TALII NA TEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA GOMBE (GOMBE STREAM NATIONAL PARK)

Mkoani Kigoma katika ukanda wa Magharibi (Western region zone) mwa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania (The United Republic of Tanzania)

Chanzo Cha Chimbuko Halisia Kimaelezo Na Ubunifu (Mwalimu Edgardo Kabulwa Welelo)

Ukweli Wa Mambo Kuhusiana Na Hifadhi Ya Taifa Ya Gombe (Gombe Stream National Park) Mkoani Kigoma Katika Ukanda Wa Magharibi (Western Region Zone) Mwa Jamhuri Ya Muungano Ya Tanzania (The United Republic of Tanzania); Ni vema na busara ikafahamika ya kwamba ‘’Hifadhi ya Taifa ya GOMBE’’ (Gombe Stream National Park) ilianzishwa rasmi kwa ajili maalumu ya kuwalinda na kuwahifadhi viumbe hai wanyamapori jamii ya ‘’Nyani’’ (Primates) wanaofahamika kama ‘’Sokwe Mtu’’ (Chimpanzees) ambao kimsingi ni adimu na walio hatarini kutoweka duniani (Endangered Species).Wanyamapori wengineo jamii ya ‘’Nyani’’(Primates) wapatikanao ‘’Hifadhini Gombe’’(Gombe Stream National Park) ni pamoja na ‘’Nyani’’(Olive/Savanna Baboons), ‘’Mbega wenye kuwa na rangi mchanganyiko ya weusi na weupe’’(Black and White Colobus Monkeys), ‘’Kima’’(Blue/Syke’s Monkeys), ‘’Tumbili/Ngedere’’(Vervet/Black – Faced Monkeys), ‘’Nyani Mkia Mwekundu’’(Red – Tailed Monkeys), ‘’Aina mbili za Komba’’(Galagos/Bushbabies), pamoja na ‘’Mbega Wekundu’’(Red Colobus Monkeys). Wanyamapori wengineo ambao sio jamii ya ‘’Nyani’’(Primates) wanaopatikana katika ‘’Hifadhi ya Taifa ya Gombe’’(Gombe Stream National Park) ni kama vile ‘’Nyati/Mbogo(African/Cape/Savanna Buffalo), ‘’Nguruwe Mwitu’’(Bush Pigs), ‘’Pongo/Mbawala’’(Bushbucks), ‘’Pimbi’’(Hyraxes), pamoja na utajiri wa hali ya juu ya upatikanaji wa aina mbalimbali za viumbe hai ndege hususani ‘’Tumbusi Minazi’’(Palm Nut Vulture/Vulturine Fish Eagles). Ikumbukwe na ifahamike ya kwamba ‘’Hifadhi hii ya Taifa ya Gombe’’ (Gombe Stream National Park) ilianzishwa rasmi mnamo mwaka wa 1968 katika ‘’Mkoa wa Kigoma’’ (Kigoma Region) unaopatikana kijiografia katika ‘’Ukanda Wa Magharibi’’ (Western Region Zone) mwa ‘’Jamhuri ya Muungano ya Tanzania’’ (The United Republic of Tanzania). Hifadhi hii ya Taifa ya Gombe (Gombe Stream National Park) ilikuwa na ukubwa wa eneo la ardhi yenye kufikia kilomita za mraba takribani 52 pale ilipoanzishwa rasmi mnamo mwaka wa 1968. Lakini mpaka hivi sasa ukubwa ulio rasmi wa eneo la ardhi ya hifadhi hii ni ‘’takribani kilometa za mraba 77’’ baada ya eneo kuongezwa ukubwa wa eneo lake. Hifadhi ya Taifa ya Gombe (Gombe Stream National Park) imebarikiwa kuumbika kwa kuwa na ‘’Ukanda Mwembamba Wa Safu Ya Milima’’ yenye kuwa na urefu wa takribani kilomita 16 katika kandokando ya ‘’Mwambao wa Mashariki’’ (Eastern Shore) mwa ‘’Ziwa Tanganyika’’ (Lake Tanganyika) na pia kutawanyika eneo la nchi kavu takribani kilomita 5 mpaka katika ‘’vilele’’ vya safu ya milima ikitengeneza ‘’Kuta Za Bonde La Ufa’’ (Rift Wall/Rift Valley Escarpment). Safu hizi za milima yenye kuwa na miteremko mikali inapatikana kutoka katika usawa wa bahari kuanzia katika ‘’Ziwa Tanganyika’’(Lake Tanganyika) takribani mita 681 mpaka mita takribani 1,524 (au wakati mwingine ni sawa na mita 750 mpaka 1,500 kutoka katika usawa wa bahari).Sehemu nyingi ndani ya ‘’Hifadhi ya Taifa ya Gombe’’(Gombe Stream National Park) zenye kuwa na mabonde yenye kuwa na miteremko mikali imeingiliana na safu za milima ambapo idadi kadhaa ina vyanzo vilivyo vingi vya kudumu vya vijito vya maji. Misitu minene inayostawi kufuata mkondo wa mto(Gallery/Riverine Forests) ipatikanayo katika mabonde sambamba na miteremko ya chini ya mabonde kawaida hutoa fursa zaidi kwa ustawi wa uoto wa asili wa ‘’Miti ya Mapori’’ yenye kuwa na tabia ya upukutishaji wa majani yake kutoka katika matawi ya miti wakati wa msimu wa kiangazi kwa ajili ya kujihifadhia akiba yake ya chakula cha maji (Deciduous woodland) ambayo kawaida hupatikana katika sehemu ya juu kabisa ya miteremko ya mabonde na sehemu nyingi za vilele katika safu ya milima sanjari na kuta za bonde la ufa nazo pia zimefunikwa na kutawaliwa na uoto