TALII NA TEMBELEA HIFADHI YA TAIFAIBANDA – KYERWA (IBANDA KYERWA NATIONAL PARK
Mkoani Kagera katika ukanda wa ziwa victoria/nyanza (lake victoria region) mwa jamhuri ya muungano wa Tanzania (The united republic of Tanzania
Chanzo Cha Chimbuko Halisia Kimaelezo (Mwalimu Edgardo Kabulwa Welelo), Master of the game.
Ukweli Wa Mambo Kuhusiana Na Hifadhi Ya Taifa Ya Ibanda – Kyerwa (Ibanda – Kyerwa National Park) katika ukanda wa’’ Ziwa Victoria/Nyanza (Lake Victoria Region) mwa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania (The United Republic of Tanzania); Hifadhi hii ya Taifa ya Ibanda - Kyerwa (Ibanda - Kyerwa National Park) ilitangazwa rasmi kuwa ‘’Hifadhi ya Taifa’’ (National Park) kupitia kwa tangazo la Serikali la tarehe 5 Julai Mwaka wa 2019 Namba 509 ikiwa na ukubwa wa eneo la ardhi yenye kuwa na kilomita za mraba takribani 294. Hifadhi hii ya Taifa ya Ibanda – Kyerwa (Ibanda – Kyerwa National Park) kijiografia inapatikana ‘’Kaskazini Magharibi’’ mwa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania (The United Republic of Tanzania) na pia ndio iliyo hifadhi peeke nchini kwetu Tanzania inayopakana eneo lake la ardhi na mataifa jirani ya ‘’ Uganda na Rwanda’’. Hivyo basi mtalii wa ndani na nje ya nchi huweza kupata fursa ya kipekee ya kuweza kujionea ‘’Mataifa Matatu’’ akiwa amesimama katika eneo moja ndani ya ‘’Hifadhi ya Taifa ya Ibanda – Kyerwa’’.
Ushauri kwa watalii raia wa Tanzania katika kujiandaa na kujipanga kimaandalizi kwa safari utalii
Ni pamoja na utumiaji wa usafiri wa Anga kupitia viwanja vya ndege vya ‘’Bukoba na Chato’’ ambapo ndege ndogo zinaweza kutua kwenye ‘’Kijiji cha Ibanda’’ au ndani ya kiwanja kilichopo ndani ya hifadhi. Vilevile kwa njia ya usafiri wa barabara: Hifadhi inafikika kupitia ‘’Mji wa Bukoba’’ hadi ‘’Murongo’’ takribani kilomita 221 au kutokea ‘’Chato’’ hadi ‘’Murongo’’ takribani kilomita 441. Pia hifadhi inafikika kutokea ‘’Nchini Uganda’’ kupitia mpaka wa kimataifa unaotambulika wa ‘’Murongo’’ ambapo ni sawa takribani kilomita 4 kutokea ‘’Makao Makuu ya Hifadhi’’.
Hifadhi hii ya Taifa ya Ibanda – Kyerwa ina misimu miwili ya mvua ambapo ‘’Mvua za vuli’’ (Mvua kidogo/ Short Rainy Season) huanzia katika ‘’Mwezi Oktoba hadi Mwezi Novemba’’ na msimu wa mvua za masika (Mvua nyingi/Long Rainy Season) ambapo kawaida huanzia katika ‘’Mwezi Machi hadi Mwezi Mei’’. Msimu wa Kiangazi (Dry Season) kawaida huanzia katika ‘’Mwezi Juni hadi Mwezi Oktoba’’ na pia kuanzia ‘’Mwezi Januari hadi Mwezi Februari’’. Maeneo ya hifadhi hupata wastani wa mvua mililita 700 hadi mililita 1000 kwa mwaka. Wastani wa hali joto ni kati ya nyuzi joto 13 hadi 26
hifadhi hii ya taifa ya ibanda – kyerwa (ibanda – kyerwa national park) imebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya utalii na miongoni mojawapo ya hivyo vivutio ni pamoja na nyika, mito na ardhi oevu ambavyo ni makazi ya wanyamapori wa aina mbali mbali
