TALII NA TEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA ZIWA MANYARA (LAKE MANYARA NATIONAL PARK)
Mkoani Arusha (wilayani Monduli) na mkoani Manyara (wilayani Babati) katika ukanda wa kaskazini (Northern zone) mwa Jamhuri ya muungano wa Tanzania
Chanzo Cha Chimbuko Halisia Kimaelezo Na Ubunifu (Mwalimu Edgardo Kabulwa Welelo)
Jina la Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara (Lake Manyara National Park) limetokana na jina au neno lililotoholewa kutoka katika lugha ya kabila la Wamaasai (Emanyara au Manyara) lenye kumaanisha mmea wa asili wa mti ujulikanao katika lugha aushi ya Kiswahili kama ‘Mnyaa’. Kisayansi na Kibotania mmea huu wa mti unafahamika katika jina lake la kisayansi kama (Eurphorbia tirucalii) na katika lugha ya Kiingerez unafahamika kama (Milk Bush au Finger Eurphorbia) na kawaida huwa na tabia ya kutoa utomvu mweupe pale utakapogongwa na jiwe katika mashina au matawi yake na vilevile hutumika kama gundi lakini pia ni hatari sana pale ambapo 9 - utomvu wake ukipenya katika macho ya binadamu huweza kuatarisha na kusababisha upofu wa macho. Kabila la Maasai hususani katika maeneo ya vijjini hupendelea kuotesha mimea hii ya miti ya ‘MNYAA’ (EMANYARA/MANYARA) kama uziob kuzunguka MABOMA ya mifugo yao sambamba na makazi yao ya kuishi. Lakini pia kwa upande mwingine kuna ubishani miongoni mwa jamii ya kabila la Wamaasai katika maana halisi ya jina au neno ‘Manyara’ kwa sababu viongozi wa jamii ya kimaasai wanadai ya kwamba asili ya neno au jina ‘Manyara’ limetokana na neno la asili ya kimaasai ‘OL MANYARA’ ikimaanisha ‘Makazi’ (Settlement). Mimea mingineyo ambayo ni jamii au koo ya EURPHORBIA ni pamoja na mimea ya miti inayofahamika katika lugha ya Kiswahili kama MTOMVU (Eurphorbia Candelabram) katika lugha ya Kiingereza. Hifadhi hii ya Taifa ya Ziwa Manyara (Lake Manyara National Park)
inapatikana katika mji maarufu wa kitalii wa ‘Mto Wa Mbu’ (Mosquito Creek) Wilayani Monduli Mkoani Arusha na vilevile inapatikana Mkoani Manyara
(Wilayani Babati).Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba hifadhi hii yote kwa ujumla wake ya Taifa ya Ziwa Manyara (Lake Manyara National Park) inapatikana ndani ya Bonde la Ufa la Mkondo wa Mashariki (Eastern Branch/Eastern or Gregory Rift).Bonde Kuu la Ufa (The Great Rift Valley) ni taswira au sura kubwa ya kijiografia barani Afrika na Ulimwenguni kwa ujumla wake ambapo kimsingi ni Mpasuko wa Ardhi katika Ganda la Dunia (a fault in the earth’s crust).Chanzo cha chimbuko lake halisia kimeanzia nchini Uturuki (Turkey) kaskazini katika bara la ASIA na kumalizikia nchini Msumbiji (Mozambique) katika mji wa Beira na inachukua takribani umbali wa kilomita 6500 mpaka 6700 (sawa na takribani maili 4000 mpaka 4200).Bonde hili Kuu la Ufa (The Great Rift Valley) lilipofikia
upande wa Kaskazini mwa nchi ya Kenya kupitia Ziwa Turkana (Lake Turkana) liliweza kugawanyika katika mikondo miwili ya kimtawanyiko ambapo Bonde la Ufa la Mkondo wa Magharibi (Western Rift Valley) lilianzia kupitia Ziwa Albert (Lake Albert), ziwa ambalo linapatikana mpakani baina ya mataifa ya Uganda kwa upande wa Magharibi mwa nchi hiyo na pia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika upande wa mashariki mwa nchi hiyo.Baada ya hapo Bonde hili la Ufa la Mkondo wa Magharibi (Western Rift Valley) liliendelea kutawanyika kuelekea uelekeo wa kusini likipitia mataifa ya nchi za Rwanda, Burundi,DRC,Tanzania na Zambia kupitia mpaka wa Ziwa Tanganyika (Lake Tanganyika) na hatimaye kuungana na Bonde Kuu la Ufa la Mkondo wa Mashariki (Eastern or Gregory Rift Valley) kupitia Ziwa Nyasa (Malawi) ambalo kimsingi Bonde Kuu hili la Ufa la 10 - Mkondo wa Mashariki (Eastern or Gregory Rift Valley) lilianzia kusini mwa ZiwaTurkana nchini Kenya na kuteremkia Kaskazini mwa nchi ya Tanzania likipitia Maziwa Natron, Eyasi na Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara kuelekea katikati ya nchi kuelekea kusini mwa nchi na hatimaye kuungana na Ziwa Nyasa (Lake Nyasa/ Malawi) sambamba na Bonde Kuu la Ufa wa Mkondo wa Magharibi (Westernm Branch).