wa mimea ya nyasi. Ikumbukwe na ifahamike ya kwamba malengo makuu ya kimsingi na kipekee cha uanzishwaji wa ‘’Hifadhi ya Taifa ya Gombe’’ (Gombe Stream National Park) ni ‘’kuwalinda na kuwahifadhi wanyamapori jamii ya ‘’Nyani’’(Primates) hususani ‘’Sokwe Mtu’’(Chimpanzees) ambao ni adimu na pia waliopo hatarini kutoweka duniani kutokana na tishio la ujangiri (Poaching), ‘’kulinda na kuhifadhi sura na mandhari ya kijiografia pamoja na makazi yake ya kimazingira na viumbe hai vinginevyo vipatikanavyo ‘’Hifadhini Gombe’’ kwa ujumla wake kuwa endelevu na salama. Kilicho cha kipekee kabisa na pia chenye kuwa na umuhimu mkubwa ni kwamba ’’Hifadhi ya Taifa ya Gombe’’ (Gombe Stream National Park) imegawanyishwa katika kanda 4 ambazo ni pamoja na; 1.’’Ukanda wa Uongozi na Utawala Hifadhini Gombe’’ (Administrative Zone); Ukanda wa Uongozi na Utawala ‘’Hifadhini Gombe’’ (Gombe Stream National Park) kawaida unahusisha maeneo ya ‘’Majengo ya Shughuli Maalumu za Kitafiti’’ katika eneo la ‘’Mitumba’’ ambapo hupatikana ‘’Makao Makuu Ya Hifadhi’’ (The Park Headquarters), ‘’Kambi ya Kudumu ya Mahema ya Gombe’’ (The Gombe Luxury Tented Camp), na vilevile ‘’Kituo Kidogo cha Kambi kwa ajili ya shughuli za tafiti za kisayansi’’ (Small Scientific Research Camp). Katika eneo la ‘’Kasekela’’ ni eneo maalumu ambapo hupatikana huduma kama vile ‘’Mapokezi’’(Park Reception), ‘’Kituo cha Askari wa Wanyamapori’’(Ranger Post), na pia ‘’ Kituo kikubwa cha shughuli za utafiti na makao makuu ya wafanyakazi wa hifadhini’’(Gombe Stream Main Research Centre Offices & Staff), wakati ambapo katika eneo la ‘’Bwavi’’, yenyewe kawaida ni kituo cha ‘’Askari wa Wanyamapori’’(Ranger Post), sambamba kabisa na ‘’Kituo kidogo na Kambi kwa shughuli za Kitafiti’’(Small Research Camp). Huduma za malazi au kulala pia hupatikana hapa kama vile ‘’Hosteli’’, ‘’Kambi ya Kasekela’’ (Kasekela Public Campsite), pamoja na ‘’Kambi ya Mahema ya Mitumba’’ (Mitumba Tented Camp). Kilicho cha kipekee kabisa na pia chenye kuwa na umuhimu mkubwa ni kwamba ‘’Maelezo yote ya kimsingi ya kitafiti yanayohusiana na ‘’Hifadhi ya Taifa ya Gombe’’ (Gombe Stream National Park) yanapatikana yakionyeshwa katika ‘’Nyumba ya kupumzikia ya JANE GOODALL’’ (Jane Goodall Rest House) ambapo leo hii jumba hili linatumika kama ‘’jumba la kumbukumbu la kihistoria’’ (Historical Building). Je wajua ‘’Hayati Jane Goodall’’ alikuwa ni nani? Jane Goodall alikuwa mtafiti wa kisayansi aliyebobea zaidi katika utafiti wa wanyamapori jamii ya nyani’’Primates’’ hususani ‘’Sokwe Mtu’’ (Chimpanzees) na pia alitumia sehemu kubwa sana ya maisha yake enzi za uhai wake akifanya kazi katika kipindi kirefu katika ‘’Hifadhi ya Taifa ya Gombe’’. Jane Goodall alifariki mnamo mwaka wa 2025. Jamhuri ya Muungano ya Tanzania (The United Republic of Tanzania) na Watanzania kwa ujumla wake, daima milele tutamkumbuka na kumlilia ‘’Hayati Jane Goodall’’ kwa mchango wake alioutoa na kuizawadia ‘’nchi yetu Tanzania’’ katika kuwalinda na kuhifadhi ‘’Sokwe Mtu’’ (Chimpanzees). Mwenyezi ‘’Mungu’’ ampumzishe kwa amani peponi, AMEN. 2.’’Ukanda wa Uhifadhi wa Uoto wa Asili’’ (Wilderness Zone); Ukanda wa ‘’Uhifadhi wa Uoto wa Asili’’ (Wilderness Zone) kawaida ukanda huu unahusisha mazingira ya makazi ya wanyamapori jamii ya ‘’Sokwe Mtu’’ (Chimpanzees) wanayotumia kutembea na kujitafutia chakula chao cha kila siku (Home Ranges). Kimsingi kunapatikana makundi 3 yaliyo mashuhuri na maarufu ya wanyamapori jamii ya ‘’Sokwe Mtu’’ (Chimpanzees) ambayo kawaida hupatikana katika maeneo ya ‘’Mitumba’’, ‘’Kasekela’’, pamoja na ‘’Kalande’’ kama mojawapo ya maeneo yao yaliyo muhimu ya makazi ya mazingira katika kuishi na kujitafutia mahitaji yao ya chakula ya kila siku. Ikumbukwe na ifahamike ya kwamba shughuli nyingi za kiutalii hufanyika zaidi katika eneo la wanyamapori jamii ya ‘’Sokwe Mtu’’ (Chimpanzees) wanaopatikana wakiishi katika eneo la ‘’Kasekela’’, ambapo hupatikana mtandao wao wa barabara au njia zao wanazotumia kutembea katika kutafuta na kujipatia mahitaji yao ya chakula cha kila siku. 3.’’Ukanda Wa Fukwe Za Ziwa Tanganyika’’ (Lake Tanganyika Beach Zone); Ukanda wa fukwe za ‘’Ziwa Tanganyika’’ (Lake Tanganyika Beach Zone) kawaida unakadiriwa kuwa na urefu wa takribani kilomita 16 katika kandokando ya ‘’Mwambao wa Ziwa Tanganyika’’ na pia ina upana unaokadiriwa takribani mita 90 ambapo kwa ujumla wake unachukua ukubwa wa eneo wa takribani hekari 141. 