipo kwa shughuli za utalii kawaida hairudishwi kabisa.
Vifaa muhimu vya kuchukua katika safari utalii hifadhini
Vifaa vyote muhimu vinavyohusiana na safari utalii yenu ya matembezi hifadhini kama vile ‘’Kamera’’’’, ‘’Vitabu mbalimbali vya mimea na wanyama’’ ‘’Video Kamera’’, ‘’Ramani’’, ‘’Viona mbali’’ (Binoculars) na kadha wa kadhalika.
Huduma za mahitaji mengineyo
Mambo ya ziada ya mahitaji yanayojitokeza na upatikanaji wake katika sehemu
husika.
Maelezo ya huduma za habari utalii wa ndani.
Kampuni ya Uelimishaji,Uratibu,Uandaaji,Uhamasishaji, na Uwezeshaji Utalii wa Ndani
Follow us:
MAWASILIANO MENGINEYO MAKAO MAKUU (TANAPA)
- Juma tatu - Ijumaa
- 8:00 Asubuhi - 4:30 Jioni
+255 272508216
info@domestictourismsafaris.c info@domestictourismsafaris.co.tz



