TALII NA TEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA MILIMA YA UDZUNGWA
Mkoani Morogoro na Iringa(asilimia 20% morogoro na asilimia 80% Iringa) katika jamhuri ya muungano wa Tanzania
Chanzo cha Chimbuko Halisia Kimaelezo Na Ubunifu (Mwalimu Edgardo Kabulwa Welelo)
Ukweli Wa Mambo Kuhusiana Na Hifadhi Ya Taifa Ya Milima Ya Udzungwa; Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa ipatikanayo kijiografia mkoani Morogoro (asilimia 20) katika wilaya ya Kilombero na mkoani Iringa (asilimia 80) katika wilaya ya Kilolo, ilianzishwa rasmi mnamo mwaka wa 1992. Ilifunguliwa na kuzinduliwa na Rais wa Shirika linalojihusisha na Mfuko wa Fedha wa Uhifadhi wa Wanyamapori Duniani 60 - (WORLDWIDE WILDLIFE FUND) katika kipindi hicho aliyefahamika kwa majina ya Prince Bernhard wa Uholanzi. Chimbuko halisia ya asili ya jina ‘UDZUNGWA’ ni kutoka katika neno la kabila la Wahehe ‘WADSUNGWA’ ikimaanisha ya kwamba watu wanaoishi ng’ambo ya pili ya milima au chini ya milima. Takribani sehemu kubwa ya Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa kijiografia katika upande wake wa Mashariki ni Msitu wa asili wa mvua wa kitropiki wenye kujumuisha jamii za mimea mbalimbali zipatikanazo zaidi ya 2500 zinazofanya makazi ya bayoanuai mbalimbali. Milima na vilele kwa ujumla wake vipatikanavyo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa ni muendelezo wa mnyororo au safu ya milima maarufu duniani ya TAO LA MASHARIKI (THE EASTERN ARC MOUNTAINS) inayoanzia kijiografia na kisayansi kwa mujibu wa wataalamu wa elimu ya miamba aidha kusini mwa nchi ya Malawi na kuishia kusini mwa nchi ya KENYA kupitia miinuko ya vilima vya TAITA. Au kwa upande mwingine na kwa mujibu wa wataalamu wengineo wa elimu ya miamba wakisema na kuelezea ya kwamba imeanzia kusini mwa nchi ya KENYA kwenye miinuko ya vilima vya TAITA na kupitia nchini kwetu TANZANIA katika milima ya PARE (kaskazini na kusini), USAMBARA (magharibi na mashariki), NGUU (TANGA), NGURU (MOROGORO), UKAGURU (MOROGORO), ULUGURU (MOROGORO), RUBEHO (MOROGORO), MALUNDWE (MOROGORO), MAHENGE (MOROGORO), LIVINGSTONE (NYANDA ZA JUU KUSINI – TANZANIA’S SOUTHERN HIGHLANDS), HIFADHI YA TAIFA YA MILIMA YA UDZUNGWA YENYEWE ( MOROGORO NA IRINGA), na kuishia MISITU YA MAKAMBAKO (MAKAMBAKO GAP) kusini mwa Tanzania. Milima hii ya TAO LA MASHARIKI (THE EASTERN ARC MOUNTAINS) inamalizikia kuishia katika nchi ya Malawi ambayo ni jirani yetu Tanzania katika upande wa kusini mwa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba sehemu kubwa ya MILIMA YA TAO LA MASHARIKI (THE EASTERN ARC) inapatikana Kijiografia nchini kwetu TANZANIA na inachukua ukubwa wa eneo lenye kukaribia takribani kilometa za mraba 10, 000. Umaarufu na upekee wa Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa kama sifa yake kubwa tofauti kabisa ukilinganisha na Hifadhi nyinginezo za Taifa nchini Tanzania ni pamoja na kuwa na baadhi ya wanyamapori, mimea, na viumbe hai adimu ambavyo kwa ujumla wake havipatikani sehemu yeyote ile si tu nchini Tanzania bali pia hata duniani na badala yake vinapatikana pekee tu katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa kama ‘KITOVU CHA UHIFADHI WA VIUMBE HAI ADIMU’. Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa inaundwa na kujengwa katika maeneo takribani matano ya akiba ya Misitu ya asili ambayo kimsingi ilishaanzishwa tangu mnamo miaka ya 1950, ambayo ni Mwanihana, Kilombero Magharibi, Nangaje, Matundu na Iwonde. Wanasayansi wanaamini ya kwamba Misitu hii ya asili ya kitropiki katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa ina umri wa miaka takribani zaidi ya millioni 30 iliyopita na ilishawahi kuungana hapo zamani pamoja na Misitu ya KONGO NA AFRIKA MAGHARIBI. Na ndio Hifadhi pekee nchini Tanzania ambayo 61 - inapatikana katika Milima ya Tao la Mashariki (The Eastern Arc Mountains) na vilevile ndio Hifadhi ambayo ina wanyamapori wengi tofautitofauti wa jamii ya nyani (primates) zaidi ya kumi (10). Vile vile ni Hifadhi pekee nchini Tanzania ambapo umeme unaozalishwa kwa njia ya maji takribani asilimia 70 chanzo chake hutokea katika Hifadhi hii.