4. ‘’Ukanda wa Ziwa Tanganyika Lenyewe’’ (Lake Tanganyika Zone); Ukanda wa ‘’Ziwa Tanganyika’’ (Lake Tanganyika) unachukua ukubwa wa takribani kilomita moja ya ziwa. Ukanda huu wa eneo kawaida unalinda na kuhifadhi utajiri wa viumbe hai wa aina mbalimbali wanaopatikana katika eneo hili lenye kuwa na kina kifupi cha maji ya ‘’Ziwa Tanganyika’’ katika mwambao wa ziwa. Wageni watalii hupendelea sana eneo hili kwa ajili ya lango la kuingilia hifadhini, kuogelea, kuota jua kwenye fukwe zenye kuwa na kichanga, pamoja na kupiga kambi nyakati za usiku. Ni vema na busara ikakumbukwa na kueleweka ya kwamba ‘’Hifadhi ya Taifa ya Gombe’’(Gombe Stream National Park) inapatikana ndani ya ‘’Bonde Kuu La Ufa’’(Great Rift Valley) la ‘’Mkondo Wa Bonde La Ufa Wa Magharibi’’ (Western Rift Valley/Albertine Rift Valley/Western Branch) ambalo asili na chimbuko lake limeanzia mpakani mwa ‘’Mataifa Mawili’’ ya ‘’DRC na UGANDA’’ kupitia ‘’Ziwa Albert’’(Lake Albert), ziwa ambalo kimsingi linapatikana mpakani mwa nchi ya ‘’DRC na UGANDA’’ na kuteremkia na kutawanyika kuelekea katika upande wa kusini katika maziwa kama vile ‘’Ziwa Edward’’(Lake Edward), ‘’Ziwa Kivu’’(Lake Kivu) na hatimaye ‘’Ziwa Tanganyika’’(Lake Tanganyika), ‘’Ziwa Rukwa’’(Lake Rukwa), na ‘’Ziwa Nyasa/Malawi’’(Lake Nyasa/ Malawi) ikiungana na ‘’Mkondo Wa Bonde La Ufa Wa Upande Wa Mashariki (Eastern Rift Valley/Gregory Rift) ambapo mkondo huu wa ‘’Bonde La Ufa Wa Mashariki’’(Eastern Rift Valley) asili na chimbuko lake umeanzia katika upande wa ‘’Kaskazini’’ mwa nchi ya Kenya kupitia ‘’Ziwa Turkana/Rudolf’’(Lake Turkana/Rudolf). Vijiji vinavyopakana kimipaka na ‘’Hifadhi ya Taifa ya Gombe’’ (Gombe Stream National Park) ni pamoja na kijiji cha ‘’Mwamgongo’’ (The Mwamgongo Village) katika upande wa ‘’Kaskazini’’, wakati ambapo kijiji cha ‘’Kazinga’’ (The Kazinga Village) ni katika upande wa ‘’Kusini’’. Upande wa ‘’Magharibi’’ mwa ‘’Hifadhi ya Taifa ya Gombe’’ (Gombe Stream National Park) ni ‘’Ziwa Tanganyika’’(Lake Tanganyika) ambalo kimsingi wake asili na chimbuko lake ni ziwa lililotokana na ‘’Bonde Kuu la Ufa’’ (The Great Rift Valley) likifahamika kama (Rift Valley Lake) kama maziwa mengineyo nchini kwetu Tanzania na ‘’Afrika Mashariki’’ kwa ujumla wake kama vile ‘’ Ziwa Manyara’’(Lake Manyara), ‘’Ziwa Burungi’’(Lake Burungi), ‘’Ziwa Babati’’(Lake Babati), ‘’Ziwa Eyasi’’(Lake Eyasi), ‘’Ziwa Nyasa/Malawi’’(Lake Nyasa/Malawi), ‘’Ziwa Rukwa’’(Lake Rukwa), pamoja na ‘’Ziwa Natron’’, kwa upande wa nchini kwetu Tanzania. Katika Taifa la Jamhuri ya ‘’Kenya’’ katika upande wa ‘’Kaskazini’’ mwa nchi hiyo kupitia katika ‘’Mkondo Wa Mashariki Wa Bonde La Ufa’’(Eastern Rift Valley/Gregory Rift) ni pamoja na ‘’Ziwa Turkana/Rudolf’’(Lake Turkana/Rudolf), ‘’Ziwa Baringo’’(Lake Baringo), ‘’Ziwa Bogoria’’(Lake Bogoria), ‘’Ziwa Nakuru’’(Lake Nakuru), ‘’Ziwa Elmentaita’’(Lake Elmentaita), ‘’Ziwa Naivasha’’(Lake Naivasha), pamoja na ‘’Ziwa Magadi’’(Lake Magadi). Ikumbukwe na ifahamike ya kwamba ziwa nambari moja barani kote Afrika na pia nambari mbili duniani kwa kuwa na kina kirefu ni ‘’Ziwa Tanganyika’’(Lake Tanganyika) likizidiwa kete na ‘’Ziwa Baikal’’(Lake Baikal) linalopatikana ‘’SIBERIA’’ katika nchi ya ‘’URUSI’’ kama ziwa lenye kuwa na kina kirefu zaidi kuliko maziwa yote yapatikanayo duniani. Vilevile pia ‘’Ziwa Tanganyika’’ (Lake Tanganyika) ndio ziwa lililo refu zaidi barani Afrika, wakati ambapo ‘’Ziwa Nyasa/Malawi’’ (Lake Nyasa/Malawi) nalo pia ni ziwa nambari mbili barani Afrika kwa kuwa na kina kirefu baada ya ‘’Ziwa Tanganyika’’ (Lake Tanganyika). Ziwa Tanganyika (Lake Tanganyika) pia ni ziwa nambari mbili kwa ukongwe zaidi duniani lenye kuwa na umri unaokadiriwa takribani miaka millioni 12 iliyopita.

