TALII NA TEMBELEA HIFADHI YA TAIFA TARANGIRE

Mkoani Manyara (wilayani Babati) katika ukanda wa kaskazini mwa jamhuri ya muungano wa Tanzania

Chanzo Cha Chimbuko Halisia Kimaelezo Na Ubunifu (Mwalimu Edgardo Kabulwa Welelo)

Ukweli Wa Mambo Kuhusiana Na Hifadhi Ya Taifa TARANGIRE Mkoani Manyara; Hifadhi ya Taifa ya Tarangire (Tarangire National Park) ipatikanayo kijiografia katika ukanda wa kaskazini mwa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mkoani Manyara (Wilayani Babati) ilijipatia jina lake hilo kutokana na ‘Mto Tarangire’ (Tarangire River) ambao kimsingi chanzo chake na asili yake cha maji ya mto huu kimeanzia maeneo ya Nyanda za Juu Kondoa (Wilayani Kondoa) katika Mkoa wa Dodoma, katikati kabisa ya nchi yetu Tanzania.Urefu wa Mto Tarangire ni takribani kilomita 120, na vile vile sehemu mojawapo ya mkondo wa mto huu Tarangire hutiririsha maji yake ya mto kuelekea uelekeo wa maeneo ya Nguselororobi pamoja na Larmakau, wakati ambapo sehemu nyingine ya mkondo wa Mto Tarangire hutiririsha maji yake ya mto kuelekea uelekeo wa Ziwa Burungi. Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba vyanzo vinginevyo vya habari na maelezo vinaelezea ya kwamba chimbuko halisia ya neno au jina ‘Tarangire’ limetokana na maneno mawili ambayo ni ‘TARA’ ikimaanisha ‘MTO’ na ‘NGIRE’ ikimaanisha ‘NGIRI’. Tafsiri kamili ikimaanisha ‘Mto wa Ngiri’ kutoka katika mojawapo ya makabila yanayozunguka na kuishi maeneo haya ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire. Miongoni mwa jamii za makabila yanayopatikana yakiishi na kuzunguka hifadhi hii ni pamaja na makabila ya Wambugwe, Wamaasai, Wadatooga na kadhalika. Wakati wa msimu wa kiangazi katika Mwezi Julai mpaka Mwezi Novemba huwa ni maskani ya makazi kwa maelfu na maelfu ya wanyamapori wahamao katika makundi kama vile Tembo 2 - (Elephants), Pundamilia (Zebras), Nyumbu (Wildebeests), na wengineo walio wengi wahamaji wakivutiwa na chanzo cha maji ya ‘Mto Tarangire’ kwa ajili ya kunywa maji na kukata kiu chao cha maji. Lakini wakati wa kipindi cha msimu wa mnvua za masika unapowadia karibia sehemu kubwa ya wanyamapori Hifadhini Tarangire kawaida huondoka na kuweza kupatikana nje ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na pia katika mazingira ya makazi ya jamii za makabila mbalimbali zinazoishi kuzunguka hifadhi hii. Mojawapo ya sababu ya kimsingi kitaalam na kisayansi ya wanyamapori Hifadhini Tarangire kuhama na kuondoka nje ya hifadhi wakati wa kipindi cha mnvua za masika ni ya kwamba nje ya hifadhi wakati wa kipindi hiki hupatikana chakula cha kutolesha cha mimea nyasi chenye kuwa na kirutubisho zaidi na vile vile madini ya chunvi kwa ajili ya kujenga na kuimarisha miili yao tofauti kabisa na jinsi inavyokuwa ndani ya hifadhi.

Ushauri kwa watalii raia wa Tanzania katika kujiandaa na kujipanga kimaandalizi na kikamilifu kwa safari utalii;

t (34 of 189)

Watanzania wazalendo watalii wa ndani ni lazima watambue ya kwamba fedha zinahitajika katika maandalizi ya usafiri na upatikanaji wake unahitaji mipango yenye kuwa na mikakati makini. Watalii wa ndani waanze na bajeti ya mahitaji ya fedha na makadirio ya gharama za safari utalii ya matembezi hifadhini. Bajeti ya mahitaji ya fedha izingatie kwa umakini mkubwa mtiririko wa mambo yafuatayo kama vile huduma za malazi au kulala, viingilio hifadhini, ghrama za kupiga kambi, chakula, usafiri na mahitaji mengineyo muhimu yanayoweza kujitokeza kama vile dharura.

