UTALII NCHINI ‘’KWETU TANZANIA

Chanzo Cha Chimbuko Halisia Kimaelezo Na Ubunifu (Mwalimu Edgardo Kabulwa Welelo)

Ukweli Wa Mambo Kuhusiana Na ‘’Sekta Ya Utalii Nchini Kwetu Tanzania’’ Taifa Letu, ‘’Mama Tanzania’’, ni maarufu sana barani kote Afrika, Afrika Mashariki na Duniani kwa ujumla wake kutokana na kufahamika kwake katika kubarikiwa kuwa na vivutio bora na vilivyo vya kipekee vya utalii wa aina mbalimbali. Mojawapo ya vivutio vya utalii vilivyo maarufu sana nchini ‘Kwetu Tanzania’’ ni pamoja na ‘’Ardhi Tambarare’’(Southern Serengeti Plains) za kusini mwa ‘’Hifadhi ya Taifa ya Serengeti’’ (Serengeti National Park), mkoani Mara, ‘’Bonde la Ngorongoro’’ (Ngorongoro Crater/Ngorongoro Caldera/ Collapsed Volcano) au ‘’Mlima Mfu wa Volkano’’ au ‘’Kipande cha sehemu ya ukuta wa Mlima wa Volkano ulioporomoka na uliosalia baada ya mlipuko wa Volkano na kuporomekea kwa ndani (CALDERA) katika ‘’Mamlaka Ya Hifadhi Ya Ngorongoro’’ (Ngorongoro Conservation Area Authority/NCAA), mkoani Arusha (Wilaya ya Ngorongoro), Mlima Kilimanjaro (Mount Kilimanjaro), ‘’Mlima mrefu zaidi barani Afrika na uliosimama wenyewe peke yake (Free Standing Mountain) katika mita takribani 5895 kutoka usawa wa Bahari, mkoani Kilimanjaro (Wilayani Moshi Vijijini pamoja na Rombo)’’, na pia pasipo kusaha fukwe za kipekee zenye kuwa na mandhari nzuri zenye kupendeza na kuvutia katika ‘’Visiwa Vya Marashi Vya Zanzibar’’. Ikumbukwe na ifahamike ya kwamba hivi vivutio vya utalii ni mojawapo ya sehemu ndogo tu kwasababu ‘’Taifa Mama Tanzania’’ lina vivutio vingi sana katika kuizawadia na kuihudumia ‘’Dunia Ya Utalii’’. Kwa mfano hai, ‘’Hifadhi Za Misitu Asilia’’ (Natural Forests), pamoja na ‘’Mapori Ya Akiba’’ (Game Reserves) nchini kwetu Tanzania ambayo pia ni mojawapo ya uoto wa asili vinachukua eneo la ardhi yenye kuwa na takribani hekta millioni 39 ambayo ni sawa na takribani asilimia 40 ya eneo lote la ardhi ya Tanzania. Zaidi ya asilimia 25 ya eneo lote la ardhi ya ‘’Tanzania Yetu Sote’’ limetengwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya ‘’Hifadhi Mali Hai’’ (Protected Areas) kama vile ‘’Hifadhi Za Taifa’’ (National Parks), pamoja na ‘’Mapori Ya Akiba Ya Wanyamapori’’ (Game Reserves au Wildlife Reserves). Nchini kote ‘Kwetu Tanzania’’, kunapatikana takribani idadi ya zaidi ya ‘’Hifadhi za Taifa’’ (National Parks) ishirini na moja (21), ‘’Mapori Ya Akiba ya Wanyamapori’’ (Game Reserves au Wildlife Reserves) takribani ishirini na sita (26), ‘’Maeneo Ya Vitalu Vya Uwindaji’’ (Game Controlled Areas) takribani arobaini na tatu (43), na bila kusahau ‘’Hifadhi Za Taifa Za Baharini’’ (Marine Parks). Vivutio vinginevyo vya utalii nchini ‘’Kwetu Tanzania’’ ni pamoja na ‘’Utalii Wa Kiutamaduni’’ (Tanzania’s Cultural Tourism), na vilevile ‘’Maeneo Ya Kihistoria (Historical Sites) na ‘’Mali Kale’’(Tanzania’s Archaeological Sites) kama vile maeneo ya ‘’Bonde la Oldupai’’ (Olduvai Gorge) katika ‘’Mamlaka Ya Hifadhi Ya Ngorongoro’’ (Ngorongoro Conservation Area Authority) katika ‘’Mkoa wa Arusha’’ (Wilayani Ngorongoro), ‘’Mapango Ya Amboni (Amboni Caves) katika ‘’Mkoa wa Tanga’’, ‘’Magofu Ya Kilwa Kisiwani Na Songo Mnara (Ruins of Kilwa Kisiwani & Ruins of Songo Mnara), ‘’Mkoani Lindi’’ na mengineyo yaliyo mengi.

Maelezo ya huduma za habari utalii wa ndani.

MAWASILIANO MENGINEYO MAKAO MAKUU (TANAPA)

+255 272508216

info@domestictourismsafaris.c  info@domestictourismsafaris.co.tz