Ushauri kwa watalii Raia wa Tanzania katika kujiandaa na kujipanga kimaandalizi kwa Safari Utalii

awe (260 of 266)

Hiki ni kipaumbele nambari moja kuliko vyote ambacho kawaida hutoa muelekeo na taswira ya uwepo wa safari utalii ya matembezi hifadhini au hapana. Aina ya usafiri utakaotumika kufika hifadhini na gharama zake. Haya yote yanahitaji rasilimali fedha na mipango madhubuti

‘’Hifadhi ya Taifa ya Gombe’’ (Gombe Stream National Park) ilianzishwa rasmi mnamo mwaka wa 1968, na ilipoanzishwa mwaka huo ukubwa wa eneo lake kwa ujumla wake ilikuwa ni kilomita za mraba 52. Lakini leo hii ‘’Hifadhi ya Taifa ya Gombe’’ (Gombe Stream National Park) ina ukubwa wa eneo unaokadiriwa kufikia kilometa za mraba 77 baada ya eneo lake kuongezwa kwa ukubwa wa eneo kwa ajili ya uhifadhi endelevu wa hifadhi yenyewe. Kijiografia, ‘’Hifadhi hii ya Taifa ya Gombe’’(Gombe Stream National Park) inapatikana umbali wa takribani kilomita 24 katika upande wa ‘’Kaskazini’’ mwa ‘’Mji wa Kigoma’’(Kigoma Town), Mkoani Kigoma katika upande wa ‘’Kaskazini Magharibi’’ mwa ‘’Jamhuri ya Muungano ya Tanzania (The United Republic of Tanzania) mwa ‘’Ukanda Wa Magharibi’’ (Western Region Zone).

Ni vema na busara ikafahamika na kueleweka ya kwamba ‘’Hifadhi ya Taifa ya Gombe’’ (Gombe Stream National Park) wakati ilipoanzishwa rasmi mnamo mwaka wa 1968, ukubwa wa eneo la ‘’Hifadhi ya Taifa ya Gombe ‘’(Gombe Stream National Park) ilikuwa ni kilomita za mraba takribani 52. Leo hii ‘’Hifadhi ya Taifa ya Gombe’’ (Gombe Stream National Park) ina ukubwa wa eneo unaokadiriwa kufikia takribani kilomita za mraba 77 baada ya eneo lake kutanuliwa na kuongezwa ukubwa wa eneo kwa ajili ya uhifadhi endelevu kimikakati katika kulinda na kuhifadhi viumbe hai vipatikanavyo ndani ya hifadhi.

