WASIFU WA MAMA TANZANIA (JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA/THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA)
Chanzo Cha Chimbuko Halisia Kimaelezo Na Ubunifu (Mwalimu Edgardo Kabulwa Welelo)
Ukweli Wa Mambo Kuhusiana Na ‘’Historia Ya Tanzania Yetu Sote’’ (Nchi ya Tanganyika pamoja na Nchi ya Visiwa Vya Zanzibar) ‘’Jamhuri ya Muungano ya Tanzania’’, (The United Republic of Tanzania) ni ‘’Muungano wa Mataifa mawili’’, ambayo ni ‘’Taifa la Tanganyika’’ (Tanzania Bara) pamoja na ‘’Taifa la Visiwa Vya Zanzibar’’ (Tanzania Visiwani) ambavyo kimsingi ni mkusanyiko wa visiwa vikubwa viwili vya PEMBA na UNGUJA (ZANZIBAR) na pia visiwa vinginevyo vidogo vidogo kadhaa takribani zaidi ya 50 vipatikanavyo katika pwani ya mwambao wa ‘’Bahari ya Hindi’’ (Indian Ocean). Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba ‘’Visiwa Vya Zanzibar’’ vina eneo dogo la ardhi lenye kuwa na ukubwa wa kilometa za mraba takribani 2,600 inayohusisha visiwa viwili vikubwa vya ‘’Pemba na Unguja’’. Tanganyika (Tanzania Bara)kwa upande mwingine ina ukubwa wa eneo la ardhi lenye kuwa na ukubwa wa kilometa za mraba takribani zaidi ya 945,000. Mataifa haya mawili (Nchi ya Tanganyika na Nchi ya Visiwa Vya Zanzibar) yaliungana rasmi mnamo tarehe 26 Aprili ya mnamo mwaka wa 1964 na kuunda ‘’Jamhuri ya Muungano ya Tanzania’’ (The United Republic of Tanzania)
Jamii Ya Makabila Mbalimbali Yapatikanayo ‘’Nchini Kwetu Tanzania’’ (Jamhuri Ya Muungano Ya Tanzania (The United Republic of Tanzania)
Tanzania) kunapatikana zaidi ya makabila 130 karibia nchi nzima (Tanganyika pamoja na visiwa vya Zanzibar). Kabila kubwa kuliko makabila yote ‘’nchini kwetu Tanzania’’ ni kabila la ‘’Wasukuma’’ wakati ambapo kabila la ‘’Wanyamwezi’’ni kabila la pili kwa ukubwa na ‘’Wachagga’’ ni kabila la tatu kwa ukubwa. Katika ‘’Visiwa vya Zanzibar’’, kabila kubwa zaidi kuliko yote visiwani humo ni kabila la ‘’Washirazi’
Imani za kidini na kiroho ni pamoja na ‘’Dini Ya Kiimani Ya Kikristo’’ yenye kuwa na madhehebu mbalimbali, na vilevile ‘’Dini Ya Kiimani Ya Kiislamu’’ yenye kuwa pia na madhehebu kadhaa na pia vilevile ‘’Dini Za Kiimani Za Kijadi Na Mila Za Kiafrika’’. Katika ‘’Nchi Ya Visiwa Vya Zanzibar’’, dini ya Kiislamu ndiyo iliyo kubwa zaidi na pia yenye kuwa na waumini wengi sana kuliko dini nyinginezo za kiimani.