 Hifadhi ya Taifa ya Tarangire (Tarangire National Park) ilianzishwa rasmi mnamo mwaka wa 1970. Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba kabla ya kuanzishwa kwake kama Hifadhi ya Taifa hapo awali ilikuwa ni mojawapo ya eneo la pori la akiba la wanyamapori maarufu kwa shughuli za uwindaji wa wanyamapori kwa kibali maalumu kinachoruhusu uwindaji. Uamuzi wa busara wa uanzishwaji wake kama Hifadhi ya Taifa ulikuwa ni kulinda na kuhifadhi viumbe hai wanyamapori, ndege, uoto wa asili na mazingira yake katika kuvinusuru katika kutoweka. Leo hii Hifadhi ya Taifa Tarangire ni mojawapo ya vivutio maarufu na pia yenye kuvutia maelfu na maelfu ya watalii wa ndani na wa nje ya nchi katika ukanda wa kaskazini mwa Janhuri ya Muungano wa Tanzania, Afrika na ulimwenguni kote kwa ujumla wake. Ndani ya Hifadhi ya Taifa Tarangire panapatikana sura za maumbile ya kijiografia mbalimbali kama vile uoto wa asili hususani miti mikubwa ya Mibuyu (Baobabs), Mto Tarangire, Ardhi Oevu kama vile Silale, Maeneo wazi tambarare, Miamba ya ardhini katika uso wa ardhi (Kopjes/Rocky Outcrops), Ziwa Burungi (Lake Burungi), bila kusahau 3 - mtawanyiko wa vilima vya hapa na pale kama vile OLDONYO NGAHARI, KALIMA, SANGAIWE, HAIDEDONGA pamoja na KITIBONG. Njia au barabara za utalii hifadhini huwasaidia na kuwawezesha watalii wa ndani na watalii wa nje kuweza kujionea wenyewe vivutio vya utalii mbalimbali kama vile wanyamapori na ndege. Mfano hai, kaskazini mwa lango la kuingilia Hifadhi ya Taifa Tarangire utakuna na njia au barabara elekezi za utalii kupitia vibao vyenye kuwa na majina kuelekea sehemu husika ya kujionea vivutio sambamba na maeneo mengineyo yaliyobakia hifadhini.

Hifadhi ya Taifa ya Tarangire (Tarangire National Park) ina ukubwa wa eneo la ardhi yenye kuwa na takribani kilometa za mraba 2850 (hii ikijumuisha pamoja na Ziwa Burungi kama mojawapo ya sehemu ya eneo lake la uhifadhi).

Hifadhi ya Taifa ya Tarangire (Tarangire National Park) inafikika kirahisi kabisa kwa njia ya usafiri wa barabara umbali wa takribani kilomita 120 ukitokea Kusini Magharibi mwa Mji wa Arusha (Arusha City) katika barabara kuu ya Arusha – Dodoma. Vile vile ni sawa na umbali wa takribani kilomita 95 ukitokea Kusini Mashariki mwa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara (Lake Manyara National Park). Inapatikana pia umbali wa takribani kilomita 155 ukitokea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (Ngorongoro Conservation Area Authority) na vile vile ni umbali wa takribani kilomita 300 ukitokea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti(Serengeti National Park). Ni sawa na umbali wa saa moja kutokea Arusha Mjini (Arusha City) na saa 3 mpaka 4 kutokea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (Serengeti National Park). Pia ndege ndogo za kukodisha (charter flights) zitoazo huduma za usafiri wa anga kwa hifadhi za ukanda wa kaskazini kwa ujumla wake zinapatikana katika kiwanja kidogo cha ndege Arusha (Arusha Airstrip).

Ni pamoja na Mto Tarangire, Kanda (8 mpaka 9) za Uoto wa asili (Vegetational zones), Maeneo yenye kuwa na ardhi oevu (Swamps), Vilima (Hills) na Miamba ya Ardhini (Rocky – outcrops/Kopjes) pamoja na miti mingi ya Mibuyu (Baobabs) iliyotawanyika sana sehemu mbalimbali hifadhini.