Ushauri kwa watalii raia wa Tanzania katika kujiandaa na kujipanga kimaandalizi kwa safari utalii
Maandalizi ya usafiri ni vema na busara yakazingatia huduma za malazi au kulala, chakula, usafiri wenyewe na mengineyo mengi yatakayojitokeza ambayo kimsingi ni yaliyo ya muhimu.
Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara (Lake Manyara National Park) ilianzishwa rasmi mnamo mwaka wa 1960, mwaka mmoja kabla ya uhuru wan nchi ya Tanganyika tarehe 9 Desemba ya mwaka wa 1961.Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba Hifadhi hii ya Taifa ya Ziwa Manyara (Lake Manyara National Park) pia ina hadhi ya kimataifa binayotambuliwa ulimwenguni kote na taasisi au shirika la umoja wa mataifa linalojishughulisha na Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO – United Nations Educational, Scientific,and Cultural Organisation) kutokana na umuhimu wake wa kipekee kimazingira kwa faida ya dunia yote kama eneo la bainuai.Umaarufu wa Hifadhi hii ya Taifa ya Ziwa Manyara unathibitishwa kupitia katika kitabu cha hadithi cha raia wa Taifa la Marekani ambaye alikuwa mtaalamu wa uwindaji wa wanyamapori duniani na pia mwandishi wa vitabu aliyejulikana kwa jina la ‘ERNEST HEMINGWAY’ katika kitabu chake kifahamikacho kwa jina la ‘Green Hills of Africa
Mpaka wakati huu kwa hivi sasa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara (Lake Manyara National Park) ina ukubwa wa eneo la ardhi takribani kilometa za mraba 648 Nukta 7. Takribani kilometa za mraba 386 ni nchi kavu, wakati ambapo takribani kilometa za mraba 262 Nukta 7 ni hifadhi ya Ziwa Manyara. Hii ni kutokana na kuongezwa kwa ukubwa wa eneo la Hifadhi ya Ziwa Manyara kupitia Hifadhi ya Msitu wa ‘MARANG’ kama mojawapo ya sehemu ya
Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara. Ni vema ikakumbukwa na kueleweka ya kwamba Hifadhi hii ya Taifa ya Ziwa Manyara pale ilipoanzishwa mnamo mwaka wa 1960 ilikuwa na ukubwa wa kilometa za mraba takribani 330 wakati ambapo (kilometa za mraba 220 zilikuwa ni eneo la Ziwa Manyara na kilometa za mraba 110 zilikuwa ni eneo la nchi
11 - kavu).Hifadhi hii ya Taifa ya Ziwa Manyara kama jinsi ilivyo katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha nayo pia ilianzishwa mnamo mwaka wa 1960 na ni miongoni mwa Hifadhi za Taifa kongwe katika Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Ziwa Manyara ni mojawapo ya
maziwa yaliyotokana na matokeo ya kupitiwa na Bonde Kuu la Ufa la Mkondo wa Mashariki likijulikana kama (Rift Valley Lake) na pia lina urefu wa kilomita 40 na upana wake ni kilomita 13. Kina chake ni kifupi na maji yake ni yenye kuwa na magadi (Alkaline/Saline Water) kama jinsi ilivyo kwa maziwa yote yanayopatikana katika Mkondo wa Bonde la Ufa la upande wa Mashariki (Eastern Rift Valey) katika mataifa ya Afrika ya Mashariki nchini Kenya pamoja na Tanzania. Maziwa yote katika Afrika Mashariki nchini Kenya na Tanzania katika Mkondo wa Bonde la Ufa la upande wa Mashariki (Eastern or Gregory Rift) yana maji yenye kuwa na magadi isipokuwa maziwa mawili nchini Kenya ambayo ni Ziwa
Baringo na Naivasha, na kwa upande wa Tanzania ni kama vile Ziwa Babati (Wilayani Babati katika Mkoa wa Manyara na ziwa Burunge katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire nayo pia wilayani Babati katika Mkoa wa Manyara), hata hivyo Mkoa wa Manyara una maziwa mengi madogo madogo yenye kutokana na Bonde Kuu la Ufa yenye kuwa na maji magadi