‘’Jamhuri ya Muungano ya Tanzania’’ (The United Republic of Tanzania) imegawanyishwa katika ‘’mikoa takribani 31’’ mpaka hivi sasa, wakati ambapo ‘’Visiwa Vya Nchi Ya Zanzibar’’ vina jumla ya ‘’Mikoa Mitano (5)’’ ambayo ni ‘’Kaskazini Pemba’’, ‘’Kusini Pemba’’, ‘’Kaskazini Unguja’’, ‘’Kusini Unguja’’, pamoja na ‘’Mjini Magharibi’’. Nchi ya Tanganyika (Tanzania Bara)ina jumla ya ‘’Mikoa’’ takribani ‘’Ishirini Na Sita (26)’’. Ikumbukwe na ifahamike ya kwamba mpaka ilipofikia ‘’Mwezi Machi – 2012’’, kulikuwepo na ‘’Mikoa 21’’ katika upande wa ‘’Nchi Ya Tanganyika’’ (Tanzania Bara) pale ambapo mikoa mingineyo mipya ilipoongezwa na pia kutangazwa rasmi kupitia ‘’Tangazo La Gazeti La Serikali’’ ambayoni ‘’GEITA’’, ‘’KATAVI’’, ‘’NJOMBE’’, pamoja na ‘’SIMIYU’’ na pia miaka ya hapa karibuni mnamo mwaka wa 2016, ‘’Mkoa wa SONGWA’’, ukatangazwa kama mkoa mpya baada ya kumegwa na kutenganishwa kutoka katika ‘’Mkoa wa MBEYA’’. Mkoa wa ‘’TABORA’’, nchini kwetu Tanzania (‘’Tanganyika’’ pamoja na ‘’Visiwa V ya Zanzibar’’) ndio mkoa ulio pekee wenye kuwa na eneo la ardhi kubwa zaidi kuliko mikoa yote Tanzania ambapo eneo lake la ardhi ni takribani kilometa za mraba 76,151, ikifuatiwa kwa ukaribu kieneo katika ukubwa na ‘’Mkoa wa MOROGORO’’, ukifahamika katika jina lake la utani kama ‘MJI KASORO BAHARI’’
Tanganyika (Tanzania Bara) ilijipatia uhuru wake kamili wa madaraka wa kujitawala wenyewe mnamo tarehe 9 Desemba ya mwaka wa 1961, chini ya uongozi wa waziri mkuu wa kwanza ‘’Hayati Baba Wa Taifa’’ na vilevile ‘’Muasisi’’ wa ‘’Taifa Letu Mama Tanzania’’, ‘’Mwalimu Julius Kambarage Nyerere’’ na mnamo mwaka wa 1962, Tanganyika (Tanzania Bara) ikawa Jamhuri na ‘’Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akawa Rais’’.
Nchi ya ‘’Visiwa Vya Zanzibar’’ vilijipatia uhuru wake mnamo tarehe 10 Desemba ya mwaka wa
1963 kutoka katika ‘’ Milki na Utawala wa Mkoloni Muingereza’’, chini ya utawala wa kimla wa
‘’Sultan Jamshid bin Abdullah’’, ambapo uhuru rasmi wa kujitawala na kujiongoza wao wenyewe
ulipatikana kwa njia ya ‘’Mapinduzi’’ katika umwagaji wa damu kwa kumng’oa kutoka
madarakani ‘’Sultan Jamshid bin Abdullah’’ mnamo tarehe 12 Januari ya mwaka wa 1964, na
baadaye ‘’Nchi ya Visiwa Vya Zanzibar’’ ikaungana rasmi na ‘’Nchi Ya Tanganyika’’ (Tanzania
Bara) na kupelekea kupatikana na kuzaliwa kwa ‘’Jamhuri Ya Muungano Ya Tanzania’’ (The
United Republic of Tanzania) mnamo tarehe 26 Aprili ya mwaka wa 1964. Ikumbukwe na
ifahamike ya kwamba jina “TANZANIA” – limetokana na muunganisho wa maneno au majina ya
awali ya ‘’Tanganyika’’ na ‘’Zanzibar’’ (“Tan”na “Zan”). Maandishi tamati yaliyobakia yaliongezwa
katika kukamilisha ladha nzuri ya jina “Tanzania” ili kuleta maana sahihi, ingawa pia kuna neno
‘Azania’ likuhusishwa katika kuchangia na kukamilisha maana halisia ya chimbuko la jina
‘Tanzania’. Na maana ya neno au jina ‘Azania’ ina maanisha ‘’PWANI YA AFRIKA MASHARIKI’’
(EAST AFRICAN COAST).