Ushauri kwa watalii raia wa Tanzania katika kujiandaa na kujipanga kimaandalizi na kikamilifu kwa safari utalii
Tafuteni na kusanyeni taarifa zote muhimu zinazohusiana na wadau wa sekta ya utalii pamoja na mamlaka husika za taasisi za kiserikali zenye kuwa na dhamana za usimamizi wa uhifadhi wa mali hai kama vile TANAPA, TAWA, NCAA, TFS na kadhalika kupitia vyanzo vyao kama vile mtandao wa intaneti kupitia tovuti husika na vilevile watoao huduma za utalii (Tour Operators) katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa. Taarifa hizo zipatikanazo ndizo zitakazowezesha kuandaa mpango mkakati wa kutembelea na kutalii hifadhini. Haya ndio mambo muhimu ambayo yatakayotoa hali halisi ya fedha zitakazohitajika na jinsi zitakavyotumika.
Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa ipatikanayo kwa pamoja mkoani Iringa na Morogoro ilianzishwa rasmi mnamo mwaka wa 1992.
Hifadhi hii ya Taifa ya Milima ya Udzungwa ina ukubwa wa eneo lenye kuwa na kilometa za mraba 1990
Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa inafikika umbali wa kilometa takribani 380 kwa njia ya usafiri wa barabara kutokea mji mkubwa wa kibiashara na kihistoria wa Dar es Salaam (takribani saa 6) katika upande wa kusini magharibi kijiografia na vilevile umbali wa kilometa 75 kutokea mji wa Mikumi na Hifadhi ya Taifa Mikumi mkoani Morogoro. Kijiografia, Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa inapatikana kwa pamoja katika mikoa ya Morogoro (asilimia 20) katika wilaya ya Kilombero, na mkoani Iringa (asilimia 80) katika wilaya ya Kilolo. Makao makuu ya Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa yanapatikana katika mji mdogo wa Mang’ula takribani kilometa zipatazo 60 kutokea mji mdogo wa Mikumi kupitia njia ya usafiri wa barabara wa Mikumi – Ifakara. Makampuni kadhaa ya usafiri wa mabasi yanatoa huduma za usafiri kupitia hifadhini kutokea Dar es Salaam na Ifakara. Wasiliana na wakala wa usafiri kwa maelezo zaidi. Vilevile kuna lango la kuingilia upande wa 62 - magharibi. Lango la Msosa ni kilometa 10 kutokea Mtandika. Na lango la Udekwa ni kilometa 63 kutokea Ilula katika barabara kuu ya Dar – es – Salaam - Iringa.