‘’Hifadhi ya Taifa ya Gombe’’ (Gombe Stream National Park) inafikika zaidi kwa njia ya usafiri wa majini kupitia ‘’Ziwa Tanganyika’’ (Lake Tanganyika). Ni sawa na takribani kilomita 24 kutokea katika ‘’Mji Wa Kigoma’’ (Kigoma Town) katika upande wa ‘’Kaskazini’’. Kijiografia, hifadhi hii ya ‘’Taifa ya Gombe’’ (Gombe Stream National Park) inapatikana katika ‘’Upande Wa Mashariki Mwa Mwambao Wa Ziwa Tanganyika (Lake Tanganyika Eastern Shore) takribani kilomita 24, kaskazini mwa ‘’Mji wa Kigoma’’ (Kigoma Town). Ni sawa na mwendo wa umbali wa saa 1 mpaka 3 kutokea ‘’Kigoma Mjini’’(Kigoma Town) kwa kutumia njia ya usafiri wa majini wa boti zenye kutumia injini. Ni vema na busara ikafahamika na kueleweka ya kwamba ‘’Hifadhi ya Taifa ya Gombe’’(Gombe Stream National Park) inapatikana ndani ya ‘’Bonde Kuu La Ufa’’(The Great Rift Valley), katika ‘’Mkondo Wa Bonde Kuu La Ufa Wa Upande Wa Magharibi’’(The Western Rift Valley/Albertine Rift Valley/Arm), ambapo hupatikana fursa ya kipekee ya kujionea mandhari nzuri yenye kupendeza na kuvutia kama vile sura ya kijiografia ya ‘’Kuta Za Milima Ya Bonde La Ufa’’(Rift Wall/Rift Valley Escarpment) ikitawanyikia upande wa magharibi katika ‘’Ziwa Tanganyika ‘’(Lake Tanganyika), uoto wa asili wa misitu na mapori(Forests & Woodland) na maeneo wazi ya uoto wa nyasi(Open Plains/Grassland), na bila kusahau ‘’Maporomoko ya Maji katika Mito ya Kakombe na Mkenke (Kakombe and Mkenke Riverine Waterfalls).

Milima (Mountains), ‘’Ziwa Tanganyika’’ (Lake Tanganyika), ‘’Mkondo Wa Magharibi Wa Bonde Kuu La Ufa’’ (Western Rift Valley/Western Branch), na pia ‘’Kuta Za Bonde Kuu La Ufa’’ (Rift Wall/Rift Valley Escarpment).

Inaanzia takribani ‘’mita 750 mpaka 1500’’ kutoka katika usawa wa Bahari. Au wakati mwingine ni sawa mita 681 inayoanzia katika ‘’Ziwa Tanganyika’’ (Lake Tanganyika) mpaka katika ‘’vilele vya milima’’ takribani mita 1524.