Ina anzia mita 1200 mpaka 1600 kutoka usawa wa bahari. Msimu wa kipindi cha mvua Hifadhini Tarangire ni pamoja na mvua za vuli (short rains) katika kipindi cha kuanzia Mwezi Oktoba na Mwezi Desemba ikifuatiwa na kipindi kifupi cha hali ya kiangazi cha ukame katika 4 - Mwezi wa Januari. Mvua ndefu za Masika (Long rains) kawaida huanzia katika kipindi cha Mwezi Februari mpaka Mwezi Juni. Kiwango cha wastani wa mvua mwaka mzima Hifadhini Tarangire ni takribani milimita 650 wakati ambapo kiwango cha mvua cha hali ya juu kabisa katika mwaka hutokea Mwezi Aprili. Ni vema ikakumbukwa na ikaeleweka ya kwamba Hifadhi ya Taifa ya Tarangire (Tarangire National Park) inapatikana kijiografia katika ukanda wa uoto wa asili wa maeneo ya ukame na pia nusu jangwa (Somali – Maasai Region) na pia Hifadhi ya Taifa Tarangire inapatikana katika ukanda wa upande wa Bonde la Ufa la Mkondo wa Mashariki (Eastern or Gregory Rift) na hii inathibitishwa zaidi kupitia Ziwa Burungi kama mojawapo ya maziwa yaliyotokana na Bonde Kuu la Ufa kupita kama vile Ziwa Natron, Eyasi, Manyara, na Babati. Hifadhi hii ya Taifa ya Tarangire kawaida hupata kiwango kidogo cha mvua takribani milimita (300 mpaka 700) za mvua kwa mwaka kwa sababu pia ya kupatikana kwake kijiografia katika upande wa ukanda wa Mkondo wa Bonde la Ufa la Mashariki. Kiwango cha juu cha joto kawaida huanzia Mwezi Desemba mpaka Mwezi Februari na kiwango kidogo cha joto kawaida ni Mwezi Juni na Mwezi Julai. Kiwango cha juu cha joto kawaida ni takribani nyuzi joto 27 wakati ambapo kiwango cha joto la wastani ni nyuzi joto 16.

Eneo la mazingira ya makazi ya miti ya migunga mwanvuli (Acacia tortilis parkland/Umbrella Thorns), Chatu Wapandao Juu ya Miti katika eneo la Larmakau (Tree Climbing Pythons), Makundi Makubwa ya Wanyamapori Tembo/Ndovu (Elephant Concentrations), Mto Tarangire (Tarangire River), Maeneo mbalimbali yenye kuwa na Ardhi Oevu (Swamps) kama vile Silale, Miti Mikubwa ya Mibuyu (Baobabs), aina mbalimbali za viumbe hai ndege ambao wanakadiriwa kitafiti na kisayansi kufikia spishi za ndege takribani 550. Miongoni mwao walio maarufu ni kama vile Mbuni (Maasai Ostrich) na Mumbi (Southern Ground Hornbills) na pi sura au taswira ya kijiografia ya mandhari nzuri ya maeneo yenye kupendeza na kuvutia.

Ni pamoja na Wanyamapori kama vile Tembo/Ndovu (African/Savanna/Bush Elephants), Pundamilia (Plains/Burchell’s/Common Zebra), Nyati/Mbogo (African/Savanna Buffalo), Swala Pala (Impala), Twiga (Maasai/Kilimanjaro Giraffe), Nyani (Olive/Savanna Baboon), Ngedere/Tumbili (Black –faced Monkeys), Swala tomi (Thomson Gazelle), Swala granti (Grant Gazelle), Kuro (Common Waterbuck), Mbweha Masikio (Bat – eared fox), Simba (Lions), Chui (Leopards), Choroa (Fringe – eared Oryx), Kongoni aina ya Cokei (Coks Hartbeest), Nyumbu (Western – white bearded wildebeest), Pofu (Patterson Eland/East 5 - African Eland),Tohe (Bohor Reedbuck),Digidigi/Saruya(Kirk’s dik dik),Tohe Mlima (Mountain Reedbuck), aina mbalimbali za Mbweha (Jackals), Pimbi Pori (Bush Hyraxes), Pongo (Bushbucks), Swala Twiga (Gerenuks), Ngiri (Common Warthog), Duma (Cheetah), Tandala Mdogo (Lesser Kudu), Tandala Mkubwa (Greater Kudu), Fisi Madoamadoa (Spotted Hyenas), na wengine walio wengi. Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba Hifadhi ya Taifa ya Tarangire (Tarangire National Park) ina zaidi ya spishi takribani 550 za viumbe hai ndege kuweza kurekodiwa na kuripotiwa kitafiti na kisayansi. Miongoni mwa viumbe hai ndege ambao huonekana mara nyingi na mara kwa mara ni pamoja na Ndege Mbuni (Maasai Ostrich), Mumbi (Southern Ground Hornbills), Fundi Chuma/ Msingwa (Hammerkop/Hammerhead), Korongo Domo Ganzi (Saddle - Billed Stork), Bata – Bukuni (Egyptian Goose), Kibilinzi (African Jacana),Taji/Korongo – Taji (Grey Crowned Crane), Chole (Lilac – Breasted Roller), Kanga (Helmeted Guinea Fowl), Karani/Ndege Kilemba (Secretary Bird), Mwezi – Maridadi (Superb Starling), YangeYange (Cattle Egret), Kuzi Kijivu (Ashy Starling), Kukutanda Zambarau (Purple Gallinule) na wengineo walio wengi sana.

