TALII NA TEMBELEA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO (NGORONGORO CONSERVATION AREA AUTHORITY)
Wilayani ngorongoro mkoani arusha katika ukanda wa kaskazini mwa jamhuri ya muungano wa Tanzania
Chanzo Cha Chimbuko Halisia Kimaelezo Na Ubunifu (Mwalimu Edgardo Kabulwa Welelo)
Ukweli Wa Mambo Kuhusiana Na ‘’Mamlaka Ya Hifadhi Ya Ngorongoro’’ (Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA) Wilayani Ngorongoro (Arusha); Ikumbukwe na ieleweke hapa ya kwamba ‘’Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro’’ (Ngorongoro Conservation Area Authority) ni eneo ambalo linalopatikana kijiografia ‘’Wilayani Ngorongoro’’ katika ‘’Mkoa wa Arusha’’ na pia si eneo ambalo ni ‘’Hifadhi ya Taifa’’ (National Park) na vilevile eneo hili la ‘’Ngorongoro’’ halipo chini ya Mamlaka na Uthibiti wa Shirika la Umma la Kiserikali la ‘’Hifadhi za Taifa Tanzania’’ (TANZANIA NATIONAL PARKS AUTHORITY) na badala yake ni ‘’Taasisi au Shirika la Umma’’ ambalo ni huru la kiserikali na pia lenye kuwa na ‘’Mamlaka na Uongozi’’ wake unaojitegemea kama jinsi ilivyo taasisi nyinginezo za kiserikali kama vile TANAPA,TAWA,TFS na kadha wa kadhalika ambazo kimsingi zimepewa dhamana na mamlaka ya kusimamia na kuziendeleza rasilimali na ulio urithi wetu wa mali asili nchini kwetu TANZANIA.Kazi na majukumu ya TANAPA(TANZANIA NATIONAL PARKS AUTHORITY) na NCAA (NGORONGORO CONSERVATION AREA AUTHORITY) zinafanana katika kuhifadhi viumbe hai na makazi yake kuwa endelevu kwa ajili ya vizazi vilivyopo na vijavyo. Lakini kwa upande wa ‘’Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro’’ (Ngorongoro Conservation Area Authority) yenyewe ni eneo ambalo ni ‘’Hifadhi Mseto’’ (Multiple Land Use Area) ambapo kimsingi kunapatikana ndani ya eneo lake takribani viumbe hai vya aina tatu vikiishi kwa pamoja ambavyo ‘’ni Watu ambao zaidi ni jamii ya Kabila la Wamaasai, Mifugo yao kama vile Kondoo, Mbuzi na Ng’ombe na tatu ni Wanyamapori’’.Katika maeneo ya ‘’Uhifadhi wa mali hai’’ (Protected Areas) yanayofahamika kama ‘’Hifadhi za Taifa (National Parks)’’ ambapo 40 - kimsingi,kiutaratibu,kiutawala na kikanuni maeneo haya yako chini ya mamlaka na uthibiti wa ‘’Shirika la Serikali la Hifadhi za Taifa nchini kwetu Tanzania’’ kwa kifupi ikifahamika kama (TANAPA) ni marufuku kabisa na pia hairuhusiwi mifugo ya nyumbani kama vile Ng’ombe, Mbuzi, Kondoo, na pia binadamu kuishi na kuwa na makazi ya kudumu kama jinsi ilivyo katika upande wa ‘’Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro’’ (Ngorongoro Conservation Area Authority) ambapo jamii ya kabila la Wamaasai, Mifugo yao na Wanyamapori wakiishi kwa pamoja katika eneo moja. Hivyo basi ni makosa kabisa kusema ‘’Ngorongoro ni Hifadhi ya Taifa’’ na badala yake ni sahihi kabisa kusema ‘’Ngorongoro ni Hifadhi Mseto’’ (Multiple Land Use Area).Kijiografia ‘’Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro’’(Ngorongoro Conservation Area Authority) inapakana kimipaka na ‘Wilaya ya Karatu’’(Karatu District) katika upande wake wa kusini,ambapo katika upande wake wa kaskazini inapakana kimipaka na ‘’Ardhi Tambarare