(Alkaline/Saline Water) na pia maji baridi (Fresh Water). Ikumbukwe na ieleweke ya
kwamba Mkoa wa Manyara nchini kwetu Tanzania ndio mkoa pekee zaidi katika ukanda wa
kaskazini mwa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ambao ndio uliopitiwa zaidi na taswira au sura ya umbile la kijiografia ya Bonde Kuu la Ufa (The Great Rift Valley), ambayo ni mojawapo ya maumbile ya asili ya sura ya kijigrafia barani Afrika katika upande wa Mashariki mwa AFRIKA. Bonde Kuu la Ufa (The Great Rift Valley) ni mpasuko wa ardhi katika ganda la dunia na linachukua takribani umbali wa takribani kilomita 6500 mpaka kilomita 6700 (ambayo ni sawa na maili kati ya 4000 mpaka 4200) kutokea chanzo chake cha halisi duniani nchini Uturuki (Turkey) barani Asia kaskazini mpaka nchini Msumbiji (Mozambique) kusini katika mji wa Beira.
Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara (Lake Manyara National Park) inafikika kirahisi sanaj kwa njia ya usafiri wa barabara umbali wa takribani kilomita 130 Kusini Magharibi mwa Mji wa Arusha katika barabara kuu ya Arusha – Dodoma. Kutokea Mji wa Arusha ni umbali wa takribani kilomita 80 mpaka njia panda ya ‘MAKUYUNI’. Mara tu ufikapo njia panda ya Makuyuni,kama unatokeo Arusha Mjini, elekea upande wako wa mkono wa kulia na kama unatokea uelekeo wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa na mikoa mingineyo nchini Tanzania, elekea upande wako wa mkono wa kushoto. Utaweza kuona Mabango elekezi byapo yanayotangaza uelekeo na utalii wa Hifadhi hizi za kanda ya kaskazini (Northern Safari 12 - Circuit). Kutokea njia panda ya ‘MAKUYUNI’ inachukua takribani umbali wa kilomita 50 kuweza kufika katika mji maarufu wa kitalii Afrika Mashariki wa ‘MTO WA MBU’ (Mosquiton Creek) ambao upo karibu kabisa na lango la kuingilia katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara. Vilevile Hifadhi hii ya Ziwa Manyara inafikika umbali wa kilomita 95 kama unatokea Hifadhi ya Taifa ya Tarangire. Ni mwendo wa umbali wa saa 2 mpaka 2.30 kutokea Arusha Mjini na saa 1 mpaka 1.30 kama unatokea Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Ni pamoja na Ukuta wa Bonde la Ufa (Rift Wall of The Great Rift Valley) katika upande wa Magharibi mwa hifadhi yenyewe, Ziwa Manyara (Lake Manyara) katika upande wa Mashariki mwa hifadhi yenyewe, Msitu wa Kaskazini wa Uhifadhi Maji Ardhini (Norhern Groundwater and Riverine Forest/Groundwater and Riverine Forest) ambao kimsingi chanzo chake cha maji ya chemichemi kinatokea katika Msitu wa Asili wa Nyanda za Juu Kaskazini (Northern Highland Forest Reserve (NHFR) upatikanao katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA) na Maji haya ya chemichemi husafiri chini ya ardhi takribani mita 600 na hatimaye kupenyeza katika nyufa za miamba ya volcano (Volcanic Rocks) chini ya Ukuta wa Bonde la Ufa katika Hifadhi hii ya Taifa ya Ziwa Manyara na kuufanya msitu huu kuwa ni wa kijani kibichi na pia kuwa na vyanzo vya uhakika vya maji karibia mwaka mzima na pia kulisha Ziwa Manyara na chemichemi za maji moto. Msitu huu wa Asili wa Uhifadhi wa Maji Ardhini unapatikana kijiografia upande wa kaskazini mwa lango la kuingilia Hifadhi hii ya Taifa ya Ziwa Manyara na kumalizikia kikomo chake katika Mto Msasa na kuchukua ukubwa wa eneo wa takribani hekta 1300. Hivyo basi ni vema na ikakumbukwa na kueleweka ya kwamba mara punde uingiapo lango la kuingilia Hifadhi hii ya Taifa ya Ziwa Manyara una anza kukutana na Msitu huu wa Uhifadhi wa Maji Ardhini (Groundwater Forest).