Ni pamoja na Milima ya Udzungwa yenyewe sambamba na vilele vyake kama vile kilele cha Mwanihana unaosimama kutoka usawa wa bahari mita takribani 2500, ambacho ni kilele cha pili kwa urefu, Luhomero mita takribani 2,576 ambacho ndicho kirefu zaidi na pia nambari moja. Maumbile utalii asilia ya kijiografia mengineyo yanayopatikana ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa ni pamoja na kuta za bonde, Misitu ya asili na Mto Ruaha Mkuu. Aina mbalimbali za sura ya eneo kijiografia kama vile vilima, milima, mabonde, maporomoko ya maji, mandhari ya eneo nzuri yenye kupendeza.
Inaanzia mita 200 mpaka mita 2579. Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa inapata mvua nyingi za kutosha kwa mwaka kuanzia mwezi Novemba mpaka mwezi Mei na vilevile mvua za vuli zinazoanzia mwezi wa Oktoba mpaka Desemba. Mvua za masika kwa mwaka katika upande wa mashariki mwa Hifadhi ni zaidi ya milimita 2,000 wakati wa msimu wa mvua nyingi, wakati ambapo katika upande wa kaskazini magharibi ni takribani milimita 600 kwa mwaka. Msimu wa kiangazi kawaida huanzia mwezi wa Septemba mpaka mwezi wa Oktoba. Kiasi cha joto la juu ni nyuzi joto takribani 31 katika mwezi wa Oktoba, ambapo kiasi cha joto la wastani ni nyuzi joto 21 katika mwezi wa Julai.
Maeneo ya kiutamaduni na kihistoria ya Mlima wa mungu (Bokelo), Nyumbanitu na milima ya Ndundulu pamoja na mapango ya Mwanaluvele yanayotoa ufahamu wa maisha ya makabila katika maeneo ya kusini mwa Tanzania namna jinsi ya maisha waliyoishi kabla ya kupisha uhifadhi. Þ Chemichemi za asili katika uwanda wa juu wa msitu wa maji zinazofanya vyanzo vya mito ya kudumu ya Lofia, Msosa, Mwaya, Mkula, Rumemo, Sonjo, Ruipa na mengineyo mingi ambayo kimsingi hutiririsha maji yake kuelekea katika bonde maarufu la Kilombero. Þ Vilele virefu zaidi vya LUHOMERO katika mita 2579 na MWANIHANA katika mita 2500 kutoka usawa wa bahari. Þ Aina 250 za vipepeo zikijumisha jamii tatu za vipepeo ambao hawapatikani popote pale nchini Tanzania pamoja na Duniani na badala yake wanapatikana pekee hapa katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa. Ni pamoja na Charaxes lucynae mwanihanae, Papilio hornimanii mwanihanae na Balionchilla mwanihanae. 63 - Þ Jamii mbalimbali za mijusi pamoja na amfibia zikijumuisha jamii mbili za mijusi ya Udzungwa (Cnemospis udzungwae na Phrynobatrachus udzungwesis) na vinyonga ambao hawapatikani sehemu yeyote ile Duniani. Þ Jamii takribani 11 za wanyamapori jamii ya nyani (primates) ambapo jamii mbili kati ya hizo 11 ambazo ni Ngolaga (Sanje Crested Mangabey) na Mbega mwenye kuwa na rangi nyekundu kichwani (Iringa Red Colobus Monkey) ambao kimsingi hawapatikani sehemu yeyote ile Duniani na badala yake wanapatikana pekee katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa. Þ Maporomoko mengi ya maji yakiongozwa na maporomoko maarufu ya SANJE yenye kuwa na urefu unaofikia mita zipatazo takribani 170. Maporomoko mengineyo ni pamoja na Prince Bernhard, Njokamoni, Mwaya, Sonjo na Msolwa. Þ Muonekano mzuri wa Msitu wenye kuwa na mandhari yenye kuvutia ambapo jamii za mimea miti takribani 2,500 ambazo zinafanya kuwa maskani ya makazi ya viumbe hai adimu na wengineo tofautitofauti. Þ Aina takribani 400 za viumbe hai ndege zikijumuisha ndege wahamaji na ndege wakazi (residents). Pia wanapatikana ndege asilia wanapatikana pekee katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa ambapo hawawezipatikana sehemu yeyote ile nchini Tanzania na Duniani kama vile Kwale Udzungwa (Udzungwa Forest Patridge) pamoja na ndege chozi (Rufous winged sunbird). Þ Njia za asili Msituni katika utalii wa matembezi ya miguu (walking safaris).