zenye kutawaliwa na uoto wa asili wa mimea ya nyasi fupi na ndefu (Short and Long Grassy Plains) za ‘’Kusini Mwa Serengeti’’ (Southern Serengeti Plains), Wilaya ya Monduli (Monduli District) katika upande wake wa Mashariki na Wilaya ya Maswa (Maswa District) katika upande wake wa Magharibi kupitia ‘’Pori la Akiba la Wanyamapori la Maswa’’(Maswa Game Reserve).Kilicho cha msingi na chenye kuwa na umuhimu wa kipekee kabisa katika kujifunza na kufahamu ni ya kwamba ‘’Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro’’ (Ngorongoro Conservation Area Authority) imegawanyishwa katika kanda 4 za makazi ya mazingira ya kuishi ambapo jamii ya kifugaji ya ‘’Kabila la Wamaasai’’ wao wanapatikana wakiishi katika upande wa ‘’Magharibi na Mashariki’’ na na pia ‘’Wanyamapori’’ katika ukanda wa upande wa ‘’Kusini na Kaskazini’’ mwa ‘’Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro’’(Ngorongoro Conservation Area Authority).Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba ‘’Wilaya ya Ngorongoro’’(Ngorongoro District) kwa ujumla wake ina jumla ya tarafa 3 ambazo ni Ngorongoro, Sale pamoja na Loliondo. Mwisho kabisa na kwa upekee wake ni ya kwamba historia ya ‘’Taifa letu Tanzania’’ na pia duniani kwa ujumla wake kama chimbuko na asilia yetu ni katika eneo hili la ‘’Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro’’ kupitia katika ‘’Bonde la Oldupai’’ (OLDUVAI GORGE).Na neno ‘’NGORONGORO’’ lina maana zaidi ya moja lakini ni neno asilia ambalo limetokana ya matamshi ya lugha ya jamii ya Kimaasai katika kuongea na kutamka ikimaanisha ‘KORONGO AU BONDE’’ na hatimaye kupatikana jina ‘’NGORONGORO’’
Ushauri kwa watalii raia wa Tanzania katika kujiandaa na kujipanga kimaandalizi na kikamilifu kwa safari utalii
Mahitaji ya fedha ni kitu cha msingi na chenye kupewa kipaumbele cha kipekee na cha hali ya juu katika kuhakikisha ya kwamba safari utalii yenu ya matembezi hifadhini ‘’Mamlaka ya Ngorongoro’’ inakuwa yenye ufanisi na mafanikio
Sababu kubwa ya kimsingi na pia yenye kuwa na upekee wa aina yake ambayo ilipelekea kuanzishwa na kupatikana kwa eneo linalofahamika leo hii la ‘’Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro’’ (Ngorongoro Conservation Area Authority) ni kutokana na ukweli wa mambo ya kwamba ‘’Jamii ya Kifugaji ya Kabila la Wamaasai’’ waliishi kwa kipindi 41 - cha miaka mingi sana iliyopita ya ‘’Mababu na Mabibi Zao’’ katika maeneo yote mawili ya leo hii ya ‘’Serengeti na Ngorongoro pamoja na Wanyamapori’’. Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba kihistoria ‘’Wamaasai ni jamii ya Nailotiki (Nilotic)’’ ambao asili na chimbuko lao ni katika ‘’Taifa la Sudani Kusini’’ (SOUTH SUDAN) na ni miongoni mwa ‘’jamii ya wafugaji kiasili’’ inayoishi aina ya maisha ya kuhamahama hapa na pale na inayotegemea mifugo yao kama sehemu na utamaduni wa maisha yao. Kwa kuwa jamii ya ‘’Kabila la Wamaasai’’ iliishi ndani ya maeneo haya mawili ya uhifadhi ya ‘’Ngorongoro na Serengeti’’ kwa wakati mmoja pasipo utaratibu maalumu na mwongozo ulio rasmi kwa kipindi kirefu cha miaka mingi ya ‘’Mababu na Mabibi’’ zao, jamii hii ya ‘’kabila la Wamaasai’’ ilikuwa katika majanga makubwa yanayohatarisha maisha yao kutoka kwa wanyamapori wakali na pia mlipuko wa maradhi au magonjwa ya maambukizo ya wanyamapori na majanga mengineyo yaliyo mengi kwa kifupi. Kwa sababu hii ilipelekea ‘’Serikali ya Watawala Wakoloni Waingereza’’ wakati wa kipindi hicho kama watawala wetu wa mwisho kututawala sisi kama Taifa tukifahamika kama ‘’TANGANYIKA (Tanzania Bara)’’ kuamua kuanzisha maeneo mawili tofauti ya uhifadhi wa mali hai (Protected Areas). Eneo moja la uhifadhi litumike maalumu kwa ajili ya ‘’Uhifadhi Wa Wanyamapori Pekee’’ ambayo ndio ‘’Hifadhi ya Taifa ya Serengeti’’ (SERENGETI NATIONAL PARK) ya leo hii na vilevile eneo jingine la ‘’Uhifadhi’’ litumike kama ‘’Hifadhi Mseto (Multiple Land Use Area)’’ ambapo wamaasai wenyewe, mifugo yao pamoja na wanyamapori wakiishi kwa pamoja yaani ‘’Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro’’ (Ngorongoro Conservation Area Authority) ya leo hii jana na leo. Hatimaye ikapelekea ‘’Wamaasai’’ wote ambao waliokuwa wakiishi eneo la ‘’Serengeti’’ ya wakati wa kipindi kile wakihamishiwa kuja kuiishi katika eneo la leo hii la ‘’Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro’’ (Ngorongoro Conservation Area Authority).Vilevile malengo mengineyo ya zoezi hili ilikuwa ni katika kulinda maslahi mapana na haki ya kuishi ya jamii ya ‘’Kifugaji ya Kabila la Wamaasai’’ ambao kimsingi na kihistoria wameiishi na ‘’Wanyamapori’’ pasipo uharibifu wowote ule kwa miaka mingi sana ya ‘’Mababu na Mabibi’’ zao. Jamii ya kifugaji ya kabila la wamaasai wanachukuliwa kuwa ni ‘’Wahifadhi Asilia’’ kwa sababu ya kuishi na wanyamapori kwa muda mrefu kihistoria na inaaminika ya kwamba jamii hii inathamini sana mifugo yao na hawapendelei kula nyamapori na ndio maana wanafahamika kama ‘Wahifadhi Asilia’.Ikumbukwe na ieleweke hapa ya kwamba ‘’Shirika la Umma la Hifadhi za Taifa Tanzania’’ (TANZANIA NATIONAL PARKS AUTHORITY -TANAPA) pamoja na ‘’Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro’’ (Ngorongoro Conservation Area Authority) uanzishwaji wake wa pamoja kama taasisi za umma zinazowajibika na mamlaka na uthibiti wa rasilimali maliasili ulio urithi wetu na tunu ya Taifa kwa ajili ya vizazi vilivyopo na vijavyo ulikuwa ni katika mwaka wa 1959.Maana yake taasisi hizi ziliasisiwa kabla ya miaka miwili ya uhuru wa 42 - ‘’Tanganyika’’ (Tanzania Bara). Hii ina maanisha ya kwamba Wakoloni waliotawala Taifa letu hata kabla ya kujipatia uhuru wetu sisi wenyewe wa kujitawala nao pia walikuwa mstari wa mbele katika kuzilinda hizi rasilimali zetu kama TAIFA ukiachana na mabaya yao waliyotutendea kwa ‘’Mababu na Mabibi’’ zetu lakini pia yalikuwepo mazuri ya kiasi fulani waliyotuachia. Kijiografia, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (Ngorongoro Conservation Area Authority) inapatikana (Wilayani Ngorongoro) Mkoani Arusha katika ukanda wa kaskazini (Northern Zone) mwa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Ewe ndugu Mtanzania, jipange na jiandae sasa katika kuitembelea ‘’Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro’’.