Ikumbukwe na ifahamike ya kwamba ‘’Hifadhi ya Taifa ya Gombe’’(Gombe Stream National Park) ni mojawapo ya hifadhi iliyo maarufu na mashuhuri ulimwenguni kote kutokana na tafiti nyingi zaidi kufanyika katika wanyamapori jamii ya ‘’Nyani’’(Primates) tokea mnamo miaka ya 1960, hususani zaidi wanyamapori jamii ya ‘’Nyani’’(Primates) wanaofahamika kama ‘’Sokwe Mtu’’(Chimpanzees). Aina (Races/Subspecies) ya ‘’ Sokwe Mtu’’ (Chimpazees) anayepatikana hapa ‘’Hifadhi ya Taifa ya Gombe’’ (Gombe Stream National Park) inafahamika katika jina lake la kisayansi kama (Pan troglodytes schweinfurthii). Hifadhi nyinginezo za Taifa (National Parks) nchini kwetu Tanzania ambapo hupatikana ‘’Sokwe Mtu’’(Chimpanzees) ni pamoja na ‘’Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale’’(Mahale Mountains National Park) ambayo pia nayo inapatikana ‘’Mkoani Kigoma’’(Kigoma Region) katika upande wa kusini mwa ‘’Mji wa Kigoma’’(Kigoma Town) katika mwambao wa mashariki wa ‘’Ziwa Tanganyika’’, na bila kusahau ‘’Hifadhi ya Taifa ya Visiwa vya Rubondo’’(Rubondo Islands National Park) inayopatikana ‘’Mkoani Mwanza’’(Mwanza Region) katika ‘’Ziwa Victoria/Nyanza’’(Lake Victoria/Nyanza). Ikumbukwe na ifahamike ya kwamba ‘’Sokwe Mtu’’ (Chimpanzees) wanaopatikana hapa ni wale ambao walioletwa kutokea ‘’Afrika ya Magharibi’’ (West Africa). Aina (Races/Subspecies) inayopatikana hapa inafahamika katika jina lake la kisayansi kama (Pan troglodytes verus).Kunapatikana takribani aina 7 mpaka 8 za wanyamapori aina ya ‘’Nyani’’(Primates) katika ‘’Hifadhi ya Taifa ya Gombe’’ (Gombe Stream National Park).Miongoni mwao ni pamoja na; ‘’Nyani’’(Olive/Savanna/Anubis Baboon), ‘’Kima’’(Blue/Syke’s Monkeys), ‘’Nyani Mkia Mwekundu’’(Red – Tailed Monkeys),’’Tumbili/Ngedere’’(Vervet/Black – Faced Monkeys),‘’Mbega Wekundu’’(Red Colobus Monkeys), pamoja na aina(Races/Subspecies) mbili za ‘’Komba’’(Bushbabies/Galagos), ambazo ni ‘’Octolemun crassicaudatus’’ na ‘’Galago matschieri’’, katika majina yao ya kisayansi. Vivutio vinginevyo vilivyo vikuu ni pamaja na ‘’Misitu Minene’’(Dense Forests), ‘’Ziwa Tanganyika’’(Lake Tanganyika), ‘’Mabonde yenye kuwa na vijito kadhaa vya maji’’(Valley with streams), ‘’Maporomoko ya Maji katika Mito ya Kakombe na Mkenke’’(Kakombe and Mkenke Riverine Waterfalls), ‘’Maporomoko ya Maji katika Mito’’(Riverine Waterfalls), na pia ‘’Sehemu ya Makutano’’ (Meeting Place) ambapo wavumbuzi maarufu kihistoria ambao walikuwa ni ‘’Dr. David Livingstone’’ na ‘’Henry Morton Stanley’’ walikutana katika ‘’Mji wa Ujiji’’, Mkoani Kigoma, katika harakati zao za utafutaji wa ‘’Chanzo Cha Mto Nile’’(River Nile Source). Na ni katika sehemu hii ya ‘’Mji wa Ujiji’’, yaliandikwa maneno kwa ajili ya kumbukizi ya wawili hawa walipokutana mnamo tarehe 10 ya ‘’Mwezi Novemba’’ ya mwaka 1871, ambayo yanasomeka katika lugha ya ‘’Kiingereza’’, kama ‘’Dr.Livingstone, I presume’’. Kilicho cha kipekee na pia chenye kuwa na umuhimu wake ni pamoja na ‘’Ziwa Tanganyika’’ (Lake Tanganyika). Ziwa Tanganyika (Lake Tanganyika), ndio ziwa ambalo ni refu zaidi na pia lenye kuwa na kina kirefu zaidi kuliko maziwa yote yanayopatikana barani kote ‘’Afrika’’, na vilevile ‘’Ziwa Tanganyika’’(Lake Tanganyika) ni ziwa nambari mbili duniani kwa kuwa na kina kirefu, likizidiwa kete na ‘’Ziwa Baikal’’ kwa kuwa na kina kirefu, ambalo linapatikana katika ‘’Mji Wa Siberia’’, nchini ‘’URUSI’’(Russia). Urefu wa kina cha maji ya ‘’Ziwa Tanganyika’’ (Lake Tanganyika) unakadiriwa ni takribani ‘’Futi 4,710’’ au sawa na ‘’Mita 1,436’’, wakati ambapo kina cha ‘’Ziwa Baikal’’, unakadiriwa ni takribani ‘’Futi 6,365’’, au sawa na ‘’Mita 1,940’’. Kingine cha ziada ni kwamba ‘’Ziwa Tanganyika’’(Lake Tanganyika) pia ni ziwa ambalo ni nambari mbili ulimwenguni kwa ukongwe na inakadiriwa kisayansi na kitafiti kuwa na umri wa takribani miaka million 12 iliyopita na vilevile lina utajiri wa hali ya juu ya upatikanaji wa aina mbalimbali za viumbe hai. Na ukweli wa mambo ni kwamba ‘’Ziwa Tanganyika’’(Lake Tanganyika) pia linahifadhi ndani yake viumbe hai asilia vinavyopatikana hapa tu na sehemu nyingine havipatikani (Endemic/Native) kama vile viumbe hai wanaotambaa (Reptiles), ‘’Viumbe hai wasiokuwa na uti wa mgongo(Invertebrates), sambamba na ‘’Nyoka Kobra wa Majini’’(Water Cobras).Viumbe hai vinginevyo vipatikanavyo ndani ya ‘’Ziwa Tanganyika’’(Lake Tanganyika) ni kama vile aina mbili za samaki aina ya ‘’Dagaa’’(Sardine), ambao wanafahamika katika majina yao ya kisayansi kama ‘’Stolothrissa tanganyikae’’, na pia ‘’Limnothrissa miodon’’. Ni vema na busara ikafahamika na ikaeleweka ya kwamba ‘’Ziwa Tanganyika’’(Lake Tanganyika) linapatikana katika ‘’Bonde Kuu La Ufa’’(The Great Rift Valley) katika ‘’Mkondo wa Bonde La Ufa wa Upande Wa Magharibi’’(The Western Rift Valley/Western Branch/Albertine Rift Valley) ambapo mkondo huu asili na chimbuko lake umeanzia mpakani mwa mataifa mawili ya ‘’DRC na UGANDA’’, kupitia ‘’Ziwa Albert’’(Lake Albert) ambalo kimsingi nalo pia lipo mpakani mwa nchi ya ‘’DRC na UGANDA’’, na kuteremka na kutawanyika katika uelekeo wa upande wa ‘’Kusini’’, kuelekea ‘’Ziwa Edward’’(Lake Edward), ‘’Ziwa Kivu’’(Lake Kivu), ‘’Ziwa Tanganyika’’(Lake Tanganyika),‘’Ziwa Rukwa’’(Lake Rukwa), na hatimaye ‘’Ziwa Nyasa/Malawi’’(Lake Malawi/Nyasa) na kuweza kuungana tena na ‘’Bonde Kuu La Ufa la Mkondo wa Mashariki’’(The Eastern Rift Valley/Gregory), mkondo ambao asili na chimbuko lake umeanzia ‘’Kaskazini Mwa Taifa la Kenya’’, likipitia na kuanzia ‘’Ziwa Turkana/Rudolph’’(Lake Turkana), ‘’Ziwa Baringo’’(Lake Baringo), ‘’Ziwa Bogoria’’(Lake Bogoria), ‘’Ziwa Nakuru’’(Lake Nakuru), ‘’Ziwa Elmentaita’’(Lake Elmentaita), ‘’Ziwa Naivasha’’, na hatimaye ‘’Ziwa Magadi’’(Lake Magadi). Baada ya hapo ‘’Mkondo huu wa Bonde Kuu La Ufa wa Upande wa Mashariki’’(The Eastern Rift Valley/Gregory Rift) unaendelea kutawanyika katika uelekeo wa ‘’Kaskazini Mwa Tanzania’’(Tanzania’s Northern Zone) na kupitia ‘’Ziwa Natroni’’(Lake Natron), ‘’Ziwa Eyasi’’(Lake Manyara), ‘’Ziwa Babati’’, ‘’Ziwa Burungi’’(Lake Burungi) katika ‘’Hifadhi ya Taifa ya Tarangire’’(Tarangire National Park) pamoja na maziwa mengi madogomadogo yapatikanayo ‘’Mkoani Manyara), kabla ya kuelekea kusini mwa nchi na kuungana na ‘’Ziwa Nyasa/Malawi, ambapo ‘’Ziwa Malawi/Nyasa’’(Lake Malawi/Nyasa) ni katika mkondo wa ‘’Bonde Kuu La Ufa wa Upande Wa Magharibi’’(The Western Rift Valley/Albertine Rift Valley). Ikumbukwe na ifahamike ya kwamba ‘’Mkoa wa Manyara’’(Manyara Region), upatikanao katika ‘’Ukanda Wa Kaskazini Mwa Tanzania’’(Tanzania’s Northern Zone), ndio mkoa pekee uliopitiwa zaidi na ‘’Mkondo