Utalii wa matembezi katika uonaji wa maporomoko ya maji na misitu ambao kimsingi hutoa fursa ya kuweza kuona jamii mbalimbali za wanyamapori jamii ya nyani (primates), ndege, mijusi, amfibia na kadhalika. Utalii wa aina hii hufanyika wakati wote katika mwaka hususani nyakati za kiangazi. ° Utalii wa upandaji milima. Utalii wa aina hii hutoa fursa ya ufikiaji vilele virefu vya Luhomero pamoja na Mwanihana na kuweza kujionea mwenyewe mandhari nzuri yenye kupendeza ya maeneo ya chini ya mlima na vilevile pia mfumo wa kilimo cha umwagiliaji cha mazao ya miwa na mpunga katika bonde maarufu la Kilombero. ° Utalii wa uonaji au utazamaji viumbe hai ndege ambao kimsingi hufanyika katika njia za asili ndani ya Misitu maalumu kwa wageni watalii wapendeleao kutazama na kutambua aina tofautitofauti za ndege. Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba kunapatikana ndani ya Hifadhi takribani zaidi ya spishi 400 za ndege wahamao (migratory birds) sambamba na ndege wakazi (resident birds) ambao hawahami na wanaopatikana nyakati zote katika mwaka. ° Utalii wa upigaji picha pamoja na filamu ambao kimsingi na kiutaratibu hufanyika mwaka mzima hususani wakati wa mvua fupi za vuli katika mwezi wa Desemba hadi mwezi Februari ambapo maua pori mengi hifadhini huonekana na 64 - kuchanua na kupamba misitu na vilevile pia kuna uwezekano mkubwa wa kujionea ndege wengi wanaohama. ° Utalii wa upigaji kambi ndani ya hifadhi kama vile kambi maalumu (special campsites) au kambi za jumuiya (public campsites). ° Utalii wa kiutamaduni na kihistoria ambao hutoa fursa ya kutembelea na kutalii maeneo ya kiutamaduni na kihistoria ya Mlima wa mungu (Bokelo), Nyumbanitu pamoja na milima ya Ndundulu na mapango ya Mwanaluvere yanayotoa ufahamu wa maisha ya baadhi ya makabila ya maeneo ya kusini mwa Tanzania yaliyoishi kabla ya kupisha uhifadhi. Nje ya Hifadhi utalii wa kiutamaduni unajumuisha kutalii kwa kutumia baiskeli katika kilimo cha umwagiliaji kwenye mashamba ya miwa, mpunga na mpira/rubber plantations ambayo ni mashamba ya wazawa asilia wa maeneo hayo. Pia shughuli nyinginezo ni pamoja na kuweza kujionea na kujinunulia vinyago, ngoma za asili, vyakula vya asili, maeneo ya matambiko na kadhalika.