‘’Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro’’ (Ngorongoro Conservation Area Authority) ina ukubwa wa eneo la ardhi lenye kuwa na kilometa za mraba takribani 8300 (ambapo ni sawa na maili za mraba 3200). Katika ukubwa wa jumla wa eneo lote la ardhi, ‘’Bonde la Ngorongoro’’ (Ngorongoro Crater/Collapsed Volcano/Caldera) pekee ina 43 - ukubwa wa eneo la ardhi wa takribani kilometa za ‘’Mraba zaidi ya 260 au sawa na asilimia 3’’, ‘’Msitu wa Asili wa Nyanda za Juu Kaskazini’’ (NORTHERN HIGHLAND FOREST RESERVE – NHFR) inachukua ukubwa wa eneo la ardhi takribani asilimia 20 (au sawa na takribani kilometa za Mraba 800),maeneo mengineyo yaliyobakia ya ‘’Milima (Mountains)’’ ni takribani asilimia 27, na maeneo ya ‘’Ardhi Tambarare’’ (Open Plains) yenye kutawaliwa na uoto wa asili wa mimea ya nyasi fupi na ndefu (Short and Long Grassy Plains) pamoja na ‘’Uoto wa Asili wa Miti ya Mapori na Vichaka’’ katika upande wa ‘’Kaskazini na Magharibi’’ ni takribani asilimia 50. Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba ‘’Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro’’ (Ngorongoro Conservation Area Authority) ni eneo ambalo kimsingi linapatikana katika ‘’Ukanda wa KIVOLKANO’’ (VOLCANIC BELT) nchini kwetu Tanzania na vilevile eneo hili lipo katika ‘’Ukanda wa Mnyororo wa Milima ya Volkano’’ hai, mfu na iliyodumaa ikifahamika kitaalamu kama ‘’CRATER HIGHLANDS’’.Mifano hai ni pamoja na ‘’Bonde la Ngorongoro’’ (Ngorongoro Crater/Collapsed Volcano/Caldera), ‘’Bonde la Empakaai’’ (Empakaai Crater/Caldera), ‘’Bonde la Olmoti’’ (Olmoti Crater/Caldera), Mlima pekee nchini Tanzania wenye kuwa na ‘’VOLKANO HAI’’ (Oldoinyo Lengai)/ Oldoinyo Lengai Mountain), ‘’Mlima wa tatu’’ kwa urefu nchini Tanzania ujulikanao kama (Mlima Lolmalasin) unapatikana pia katika ukanda huu na mingineyo iliyo mingi.
‘’Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro’’ (Ngorongoro Conservation Area Authority) ina ukubwa wa eneo la ardhi lenye kuwa na kilometa za mraba takribani 8300 (ambapo ni sawa na maili za mraba 3200). Katika ukubwa wa jumla wa eneo lote la ardhi, ‘’Bonde la Ngorongoro’’ (Ngorongoro Crater/Collapsed Volcano/Caldera) pekee ina 43 - ukubwa wa eneo la ardhi wa takribani kilometa za ‘’Mraba zaidi ya 260 au sawa na asilimia 3’’, ‘’Msitu wa Asili wa Nyanda za Juu Kaskazini’’ (NORTHERN HIGHLAND FOREST RESERVE – NHFR) inachukua ukubwa wa eneo la ardhi takribani asilimia 20 (au sawa na takribani kilometa za Mraba 800),maeneo mengineyo yaliyobakia ya ‘’Milima (Mountains)’’ ni takribani asilimia 27, na maeneo ya ‘’Ardhi Tambarare’’ (Open Plains) yenye kutawaliwa na uoto wa asili wa mimea ya nyasi fupi na ndefu (Short and Long Grassy Plains) pamoja na ‘’Uoto wa Asili wa Miti ya Mapori na Vichaka’’ katika upande wa ‘’Kaskazini na Magharibi’’ ni takribani asilimia 50. Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba ‘’Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro’’ (Ngorongoro Conservation Area Authority) ni eneo ambalo kimsingi linapatikana katika ‘’Ukanda wa KIVOLKANO’’ (VOLCANIC BELT) nchini kwetu Tanzania na vilevile eneo hili lipo katika ‘’Ukanda wa Mnyororo wa Milima ya Volkano’’ hai, mfu na iliyodumaa ikifahamika kitaalamu kama ‘’CRATER HIGHLANDS’’.Mifano hai ni pamoja na ‘’Bonde la Ngorongoro’’ (Ngorongoro Crater/Collapsed Volcano/Caldera), ‘’Bonde la Empakaai’’ (Empakaai Crater/Caldera), ‘’Bonde la Olmoti’’ (Olmoti Crater/Caldera), Mlima pekee nchini Tanzania wenye kuwa na ‘’VOLKANO HAI’’ (Oldoinyo Lengai)/ Oldoinyo Lengai Mountain), ‘’Mlima wa tatu’’ kwa urefu nchini Tanzania ujulikanao kama (Mlima Lolmalasin) unapatikana pia katika ukanda huu na mingineyo iliyo mingi.