Hifadhi ya Taifa ya Tarangire (Tarangire National Park) ina takribani kanda (8 mpaka 9) za maeneo yenye kutofautiana ya uoto wa asili. Watalii raia wa Tanzania wanapotembelea na kutalii ndani ya hifadhi huweza kujionea wenyewe kwa macho yao vibao elekezi vya majina vinavyotambulisha maeneo haya ya uoto wa asili kikanda kupitia njia au barabara za utalii hifadhini. Maeneo haya ya kikanda ya uoto wa asili yana anzia kaskazini mwa lango la kuingilia Hifadhi ya Taifa Tarangire kuelekea uelekeo wa kusini mwa hifadhi yenyewe. Kuanzia kaskazini mwa hifadhi kuelekea kusini mwa hifadhi, maeneo haya ni pamoja na Lemiyoni (Kaskazini), Matete (Kusini Mashariki mwa Lemiyoni), Burungi (Kaskazini Magharibi), Kitibong (Kusini Magharibi mwa Burungi), Gursi na Larmakau (Maeneo haya mawili yanakamilisha kwa ujumla wake eneo lote la katikati ya Hifadhi, ambapo Gursi ni katika upande wa kati Magharibi na Larmakau ni upande wa kati Mashariki, Larmakau ni maskani ya chatu wapandao juu ya miti), Nguselororobi na Mkungunero yanakamilisha kwa ujumla wake kama sehemu ya kusini mwishoni kabisa mwa Hifadhi ya Taifa ya Tarangire ambapo kawaida hupatikana aina mbalimbali za mazingira ya makazi kama vile maeneo wazi tambarare ya uoto wa mimea nyasi(Open Plains), uoto wa asili wa miti ya mapori (woodlands), ardhi nyeusi iliyotawaliwa na uoto wa mimea nyasi na pia yenye kuwa na rutuba inayopasukapasuka (Black Cotton Grasslands) pamoja na ardhi oevu (Swamps) kama vile Silale. Kijiografia, Hifadhi ya Taifa ya Tarangire (Tarangire National Park) inapatikana katika eneo la uoto wa asili wa maeneo makame pamoja na nusu jangwa (Somali- Maasai 6 - Region) wenye kutawaliwa na uoto wa asili wa mimea wa miti ya Migunga (Acacia/Acheli) na Mbabara au Mturituri(Commiphora), Mibuyu (Baobabs),Vichaka vya hapa na pale (Thickets) na maeneo wazi yaliyotawaliwa na uoto wa nyasi (Grassland/Open Plains Grass). Ikumbukwe na ieleweke kwa Watanzania wazalendo watalii wa ndani ya kwamba ukanda huu wa uoto wa asili hupata mvua kidogo sana kwa mwaka baina ya milimita 300 mpaka 700. Miongoni mwa jamii nyinginezo za mimea miti ipatikanayo hifadhini Tarangire ni kama vile Mlegea/Mwegea (Sausage tree), Mkwaju (Tamarind), Mjunju (Desert date), Mgunga Mwanvuli (Umbrella thorn), Mgunga Maji (Yellow Barked Acacia), Mtonvu (Candelabrum trees) na kadha wa kadhalika.

Mwezi wa Desemba mpaka Mwezi Julai kwa ajili ya kujionea na kushuhudia ‘’Msafara  wa Uhamaji wa Wanyamapori’’ kama vile  Nyumbu  na Wanyamapori  wengineo walio wengi. Vilevile   Mwezi wa Juni  mpaka  Mwezi Oktaba kwa ajili ya kujionea  ‘’Wanyamapori Wawindaji na Walao Nyama (Predators)’’  kama vile  Simba (Lions), Chui (Leopards), Fisi Madoadoa (Spotted Hyenas),  Duma (Cheetah) na wengineo walio  wengi.