Jamii 11 za wanyamapori jamii ya nyani (primates) zikijumuisha aina 2 za nyani ambao kimsingi hawapatikani sehemu yeyote ile nchini Tanzania na Duniani kote isipokuwa pekee tu katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa kama vile Ngolaga (Sanje Crested Mangabey) pamoja na Mbega mwenye kuwa na rangi nyekundu kichwani wa Iringa (Iringa Red Colobus Monkey). Wanyamapori wengineo jamii ya nyani ambao ni sehemu kati ya spishi 11 ni pamoja na aina 3 za Galago au Komba kama vile Matundu dwarf galago, Galago mwenye kuwa na masikio madogo (Small eared galago) pamoja na Galago wa mlimani (Mountain dwarf galago). Wanyamapori wengineo tofauti na wale jamii ya nyani ni kama vile Tembo (Ndovu), Nyati (Mbogo), Simba, Chui, Pongo, Tandala, Fungo, Fisi, Ngiri, Viboko, Nguchiro, Vicheche, Mbawala, Funo, Nguruwepori, Muhanga, Pimbi, Sengi, Nungunungu, Panyabuku na kadhalika. Viumbe hai wanaotambaa kama vile Mamba hutumia muunganiko wa mazingira yaliyofunikwa na msitu mkubwa wenye mimea kuanzia jamii ndogo kabisa za kawaida na kushangaza kama vile Saintpaulia (African Violet) mpaka jamii za miti mirefu zaidi ya mita 30 kutoka uso wa ardhi kama vile Sterculia appendiculata) pamoja na Parinari excesa. Wataalamu wa viumbe hai wanaotambaa (Herpetologists) wana fursa nzuri ya kipekee kuweza kufanya tafiti zao za kisayansi kwa mfano kama vile mijusi wa aina mbalimbali hifadhini zikijumuisha jamii mbili za mijusi zinazopatikana pekee hapa Udzungwa kama vile (Cnemaspis udzungwae) na (Phrynobatranchus udzungwesis). Mijusi hii hupata chakula chake kutoka katika jamii zipatazo takribani 250 za vipepeo zikijumuisha jamii 3 ambazo hazipatikani sehemu yeyote nchini Tanzania na Duniani na badala yake zinapatikana pekee katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa kama vile (Charaxes lucyae mwanihanae), (Papilio hornimanii mwanihanae), pamoja na (Baliochilla mwanihanae). Takribani zaidi ya spishi 400 za ndege wameripotiwa na kurekodiwa 65 - kupatikana ndani ya Hifadhi. Aina hizi za ndege karibia 400 mbalimbali zinajumuisha pia jamii 2 za ndege ambazo hazipatikani sehemu yeyote ile nchini Tanzania na Duniani kote isipokuwa pekee tu katika Hifadhi hii kama vile Kwale Udzungwa (Udzungwa Forest Patridge) pamoja na ndege chozi (Rufous Winged Sunbird). Kutokana na sifa hii imeweza kuifanya Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa kuingia katika ramani Duniani ya maeneo tengefu yenye kuwa na jamii nyingi za ndege (Important Bird Areas – IBA). Vilevile imepewa heshima ya kipekee ya kuwa katika muendelezo wa moja ya maeneo 34 yanayotambulika kidunia kwa kuwa na bayonuai nyingi zaidi.
Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa inaangukia katika uoto wa asili wa misitu ya milimani na ndio hifadhi ya pekee inayopatikana katika ukanda wa milima ya Tao la Mashariki (Eastern Arch Mountains).
Mwezi wa Desemba mpaka Mwezi Julai kwa ajili ya kujionea na kushuhudia ‘’Msafara wa Uhamaji wa Wanyamapori’’ kama vile Nyumbu na Wanyamapori wengineo walio wengi. Vilevile Mwezi wa Juni mpaka Mwezi Oktaba kwa ajili ya kujionea ‘’Wanyamapori Wawindaji na Walao Nyama (Predators)’’ kama vile Simba (Lions), Chui (Leopards), Fisi Madoadoa (Spotted Hyenas), Duma (Cheetah) na wengineo walio wengi.
Mpaka wakati huu ukweli halisi wa mambo ni kwamba Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa ina huduma moja ya Hoteli ya Twiga ambayo ina uwezo wa kulaza wageni takribani 30 kwa usiku mmoja. Huduma za kupiga mahema zinapatikana katika maeneo yaliyo ya nje kuzunguka Hoteli katika bei nafuu. Katika matembezi ya kutalii katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa ni lazima na wajibu kwa wageni watalii wa kitanzania kuhakikisha ya kwamba wanabeba mahema ya kwao wenyewe kama ni safari utalii ya zaidi ya siku moja katika kupanda milima. Wageni watalii wa kitanzania wanaweza kupata huduma za malazi katika maeneo ya kupiga kambi maalumu (special campsites) au kambi za jumuiya (public campsites) ndani ya hifadhi katika viwango maalumu. Kwa maelezo zaidi chanzo cha tovuti ya shirika la hifadhi za taifa kinatoa taarifa zote (www.tanzaniaparks.go.tz). Hatahivyo, huduma za malazi nje ya Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa zinapatikana pia katika mji mdogo wa Mang’ula kupitia wamiliki binafsi za nyumba za kulala wageni kama vile Hondohondo, Wildthings Tented Camp na kadhalika.