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro’’ (Ngorongoro Conservation Area Authority) inafikika kirahisi kabisa umbali wa takribani kilomita 145 kwa njia ya usafiri wa barabara ukitokea katika ‘’Hifadhi ya Taifa ya Serengeti’’ (Serengeti National Park), takribani kilomita 60 ukitokea katika ‘’Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara’’ (Lake Manyara National Park), na vilevile takribani kilomita 180 mpaka 190 (au sawa na zaidi ya maili 112) ukitokea ‘’Mkoani Arusha (Arusha City)’’ (Magharibi ya Mji wa Arusha). Ni sawa na mwendo wa saa 2 mpaka 3 ukitokea Arusha. Saa 1 ukitokea ‘’Hifadhi ya Ziwa Manyara’’ na saa 2 mpaka 3 ukitokea ‘’Serengeti’’. Kijiografia ni hifadhi ambayo ipo katikati baina ya ‘’Ziwa Victoria(Nyanza), ziwa kubwa kuliko yote barani Afrika, na ‘’Mlima Kilimanjaro’’, Mlima mrefu kuliko yote katika bara la Afrika.
‘’Safu ya Milima’ yenye kuwa na Volkano mfu (Extinct/Dead Vocano/Caldera/Collapsed Volcano), hai (Active/Living Volcano) pamoja na iliyodumaa (Dormant Volcano), Msitu wa Asili wa Nyanda Juu Kaskazini (NORTHERN HIGHLAND FOREST RESERVES – NFHR), Maeneo wazi makubwa yenye kuwa na ‘’Ardhi Tambarare’ iliyotawaliwa na uoto wa asili wa mimea ya nyasi fupi na ndefu (Short and Long Grassy Plains) mchanganyiko na miti ya mapori na vichaka vya hapa na pale, na kadha wa kadhalika.
Ina anzia mita ‘’1500 mpaka 3600’’ kutoka katika usawa wa bahari.
Bonde la Ngorongoro’(Ngorongoro Crater/Collapsed Volcano/Extict Volcano/Caldera), Bonde la Empakaai (Empakaai Crater/Collapsed Volcano/Dead Volcano), Mlima Oldoinyo Lengai (Oldoinyo Lengai Mountain) ambao ndio Mlima ulio pekee nchini Tanzania ambapo Volkano yake bado ni hai(Active/Living Volcano). Bonde la Oldupai(Olduvai Gorge), sehemu ambayo ndio chimbuko na asilia ya historia yetu Tanzania na Duniani kwa ujumla wake.Bila kusahau Msitu wa Asili wa Nyanda za Juu Kaskazini (Northern Highland Forest Reserve) wenye kuwa na mandhari nzuri ya kuvutia na kupendeza. Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba ‘’Msitu huu wa Asili wa Nyanda za Juu Kaskazini’’(Northern Highland Reserve) kitafiti na kisayansi husafirisha maji yake ya chemichemi chini ya ardhi takribani mita 600 na kufikia katika ‘’Hifadhi ya Ziwa Manyara’’ (Lake Manyara National Park) na kupenyeza katika nyufa za miamba ya volkano (volcanic rocks) chini kabisa ya ‘’Ukuta wa Bonde la Ufa’’ (Escarpment/Rift Wall of the Great Rift Valley) katika upande wa ‘’Magharibi’’ mwa ‘’Hifadhi ya Ziwa Manyara’’(Lake Manyara National Park) na kutiririsha maji yake na pia kulisha ‘’Msitu wa Uhifadhi Maji Ardhini’’ (Groundwater and Riverine Forest) sambamba na ‘’Ziwa jenyewe la Manyara’’(Lake Manyara) na chemichemi za maji moto (Hot Water Sulphur Springs). Msitu huu pia ni muhimu sana kwa wananchi wakaazi wenye kuwa na mashamba wanaoishi katika wilaya za KARATU, MONDULI na MBULU kama chanzo chao muhimu kabisa cha upatikanaji maji ya kudumu kwa maisha yao ya kila siku.