Ina anzia katika Ziwa Manyara takribani mita 960 mpaka 1478. Wastani wa mnvua katika mwaka Hifadhini Ziwa Manyara ni takribani milimita za mnvua 760. Mnvua za Masika huanzia Mwezi wa Machi na kuendelea mpaka mwishoni mwa Mwezi Mei. Mnvua kubwa zaidi hutokea kunyesha baina ya kipindi cha Mwezi Aprili au Mwezi Mei na hii wakati mwingine hupelekea baadhi ya barabara za utalii ndani ya Hifadhi kufungwa na kusitishwa kwa matumizi. Nyuzi joto kwa wastani Hifadhini Ziwa Manyara ni takribani Nyuzi Joto 22.
Ni kama vile Ukuta wa Bonde la Ufa (Rift Valley Ridge/Escarpment) katika upande wa Magharibi mwa hifadhi, Ziwa Manyara (Lake Manyara) katika upande wa Mashariki mwa 13 - hifadhi, Simba Wapandao Juu ya Miti (Tree Climbing Lions), Viumbe hai ndege, Chemichemi za maji moto katika upande wa kusini mwishoni kabisa mwa Hifadhi (Hot Water Sulphur Springs), na bila kusahau Msitu wa Uhifadhi Maji Ardhini (Northern Groundwater and
Riverine Forest/ Groundwater and Riverine Forest).Kibayolojia, Msitu wa Uhifadhi Maji Ardhini (Groundwater and Riverine Forest) ni mojawapo ya maeneo muhimu sana katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.Takribani asilimia 50 ya uoto wa asili wa mimea ipambayo maua, takribani asilimia 70 ya viumbe hai ndege, na takribani asilimia 60 ya Mammalia wakubwa wanapatikana katika msitu huu, na cha ziada ni ya kwamba msitu huu unachangia kwa kiwango kikubwa sana kama mvuto wa kipekee na wenye kupendeza ndani na nje ya hifadhi yenyewe kuwa yenye thamani ya hali juu sana.
Ni pamoja na Viboko (Hippopotamuses), Tembo/Ndovu (Bush/Savanna/African Elephant), Nyati/Mbogo (Savanna/African Buffaloes), Simba (Lions), Twiga (Maasai/KilimanjaroGiraffes), Kuro (Common Waterbucks), Pundamilia(Common/Plain Zebra), Swala Pala (Impala), Pongo (Bushbuck), Kima (Blue Monkeys/Syke Monkeys), Nyani (Olive Baboon/Savanna Baboon), Tumbili/Ngedere (Black – Faced Monkeys), Ngiri (Common Warthog),Nyumbu wa Kijivu (Eastern White – Bearded Wildebeest) mojawapo wa aina ya
nyumbu (races/subspecies) tofauti kabisa na aina ya nyumbu wapatikanao Tarangire, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ndani ya Bonde la Ngorongoro (Ngorongoro Crater) na pia nje ya Bonde la Ngorongoro pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Wanyamapori wengineo Hifadhini Manyara ni pamoja na Digidigi /Saruya (Kirk’s DikDik), Fisi Madoadoa (Spotted Hyena) Pimbi Miamba (Rock Hyraxes), Mbuzi Mawe (Klipspringers) na wengineo wengi wa kutosheleza. Wanyamapori ambao hawapatikani kabisa katika Hifadhi hii ya Taifa ya Ziwa Manyara ni kama vile Mbega wenye kuwa na rangi nyeusi na nyeupe (Black and Whiteb Colobus Monkeys), Pofu (Eland), Tandala Wakubwa na Wadogo (Greater and Lesser Kudu), Korongo (Roan), Palahala (Sable), Isha (Steenbok), Nyamera (Topi), Mbwa Mwitu (Wild dog) na Faru (Rhinos). Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara (Lake Manyara National Park) ina zaidi ya takribani spishi 380 za viumbe hai ndege kuweza kurekodiwa na kuripotiwa kisayansi na kitafiti. Katika orodha hii ya spishi za viumbe hai ndege Hifadhini Ziwa Manyara ni pamoja na Korongo Pwani/Dandala (Little Egret), YangeYange Mkubwa (Yellow – billed Egret), Korongo Msuka (Great – White Egret), Ponda Gundi Mkubwa (Goliath Heron), Korongo Kisiwa (Grey Heron), Mnandi Mkia Mrefu (Long – Tailed Cormorant), Marabu (Marabou Stork), Mwari Mweupe (Great - White Pelican) na wengineo walio wengi.