Ni pamoja na Nyati/Mbogo (Savanna/ Cape/ African Buffalo) wakiwa kwenye makundi, Viboko (Common Hippopotamus/East African Hippopotamus), Nyani (Savanna Baboon/ Anubis Baboon), Chui (Leopards) na vilevile ‘’Wanyamapori Swala’’ wa aina mbalimbali wote hawa wanaifanya safari utalii yako isiwe ya kusahaulika ndugu mtanzania mtalii wa ndani
Ni pamoja na Nyati/Mbogo (Savanna/ Cape/ African Buffalo) wakiwa kwenye makundi, Viboko (Common Hippopotamus/East African Hippopotamus), Nyani (Savanna Baboon/ Anubis Baboon), Chui (Leopards) na vilevile ‘’Wanyamapori Swala’’ wa aina mbalimbali wote hawa wanaifanya safari utalii yako isiwe ya kusahaulika ndugu mtanzania mtalii wa ndani
Kwa ujumla wake mikoa ya ukanda wa ‘’Ziwa Victoria’’ nchini kwetu Tanzania ina uoto wa asili ulio maalumu unaofahamika kama ‘’Lake Victoria Region Vegetation Zone’’. Hivyo basi kuwepo kwa aina nyingi za uoto wa asili kuanzia nyika za miti ya migunga, milima na mabonde, mito na tambarare zinaifanya hifadhi hii kuwa na mandhari mazuri ya kuvutia na kupendeza hivyo kuwapa watalii fursa nzuri ya kujionea aina hizi tofauti za uoto wa asili.
- UTAZAMAJI WA WANYAMAPORI;
Kama mojawapo ya hifadhi yenye kuwa na makazi ya nyika ya savana, milima, mto Kagera na mabonde; vyote hivi vikiwa na wanyamapri wa aina mbalimbali, utalii wa utazamaji wanyamapori ni wa kipekee kwani utaweza kujionea wanyamapori kama vile nyati/mbogo, chui, viboko, swala wa aina mbalimbali, nyani na kima.
- MATEMBEZI YA MIGUU HIFADHINI
Aina hii ni ya utali humsaidia mgeni mtalii kuwa karibu zaidi na wanyamapori na kuweza kujifunza zaidi tabia na maisha yao ya porini. Zipo njia mbalimbali zinazotumika kwa ajili ya utalii huu ambapo utaongozwa na askari wa hifadhi mwenye silaha kwa ajili ya kulinda usalama.
- MALAZI NA HUDUMA KWA WAGENI WATALII’
Ni pamoja na maeneo ya kupiga kambi ambapo mtalii anapotembelea hifadhi hii huweza kupiga mahema na kuweza kulala kwenye mazingira mazuri huku usiku ukisindikzwa na sauti za wadudu na wanyamapori hivyo kufanya usiku wako kuwa mzuri na wa kipekee.
- Wageni ni lazima kuwa na kibali kinachotumika wakati wote ndani ya saa 24
- Hairuhusiwi kuwinda, kuchukua mnyama au mmea wa aina yoyote hifadhini
- Ni marufuku kutupa taka hifadhini
- Tumia barabara na njia zilizoruhusiwa na uongozi
- Usichome au kuanzisha moto hifadhini
- Hairuhusiwi kubughudhi wageni wengine kwa namna yoyote uwapo hifadhini
- Hairuhusiwi kufanya utalii hifadhini kati ya saa 1:00 jioni hadi saa 12:00 asubuhi,isipokuwa kwa kibali maalum
- Hairuhusiwi kuingia na wanyama wa kufugwa hifadhini
- Hairuhusiwi kuendesha gari kwa mwendo kasi zaidi ya kilometa 50 kwa saa
- Mwendokasi unaruhusiwa kwa ajili ya kuangalia wanyama ni kilometa 25 kwa saa
- Hairuhusiwi kupiga kelele, kupiga honi au kupiga muziki hifadhini
- Hairusiwi kulisha wanyamapori
Maelezo ya huduma za habari utalii wa ndani.
Kampuni ya Uelimishaji, Uratibu, Uandaaji, Uhamasishaji na Uwezeshaji Utalii wa Ndani na Mazingira,
Follow us:
MAWASILIANO MENGINEYO MAKAO MAKUU (TANAPA)
- Juma tatu - Ijumaa
- 8:00 Asubuhi - 4:30 Jioni