Simba(Lions), Fisi Madoadoa(Spotted Hyena), Nyumbu(Western - White Bearded Wildebeest), Viboko(Common Hippopotamus/East African Hippopotamus), Swala Granti (Grant Gazelle), Swala Tomi (Thomson Gazelle), Kongoni (Coke’s Hartebeest), Ngiri(Common Warthog), Pofu(Patterson Eland/East African Eland), Pundamilia(Common/Plains/Burchell’s Zebra), Duma (Cheetah), Mbogo/Nyati(African/Savanna/Cape Buffalo), Tembo/Ndovu(African/Bush/Savanna Elephant) Madume (Ndani ya Bonde la Ngorongoro), Tembo majike na watoto nje ya Bonde la Ngorongoro (Ngorongoro Crater/Caldera). Viumbe hai ndege ni pamoja na Mbuni (Maasai Ostrich), Tandawala Mkubwa (Kori Bustard), Kanga (Helmeted Guinea Fowl),Heroe Wakubwa na Wadogo (Greater and Lesser Flamingo) na wengineo walio wengi. Vilevile Bonde la Ngorongoro (Ngorongoro Crater/Collapsed Volcano) ndio sehemu pekee zaidi nchini Tanzania unaweza kupata fursa ya kipekee kabisa kuwaona wanyamapori aina ya Faru (Black Rhinoceros) zaidi. Nje ya Bonde la Ngorongoro (Ngorongoro Crater/Caldera/Collapsed Volcano) wanyamapori Twiga 45 - (Kilimanjaro/Maasai Giraffes), Swala Pala (Impala),Kuro (aina zote mbili; Common Waterbuck na Defassa Waterbuck) na wengineo walio wengi.
‘’Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro’’(Ngorongoro Conservation Area Authority) ina aina kadhaa zilizo nyingi za uoto wa asili kama vile ‘’Msitu wa Asili wa Nyanda za Juu Kaskazini’’ (NORTHERN HIGHLAND FOREST RESERVE – NHFR), ‘’Maeneo wazi ya Ardhi Tambarare’’ yenye kutawaliwa na uoto wa asili wa mimea nyasi fupi na ndefu (Short and Long Grassy Plains), uoto wa asili wa mimea katika ardhi nusu jangwa, Mapori na kadha wa kadhalika. Katika barabara za kuteremkia chini ya Bonde na pia kutokea nje ya bonde ni ‘’Misitu ya Kitropiki ya Milimani’’ (Montane Forest). Chini ya Bonde la Ngorogoro (Crater Floor) panapatikana pia aina kadhaa za mazingira ya makazi ya uoto wa mimea kama vile ‘’Ardhi Oevu’’ (Swamps) kama vile MANDUSI na GORIGOR; chemichemi za maji (SPRINGS) kama vile SENETO, LERAI na NGOITOKTOK; Vijito vya maji (STREAMS) kama vile MUNGE na OLJORO – ONYOKIE ambavyo kwa pamoja chimbuko na asilia yake vinatokea katika mnyororo wa safu ya milima yenye kuwa na Volkano mfu, hai na iliyodumaa (Crater Highlands). Vilevile panapatikana ‘’Ziwa Magadi’’ (Makati) katikati ya bonde la Ngorongoro. Ardhi kame (ARID AREAS) pia ipo yenye kuwa na uoto wa asili wenye kutofautiana. Maeneo mengineyo ya uoto wa asili ndani ya hifadhi ni pamoja na ‘’Uoto wa Asili wa Misitu ya Mianzi ya OLDEAN(OLDEAN BAMBOO FOREST), ‘’Msitu wa Asili wa Miti ya Migunga aina ya LAHAI(ACACIA/ACHELIA LAHAI FOREST)’’, ‘’Msitu wa Asili wa Miti ya Migunga Maji’(YELLOW BARKED ACACIA FOREST) upatikanao chini ya Bonde la Ngorongoro (Ngorongoro Crater/Caldera) ambao kimsingi hutegemea ustawi wake kutokana na chemichemi za maji chini ya ardhi (Underground streams) ambapo hapa hupatikana uwezekano mkubwa wa fursa ya kujionea wanyamapori kama vile Chui(Leopards), Tembo/Ndovu(African/Savanna/Bush Elephant), Kuro(Common Waterbuck), Faru(Black Rhinoceros) na kadha wa kadhalika.
Mwezi wa Desemba mpaka Mwezi Februari. Vilevile Mwezi Mei mpaka Mwezi Julai.
Je mtakuwa na mpishi wenu maalumu wa kuwapikia chakula? Au mtajibebea vyakula vyenu wenyewe vya kujipikia? Kama ndivyo sivyo,je huduma za chakula mtazipata wapi? ‘’Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro’’ (Ngorongoro Conservation Area Authority) kijiografia ipo karibu sana jirani na ‘’Mji wa KARATU’’ katika upande wake wa Kusini ambapo sehemu nyingi zitoazo huduma za vyakula hupatikana.