Ni pamoja na Msitu wa Uhifadhi Maji Ardhini (Groundwater and Riverine Forest) ambapo hupatikana aina mbalimbali ya mimea ya miti kama vile Mkomba (Tabernaemontana usambarensis), Mlegea (Sausage Tree), Mkwaju (Tamarind), Mtagaico (Cape Mahogany),
Marumbay (Croton megalocarpus), aina kadhaa za miti ya Mikuyu (Fig Trees), Migunga (Acacias/Achelia) ya aina mbalimbali na miti mingineyo iliyo yaina nyingi. Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba Msitu wa Uhifadhi Maji Ardhini (Northern Groundwater and Riverine Forest/ Groundwater and Riverine Forest) hujipatia na kulishwa na chemichemi za maji ya kudumu zinazotiririka chini kwa chini kutokea kwenye miamba ya volcano (Volcanic Rocks) chini ya Ukuta wa Bonde Kuu la Ufa (Rift Wall of The Great Rift Valley). Karibu jirani kabisa na eneo la Msitu wa Uhifadhi Maji Ardhini (Groundwater and Riverine Forest) panapatikana eneo jingine la uoto wa asili wa mapori ya miti ya Migunga (Acacia/Achelia Woodland) yenye kuwa na jumla ya eneo takribani hekta 1820 na kutawanyika kutokea Msasa mpaka Mto Bagayo. Jamii ya uoto wa asili uliotawala eneo hili ni pamoja na mimea miti aina ya Migunga Mwanvuli (Umbrella Thorns). Vilevile katika eneo hili hupatikana pia aina ya uoto wa
asili unaovumilia mazingira ya makazi ya ardhi kame (Drought tolerant species) kama vile Mjunju (Desert Date). Eneo hili la mazingira ya makazi hutawaliwa na kupendelewa na wanyamapori walao mimea nyasi pamoja na majani ya juu katika matawi ya miti (Grazers and Browsers) kama vile Swala Pala (Impala), Nyati au Mbogo (Buffalo) pamoja na Twiga (Giraffes). Kutokea eneo la Mto Endabash (Endabash River) kuelekea uelekeo wa mwishoni kabisa kusini mwa Hifadhi hii ya Taifa ya Ziwa Manyara hupatikana zaidi eneo la uoto wa asili wa mimea mchanganyiko ya miti ya mapori ya Migunga (Acacia/Achelia Woodland). Eneo hili la uoto wa asili wa mimea miti mchanganyiko ya Migunga (Acacia Woodland) linachukua ukubwa wa eneo takribani hekta 2290. Aina ya uoto wa asili wa mimea miti inayopatikana katika eneo hili ni kama vile Migunga Mwanvuli (Umbrella Thorns), Mjunju (Desert Date), Mlegea (Sausage Tree) na mimea mingineyo midogo midogo iliyo mingi kama vile Ndulele (Sodom Apple). Mazingira haya ya makazi huweza kuonekana kwa wanyamapori kama vile Tembo (Elephant), Swala Pala (Impala), Twiga (Giraffe) pamoja na Pundamilia (Zebras). Baada ya hapo eneo jingine la uoto wa asili linalofuatia ni eneo la uoto wa asili wa kandokando ya mwambao wa Ziwa Manyara sambamba na maeneo wazi katika msitu (Alkaline Grassland and Glades) ikichanganyikana na eneo la Uoto wa Msitu wa Uhifadhi Maji Ardhin (Groundwater and Riverine Forest). Kwa ujumla wake eneo hili limetawaliwa na uoto wa asili
wa mimea nyasi ya aina mbalimbali. Wanyamapori wapatikanao na kuonekana katika maeneo haya ya mazingira ya makazi ni kama vile Nyati au Mbogo, Nyumbu wa Kijivu, pamoja na 15 - Pundamilia. Katika upande wa Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara ni Ukuta wa
Bonde la Ufa (Escarpment/Rift Wall of The Great Rift Valley) ambapo kimsingi hupatikana aina ya uoto wa asili katika miamba kama vile Mturituri (Commiphora), Mibuyu (Baobabs) karibia imetapakaa na kutawanyika eneo lote la Ukuta wa Bonde, Migunga ya aina mbalimbali na kadhalika.