Kumeripotiwa na kurekodiwa kitafiti na kisayansi kupatikana na vilevile kutambulika ndani ya ‘’Hifadhi ya Taifa ya Gombe’’(Gombe Stream National Parks), zaidi ya spishi 35 za viumbe hai, hii ni pamoja na aina kadhaa za ‘’Mammalia’’(Mammals), kama vile ‘’Pongo’’(Bushbucks), ‘’Nguruwe Mwitu’’(Bushpigs), ‘’Chui’’(Leopards), ‘’Funo’’(Duikers), ‘’Fungo’’(Civets), ‘’Nguchiro Mkia Mweupe’’(White – Tailed Mongoose), ‘’Njule/Isanje’’(Elephant Shrew),’’Ngiri’’(Common Warthog), ‘’Pimbi’’(Hyraxes), ‘’Nyati/Mbogo’’(African/Cape/Savanna Buffalo), ‘’Kuro’’(Common Waterbuck).Ikumbukwe na ifahamike ya kwamba katika ‘’Hifadhi ya Taifa ya Gombe’’(Gombe Stream National Park) kunapatikana takribani aina ‘’7 mpaka 8’’ za wanyamapori jamii ya ‘’Nyani’’(Primates), kama vile ‘’Sokwe Mtu’’(Chimpazees), ‘’Aina (Races/Subspecies) 2 za ‘’Komba’’(Galagos/Bushbabies) wanaofahamika katika majina yao ya kisayansi kama ‘’Octolemun crassicaudatus’’ na ‘’Galago matschieri’’. Wengineo ni pamoja na ‘’Nyani Mkia Mwekundu’’ (Red – Tailed Monkeys), ‘’Mbega Wekundu’’ (Red Colobus Monkeys), ‘’Tumbili/Ngedere’’ (Vervet/Black – Faced Monkeys), ‘’Kima’’ (Blue/Syke’s Monkeys), na pia ‘’Nyani’’ (Olive/Savanna/Anubis Baboon). Hata hivyo, pia kunapatikana aina kadhaa za mammalian wadogowadogo. Zaidi ya spishi takribani 250 za viumbe hai ‘’Ndege’’ (Birds) wameripotiwa na kutambulika wakiishi ndani ya ‘’Hifadhi ya Taifa ya Gombe’’ (Gombe Stream National Park). Pia panapatikana idadi kadhaa za ‘’Viumbe hai wanaotambaa (Reptiles)’’, kama vile nyoka aina ya ‘’Chatu’’(Pythons), ‘’Kenge’’(Nile Monitors), ‘’Nyoka Kobra wa Majini’’(Water Cobra Snakes), na bila kusahau utajiri mkubwa wa upatikanaji wa viumbe hai wadudu(Insects), hususani ‘’Vipepeo’’(Butterflies).