Safari utalii yenu ya matembezi hifadhini ni lazima izingatie mambo muhimu kama mtalala ndani ya hifadhi (kupiga kambi au mtabeba mahema yenu wenyewe). Kama hamtalala ndani ya 46 - hifadhi, je ni mpango gani kimkakati na utaratibu upi ambao tayari umekwishaandaliwa? Hii ndio dira itakayowapatia picha halisi ya mambo kama ni kubeba vifaa vya kupiga kambi au hapana. Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba Nyumba nyingi za kulala wageni zinapatikana pia katika mji wa ‘’KARATU’’ ambao upo karibu sana jirani na lango la ‘’LODUARE’’ la kuingilia ‘’Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro’’ (Ngorongoro Conservation Area Authority). Huduma nyinginezo za malazi Hifadhini Ngorongoro ni pamoja na Hoteli za kisasa za kitalii kama vile Ngorongoro Crater Lodge, Ngorongoro Wildlife Lodge, Ngorongoro Sopa Lodge, Ngorongoro Serena Lodge, Rhino Lodge na kadha wa kadhalika. Maeneo ya kupiga kambi pia yanapatikana kama vile kambi za jumuiya (Public Campsites) na kambi maalumu (Special Campsites).Nje ya eneo la ‘’Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro’’ (Ngorongoro Conservation Area Authority) panapatikana pia huduma za malazi na kupiga kambi. Mfano hai ni pamoja na ‘’GIBBS FARM na KUDU LODGE’’.
Hii ndio dira elekezi itakayotoa picha halisi ya matokeo ya safari utalii yenu ya matembezi hifadhini.Haya yote ni baada ya kukamilisha mambo muhimu kama vile maandalizi ya usafiri, huduma za chakula, malazi au kulala na mengineyo yaliyo mengi yatakayoweza kujitokeza kama vile dharura zisizotarajiwa.
Kama mtatumia usafiri maalumu wa ‘’Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro’’ kama mpango safari utalii yenu unahusu kuteremka chini ya ‘’Bonde la Ngorongoro’’ (Ngorongoro Crater) au usafiri wenu binafsi au wa kukodisha kama unakidhi vigezo vya kuteremka chini ya bonde. Kama huduma hii haipatikani basi utaratibu mwingine uandaliwe. Kufahamu haya yote kuna ulazima wa kuwasiliana na uongozi wa ‘’Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro’’ (Ngorongoro Conservation Area Authority) kama kuna uwezekano huo upo au hapana kwa sababu gari maalumu la ‘’Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro’’ linahitaji kufanyiwa ‘BOOKING’ kwa kuwa idadi ya waombaji huwa ni wengi ikitegemea zaidi na msimu husika wa watalii. Je ni kampuni zipi za utalii (TOUR OPERATORS) mtakazozitumia ambazo nazo pia hutoa huduma kama hizo za kuteremka chini ya ‘’Bonde la Ngorongoro’’ (Ngorongoro Crater).
Mambo muhimu ya kufanya na kuzingatia
(kanuni na taratibu ndani ya hifadhi)
Watanzania raia wa Tanzania walio watalii wa ndani ni vema wakaelimishana na kujulishana miongoni mwao na pia katika makundi yao ya utalii kuhusiana na elimu ya huduma ya kwanza katika kukabiliana na changamoto zisizotarajiwa katika safari utalii zao.Sheria na taratibu ndani ya hifadhi ya kutochafua mazingira na nyinginezo zilizo nyingi zinazohusiana uhifadhi wa mazingira pamoja na viumbe hai vyake hifadhini.
Vifaa muhimu vya kuchukua katika safari utalii hifadhini
Ni pamoja na vifaa kama vile viona mbali (Binoculars), Kamera, Note Book na Kalamu,
Vitabu viongozi vya elimu viumbe hai (GUIDE BOOKS) kama vile vitabu vya ndege,
wadudu, na wanyamapori, na kadha wa kadhalika.
Huduma za mahitaji mengineyo
Ni tahadhari zitakazojitokeza katika safari utalii na namna ya kukabiliana nazo. Waswahili walisema safari sio kifo na vilevile safari ni hatua. Dharura hujitokeza. Tukabiliane nazo.
Maelezo ya huduma za habari utalii wa ndani.
Kampuni ya Uelimishaji,Uratibu,Uandaaji,Uhamasishaji, na Uwezeshaji Utalii wa Ndani
Follow us:
MAWASILIANO MENGINEYO MAKAO MAKUU (TANAPA)
- Juma tatu - Ijumaa
- 8:00 Asubuhi - 4:30 Jioni
+255 272508216
info@domestictourismsafaris.c info@domestictourismsafaris.co.tz