Kwa takribani zaidi ya miaka 40 iliyopita mpaka mwishoni kabisa mwa ‘’Vita Vya Kwanza Vya Dunia’’ (World War One) ambavyo kimsingi vita hivi vilifanyika na kupigwana mnamo baina ya miaka ya ‘’1914 mpaka 1918’’, ‘’Nchi Ya Tanganyika’’ (Tanzania Bara) ilikuwa chini ya uongozi na uthibiti wa himaya ya ‘’Kampuni Ya Wajerumani Ya Afrika Mashariki’’ (German East Africa Company) na baadaye tena katika ‘’Dola Ya Watawala Wakoloni Wajerumani’’. Baadaya vita vya kwanza vya dunia (World War One) kumalizika kati ya mwaka ‘’1914 – 1918’’, udhibiti na mamlaka ya ‘’Nchi Ya Tanganyika’’ (Tanzania Bara) ukawa ‘’Chini Ya Utawala Na Uongozi Wa Watawala Wakoloni Waingereza’’, kuanzia mnamo mwaka wa 1919 mpaka mnamo tarehe 9 Desemba ya mwaka wa 1961, pale ambapo ‘’nchi ya Tanganyika’’ ilipojipatia uhuru wake rasmi wa kujitawala na kujiongoza chini ya Hayati Baba wa Taifa, ‘’Mwalimu Julius Kambarage Nyerere’’. Hivyo basi ‘’Mkoloni Muingereza’’ alitawala ‘’Nchi ya Tanganyika’’ (Tanzania Bara) kwa takribani miaka 42. Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba ‘’Watawala WakoloniWaingereza’’ vilevile walivitawala ‘’Visiwa Vya Nchi Ya Zanzibar ‘’ ambavyo kimsingi vilikuwa chini ya utawala wa kimla na usimamizi wa ‘’Sultan Wa Kiarabu , Sultan Jamshid bin Abdullah’’, lakini chini ya ‘’Himaya Ya Waingereza’’ tangu mnamo wa miaka ya 1890.
Baba wa ‘’Taifa Mama Tanzania’’, Hayati Mwalimu ‘’Julius Kambarage Nyerere’’, ambaye pia ni ‘’Muasisi’’ wa kwanza wa ‘’Taifa Letu Sote Tanzania’’ (Tanganyika na Zanzibar), aliitawala Tanzania katika mfumo wa ‘’Chama Kimoja Cha Siasa’’(Single Party Political System) akiwa madarakani tangu mnamo mwaka wa 1961 mpaka alipojiuzulu na kung’atuka kutoka madarakani na katika uongozi wa nchi yeye mwenyewe binafsi mnamo mwaka wa 1985. ‘’Chama Tawala Cha Mapinduzi (CCM)’’ cha Mwalimu ‘’Julius Kambarage Nyerere’’, tokea kuasisiwa na kuanzishwa kwake mnamo wa ‘’Tarehe 5 Mwezi Februari’’ ya mwaka wa 1977, kimekuwepo madarakani katika uongozi wa nchi kwa kipindi kirefu sana na kuweza kushinda katika ‘’Uchaguzi wa mfumo wa vyama vingi vya siasa (Multi – Party Political System) kwa takribani mara 4 tokea kuasisiwa na kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa (Multi – Party Political System) nchini ‘’kwetu Tanzania’’ tangu mnamo mwaka wa 1995’’. Marais wengineo waliowahi kutawala na kuongoza ‘’nchini kwetu Tanzania’’ (Tanganyika pamoja na visiwa vya Zanzibar) baada ya Baba wa Taifa, ‘’Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere’’, ni pamoja na ‘’Mheshimiwa Hayati Ali Hassan Mwinyi’’ (mnamo mwaka wa 1985 mpaka 1995 katika mfumo wa chama kimoja cha siasa), ‘’Mheshimiwa Hayati Benjamin William Mkapa’’, katika mfumo wa vyama vingi vya siasa (mnamo mwaka wa 1995 mpaka 2005), ‘’Mheshimiwa Daktari Jakaya Mrisho Kikwete’’, mnamo mwaka wa 2005 mpaka 2015), ‘’Mheshimiwa Hayati Daktari John Pombe Joseph Magufuli’’, mnamo mwaka wa 2015 mpaka 2021), na hivi sasa ‘’Mheshimiwa Daktari Samia Hassan Suluhu’’, mnamo mwaka wa 2021 mpaka 2025), na pia ni mgombea urais tena kupitia tiketi ya ‘’Chama Chake Cha Mapinduzi /CCM’’ katika ‘’Uchaguzi Mkuu Wa Urais, Wabunge na Madiwani’’ uliofanyika mnamo tarehe 29 Oktoba ya mwaka wa 2025, na kuweza kufanikiwa kuchaguliwa na kushinda tena kiti cha urais wa kuingoza nchi ya Tanzania kwa kipindi kingine kijacho cha miaka mitano.