Je, mtajibebea vyakula vyenu wenyewe? Au mtapata huduma za chakula katika sehemu au
maeneo mliyopo yanayotoa huduma hizo?

Safari utalii yenu ya matembezi hifadhini ni lazima izingatie kwa umakini mkubwa huduma za malazi au kulala. Kama safari utalii yenu ya matembezi hifadhini ni ya kulala ndani ya hifadhi, je mnayo mahema ya kupiga kambi? Na kama hamna hayo mahema ni sehemu gani mtayapata au kuyakodi? Kama hamtalala ndani ya hifadhi, je, ni sehemu gani za nyumba za kulala wageni mtafikia? Haya yote yatategemea na hali halisi ya safari utalii yenu ya kimatembezi hifadhini jinsi au namna ilivyopangiliwa. Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba Hifadhi ya Taifa ya Tarangire (Tarangire National Park) panapatikana huduma kadhaa za malazi au kulala. Mfano hai ni pamoja na Hoteli ya Kitalii ya Tarangire Safari Lodge (Tarangire Safari Lodge) ambayo kimsingi ina vitanda vya kulaza wageni watalii takribani 84, Hoteli ya Kitalii ya Tarangire Sopa Lodge (Tarangire Sopa Lodge) yenye kuwa na vitanda takribani 150 vya kulaza wageni watalii. Pia huduma za malazi ya kambi za jumuiya (Public campsites) na kambi maalumu (Special campsites) zinapatikana katika kuhudumia maelfu na maelfu ya watalii wa ndani na wan je ya nchi.

Gharama za usafiri wote zitakamilika na kufahamika baada ya mchakato mzima wa
mtiririko wa mambo muhimu ya kimsingi kama vile maandalizi ya usafiri, huduma za
7 - chakula, malazi au kulala, usafiri wenyewe pamoja na huduma za mahitaji mengineyo
muhimu yatakayojitokeza

Je safari utalii yenu ya matembezi hifadhini ni ya siku ngapi? Kama safari utalii yenu ya matembezi hifadhini ni ya siku moja, je kuna una ulazima wowote ule wa kubeba vyakula vyenu wenyewe vya kujipikia au hakuna ulazima huo? Na kama safari utalii yenu ya matembezi hifadhini ni zaidi ya siku moja bila shaka kuna ulazima wa kubeba vifaa vyote muhimu kama vile mahema, vyakula pamoja na mahitaji mengineyo yaliyo ya muhimu.

Mambo ya kufanya na kuzingatia (kanuni na taratibu ndani ya hifadhi

Ikiwezekana kwa hali yeyote ile katika safari utalii ya matembezi hifadhini kuwa na utamaduni wa kubeba boksi la huduma ya kwanza kwa ajili ya dharura ambazo hazitabiriki. Kanuni na taratibu ndani ya hifadhi ni muhimu kuzingatiwa na watalii wote wa ndani katika kuepuka faini ambazo si za ulazima. Mfano hai, mazingira mliyoyakuta hifadhini ni safi, msiyaache mazingira hifadhini yakiwa machafu.

Wananchi watalii wa ndani wanawajibika kuzingatia na kuzitekeleza kanuni na taratibu hifadhini kama vile; ◦Ni marufuku kuwapa vyakula viumbe hai wanyamapori. ◦Kutoka nje ya usafiri wa gari isipokuwa tu katika yale maeneo yaliyoruhusiwa. ◦Kuingia na silaha ndani ya hifadhi ni marufuku. ◦Kuwa ndani ya hifadhi kabla ya saa 12:00 asubuhi na baada ya saa 1:00 jioni, isipokuwa tu kwenye maeneo ya kulala wageni, au kambi maalumu au kambi za jumuiya.

Mkomazi4

Vifaa muhimu vya kuchukua katika safari utalii hifadhini

Ni kama vile vitabu vya viongozi (Guide books), kama vile vitabu vya elimu viumbe hai vya mimea, wanyamapori pamoja na ndege. Vile vile viona mbali (Binoculars), Kamera, Daftari dogo, pamoja na vifaa vinginevyo muhimu katika matembezi hifadhini.

Huduma za mahitaji mengineyo

Ni mambo ya ziada ya mahitaji yatakayojitokeza na upatikanaji wake katika sehemu husika mlipo katika safari utalii yenu ya matembezi hifadhini.

Maelezo ya huduma za habari utalii wa ndani.

MAWASILIANO MENGINEYO MAKAO MAKUU (TANAPA)

+255 272508216

info@domestictourismsafaris.c  info@domestictourismsafaris.co.tz