Ni wakati wa kipindi wa msimu wa kiangazi kuanzia mwezi Julai, Oktoba, Novemba mpaka
Juni.
Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara (Lake Manyara National Park) inapatikana karibu kabisa na mji wa ‘Mto wa Mbu’ (Mosquito Creek) wilayani Monduli katika Mkoa wa Arusha maarufu kwa shughuli za kiutalii ambapo huduma kama vile za vyakula, malazi na burudani zinapatikana kwa urahisi na kwa bei nzuri. Lakini hata hivyo watanzania wazalendo watalii wa ndani wanaweza kujibebea vyakula vyao wenyewe vya kujipikia.
Nyumba za kulala wageni na maeneo ya kupiga kambi za watu binafsi zinapatikana katika Mji wa ‘Mto wa Mbu’ (Mosquito Creek), uliopo jirani na karibu kabisa na hifadhi yenyewe. Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba kwa watanzania wazalendo watalii wa ndani hakuna ulazima sana wa kubeba mahema ya kupiga kambi.
Maandalizi ya usafiri, huduma za chakula, malazi au kulala na mengineyo ni ya muhimu kutekelezwa ili kupata hali halisi ya safari utalii yenu ya matembezi hifadhini, lakini vilevile pasipo kusahau gharama za usafiri wenyewe uwe wa kukodi au wa kwenu wenyew binafsi. Hii ndiyo dira kamili itakayowapatia picha kamili ya mambo kama safari utalii inaendeka au haiendeki? Je ni kitu gani kirekebishwe na kipi chenye kuwa na mapungufu kiweze kuondolewa ili safari utalii yenu ya matembezi hifadhini iendeke kulingana na fungu la fedha zilizopo.
Mambo muhimu ya kufahamu na kujiuliza
Maandalizi ya sanduku la huduma ya kwanza ni muhimu sana na vile vile kwa wananchi wenyewe katika matembezi hifadhini wanashauriwa kuwa na vijisanduku vyao binafsi vya huduma ya kwanza kwa ajili ya dharura zinazoweza kujitokeza katika matembezi hifadhini. Elimu itolewe kwa wananchi watalii wa ndani inayohusiana na huduma ya kwanza. Maandalizi ya sanduku la huduma ya kwanza ni muhimu sana na vile vile kwa wananchi wenyewe katika matembezi hifadhini wanashauriwa kuwa na vijisanduku vyao binafsi vya huduma ya kwanza kwa ajili ya dharura zinazoweza kujitokeza katika matembezi hifadhini. Elimu itolewe kwa wananchi watalii wa ndani inayohusiana na huduma ya kwanza.
Vifaa muhimu vya kuchukua katika safari utalii hifadhini
Vifaa vyote vilivyo vya muhimu katika safari utalii yenu ya matembezi hifadhini kama vile
Kamera, Video Kamera, Vitabu vya viongozi (Guide books) vya mimea, wanyamapori na ndege, Kalamu na madaftari madogo madogo ya kujiandikia na kujiwekea kumbukumbu zenu wenyewe.
Huduma za mahitaji mengineyo
Ni pamoja na mambo ya ziada ya mahitaji yanayojitokeza na upatikanaji wake katika
sehemu husika watalii wa ndani walipo.
Maelezo ya huduma za habari utalii wa ndani.
Kampuni ya Uelimishaji, Uratibu, Uandaaji, Uhamasishaji na Uwezeshaji Utalii wa Ndani na Mazingira,
Follow us:
MAWASILIANO MENGINEYO MAKAO MAKUU (TANAPA)
- Juma tatu - Ijumaa
- 8:00 Asubuhi - 4:30 Jioni
+255 272508216
info@domestictourismsafaris.c info@domestictourismsafaris.co.tz