Mpaka wakati huu ukweli halisi wa mambo ni kwamba Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa ina huduma moja ya Hoteli ya Twiga ambayo ina uwezo wa kulaza wageni takribani 30 kwa usiku mmoja. Huduma za kupiga mahema zinapatikana katika maeneo yaliyo ya nje kuzunguka Hoteli katika bei nafuu. Katika matembezi ya kutalii katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa ni lazima na wajibu kwa wageni watalii wa kitanzania kuhakikisha ya kwamba wanabeba mahema ya kwao wenyewe kama ni safari utalii ya zaidi ya siku moja katika kupanda milima. Wageni watalii wa kitanzania wanaweza kupata huduma za malazi katika maeneo ya kupiga kambi maalumu (special campsites) au kambi za jumuiya (public campsites) ndani ya hifadhi katika viwango maalumu. Kwa maelezo zaidi chanzo cha tovuti ya shirika la hifadhi za taifa kinatoa taarifa zote (www.tanzaniaparks.go.tz). Hatahivyo, huduma za malazi nje ya Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa zinapatikana pia katika mji mdogo wa Mang’ula kupitia wamiliki binafsi za nyumba za kulala wageni kama vile Hondohondo, Wildthings Tented Camp na kadhalika.
Hii ndio dira ya safari utalii ya matembezi hifadhini ambayo itakayotoa picha na majibu halisi na sahihi ya safari utalii yenu ya matembezi hifadhini kwa ujumla wake. Je nini kifanyike? Je suluhisho lake ni nini? Haya yote yatafahamika baada ya
ukamilifu wa maandalizi ya usafiri, huduma za chakula, malazi au kulala kuzingatiwa kwa umakini mkubwa. Tozo Hifadhini ni kama vile;
1. Tozo za kuingia Hifadhini kwa saa 24.
2.Tozo za kupiga kambi za jumuiya (public campsites)
3.Tozo za kupiga kambi maalumu (special campsites)
4. Tozo ya Malazi Hoteli ya Twiga
5. Tozo za utalii wa filamu
6. Tozo ya muongozaji wageni watalii/ askari wa wanyamapori katika matembezi ya
utalii wa miguu (walking safari).
7. Tozo za kupiga kambi katika Hoteli ya Twiga.
Mawasiliano ya pande mbili ni muhimu sana. Maswali kama vile huduma gani zinazopatikana ndani ya hifadhi. Je wanaojiandaa kutembelea na kutalii hifadhini wajiandae vipi?
Mambo muhimu ya kufanya na kuzingatia
(kanuni na taratibu ndani ya hifadhi)
Vifaa vyote muhimu viandaliwe na vichukuliwe vinavyohusiana na huduma ya kwanza mara punde dharura zinapojitokeza. Kanuni na taratibu ndani ya Hifadhi ni muhimu sana kupewa kipaumbele na zinafahamika. Kanuni na taratibu hifadhini zipewe kipaumbele cha hali ya juu na wageni watalii.
Vifaa muhimu vya kuchukua katika safari utalii hifadhini
Dhana zote zinazohusiana na safari utalii ya matembezi hifadhini.
Huduma za mahitaji mengineyo
Mambo ya ziada ya mahitaji yanayojitokeza na upatikanaji wake katika sehemu husika.
Maelezo ya huduma za habari utalii wa ndani.
Kampuni ya Uelimishaji,Uratibu,Uandaaji,Uhamasishaji, na Uwezeshaji Utalii wa Ndani
Follow us:
MAWASILIANO MENGINEYO MAKAO MAKUU (TANAPA)
- Juma tatu - Ijumaa
- 8:00 Asubuhi - 4:30 Jioni
+255 272508216
info@domestictourismsafaris.c info@domestictourismsafaris.co.tz