Mama Tanzania yenye kuwa na ukubwa wa eneo la ardhi takribani kilometa za mraba 947,300, imetenga na kuhifadhi maeneo ya akiba ya misitu asilia pamoja na mapori ya wanyamapori takribani hekta millioni 39 ambayo ni sawa na asilimia 40 ya jumla yote ya ukubwa wa ardhi ya Tanzania. Zaidi ya asilimia 25 ni akiba ya maeneo ya ardhi yanayofahamika kama ‘’Hifadhi Za Taifa’’ (National Parks) au malihai (Protected Areas) sambamba na ‘’Mapori Ya Akiba Ya Wanyamapori (Game Reserves/Wildlife Reserves). Mpaka kufikia mnamo mwaka wa 2014, ‘’nchini kwetu Tanzania’’ kulipatikana jumla ya ‘’Hifadhi Za Taifa 16’’, ‘’Mapori Ya Akiba Ya Wanyamapori 32’’ (Game Reserves/ Wildlife Reserves), ‘’Maeneo Ya Uhifadhi Ya Vitalu Vya Uwindaji 43’’ (Game Controlled Areas), pamoja na ‘’’’Hifadhi Za Baharini (Marine Parks). Mpaka hivi sasa ‘’nchini kwetu Tanzania’’ katika mwaka huu wa 2025 na kuendelea, ‘’Mama Tanzania’’, imetenga na kuhifadhi eneo lake la ardhi kwa ajili ya uhifadhi mbalimbali wa mali hai ‘’Protected Areas’’, eneo la ardhi lenye kufikia takribani asilimia 32 nukta 5, ambapo ‘’Hifadhi Za Taifa’’ (National Parks) ni takribani 21, ‘’Mapori ya Akiba ya Wanyamapori 26’’ (Game Reserves/ Wildlife Reserves), pamoja na ‘’Hifadhi Za Misitu Asilia (Natural Forests), na pia ‘’Eneo La ‘’Hifadhi Mseto’’ (Multiple Land Use Area), la ‘’Mamlaka Ya Hifadhi Ya Ngorongoro’’ (Ngorongoro Conservation Area Authority/NCAA), ‘’Mkoani Arusha’’, ‘’Wilayani Ngorongoro’’, katika ‘’Kanda Ya Kaskazini (Northern Zone) ya ‘’Jamhuri Ya Muungano Ya Tanzania (The United Republic of Tanzania).
Maelezo ya huduma za habari utalii wa ndani.
Kampuni ya Uelimishaji, Uratibu, Uandaaji, Uhamasishaji na Uwezeshaji Utalii wa Ndani na Mazingira,
Follow us:
MAWASILIANO MENGINEYO MAKAO MAKUU (TANAPA)
- Juma tatu - Ijumaa
- 8:00 Asubuhi - 4:30 Jioni
+255 272508216
info@domestictourismsafaris.c info@domestictourismsafaris.co.tz