Hifadhi ya Taifa ya Gombe (Gombe Stream National Park) inapatikana ndani ya ‘’ukanda wa uoto wa asili ‘’ unaofahamika kama ‘’uoto wa asili wa mimea miti ya miombo’’(Miombo Woodland/Zambezian Region) ambayo imechukua takribani nusu ya eneo la ardhi ya Tanzania katika maeneo mengi ya kusini, kati na magharibi wan chi ya Tanzania, ambapo hupatikana ‘’Koo’’(Genera) za mimea ya Miti kama vile ‘’Julbernardia’’, ‘’Isoberlinia’’, pamoja na ‘’Brachystegia’’. Aina nyinginezo za uoto wa asili ni pamoja na ‘’uoto wa mimea nyasi wa milimani’’(Mountain/Montane Grassland), ‘’uoto wa asili wa miti ya misiti unaostawi kufuata mkondo wa mto’’(Gallery/Riverine Forests) na kadha wa kadhalika. Misitu ya Gombe ina viashiria ya uasili wa ‘’Afrika ya Magharibi, Mashariki, pamoja na Kusini mwa Afrika’’, ambapo hupatikana ‘’Koo’’ (Genera) za mimea kama vile ‘’Pleiotaxis’’, ‘’Maerua’’, ‘’Piliostigma, na pia ‘’Vernonia’’. Pia kunapatikana idadi kadhaa ya mimea miti ya matunda ambayo hutoa fursa ya upatikanaji wa chakula cha kutosheleza na kilicho muhimu kwa wanyamapori ‘’Sokwe Mtu’’ (Chimpanzees) pamoja na aina nyinginezo za viumbe hai.

Inashauriwa na kupendekezwa kwa ‘’Watanzania Watalii’’ wa ndani wakajibebea vyakula vyao wenyewe vya kujipikia. Vilevile, hoteli zenye kutoa huduma za vyakula zinapatikana.

Wageni watalii wa ndani huweza kujipatia huduma za malazi au kulala zinazopatikana katika ‘’Nyumba Kadhaa Za Kulala Wageni’’ (Guest Houses), pamoja na ‘’Lodges’’, katika ‘’Mji wa Kigoma’’ (Kigoma Town) kama vile, ‘’Railway Hotel’’, ‘’Lake View Hotel’’, pamoja na ‘’Community Centre’’. Usafiri wa majini wa utumiaji ‘’BOTI’’ (BOAT) zenye kutumia injini kwa ajili ya kukodisha kuelekea katika ‘’Hifadhi ya Taifa ya Gombe’’ (Gombe Stream National Park) hupatikana katika ‘’Mji wa Kigoma’’ (Kigoma Town).

Ni pamoja na jumla ya mambo yenye kuwa na msingi katika safari utalii ya matembezi hifadhini kukamilika.

Maelezo muhimu wapatiwe ‘’Watanzania Watalii’’ wa ndani ya kwamba wanapokuwepo hifadhini ni nini kilicho cha muhimu kinachotakiwa wawenavyo na pia kufanya. Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba maelezo kabla ya safari utalii ya matembezi hifadhini ni kitu muhimu kilicho cha msingi ili kuweza kuepuka matatizo ambayo huweza kujitokeza katika safari utalii ya matembezi hifadhini.

Mambo muhimu ya kufahamu na kujiuliza

Ratiba ya safari utalii ya matembezi hifadhini, utaratibu na mpangilio mzima wa safari utalii uko vipi. Hali kadhalika safari utalii ya matembezi hifadhini ni ya muda wa siku ngapi? Je, fedha zenu mlizo nazo zinatosheleza au hapana. Kanuni na taratibu ndani ya hifadhi ni mambo ya kisheria yanayotakiwa kufuata pale ambapo watalii wanapokuwa hifadhini.

_MG_0840

Vifaa muhimu vya kuchukua katika safari utalii hifadhini

Vifaa vyote vilivyo muhimu vinavyohitajika katika matembezi yenu hifadhini. Hii inategemeana zaidi na jinsi mlivyojipanga.

Huduma za mahitaji mengineyo

Mambo ya ziada ya mahitaji yatakayojitokeza na upatikanaji wake katika sehemu husika mlipo katika safari utalii yenu ya matembezi hifadhini.

Maelezo ya huduma za habari utalii wa ndani.

MAWASILIANO MENGINEYO MAKAO MAKUU (TANAPA)

+255 272508216

info@domestictourismsafaris.c  info@domestictourismsafaris.co.tz