TALII NA TEMBELEA HIFADHI YA TAIFA SAADANI

Mkoani Tanga na mkoani pwani katika mwambao wa pwani ya jamhuri ya muungano wa Tanzania

Chanzo Cha Chimbuko Halisia Kimaelezo Na Ubunifu (Mwalimu Edgardo Kabulwa Welelo)

Ukweli Wa Mambo Kuhusiana Na Hifadhi Ya Taifa SAADANI (Tanga & Pwani); Hifadhi ya Taifa ya Saadani Mkoani Pwani pamoja na Tanga ipatikanayo katika Pwani ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na AFRIKA MASHARIKI imebeba jina la kijiji cha SAADANI ambacho ni cha kihistoria kilichoanza kama kambi ya uvuvi kuanzia katika karne ya 19. Chimbuko halisia la jina Saadani ni mseto wa maneno mawili ya Kiswahili yaliyokosewa kutamkwa ambayo ni saa na ndani. Maneno haya yalikuwa yakitamkwa na mfanyabiashara 32 - mwenye asili ya Kiarabu wakati akiwaelekeza wafanyakazi na wateja wake saa ilipo ambao walikuwa wakiulizia muda mara kwa mara. Ili kupunguza usumbufu kwake yeye kuingia ndani kila wakati aliwaeleza wateja wake pamoja na wafanyakazi wake ya kwamba saa iko ndani kwa kutamka Saa – dani ili waingie kuangalia muda wao wenyewe. Hatimaye mfanyabiashara huyo mwenye asili ya Kiarabu akapewa jina hilo la Saa – dani ambaye yeye alilikosea katika kulitamka akiwa na nia njema na nzuri ya kusema Saa iko ndani. Mtaa aliokuwa akiishi mfanyabiashara huyo ukaitwa Saa – dani na hatimaye ukawa ndio mwanzo wa jina la kijiji cha Saadani ambacho hapo zamani kilijulikana kwa jina la UTONDWE. Hifadhi ya Taifa Saadani ilitangazwa rasmi mnamo mwaka wa 2005 ikiwa na ukubwa wa kilometa za mraba 1,148 ambazo ni nchi kavu ambapo kilometa za mraba 30 ni eneo la bahari (kwa ujumla eneo lote la hifadhi ya SAADANI ni kilometa za mraba 1,178). Ni Hifadhi pekee nchini Tanzania na Afrika ya Mashariki yenye fukwe za bahari na inayotazamana na Bahari ya Hindi. Vilevile ni Hifadhi pekee ambapo fukwe za bahari zake zinakutana na uoto wa asili wa nchi kavu (kwa maana nyingine eneo pekee ambapo nyika na bahari hukutana). Uwepo wa hifadhi ya Taifa ya Saadani ni matokeo ya pori la akiba la Saadani, ranchi ya mkwaja na sehemu ya kaskazini ya mkwaja sambamba na akiba ya msitu wa asili wa Zaraninge, pamoja na maeneo mengineyo kama vile Mto Wami, Kisauke Sisal Estate, Madete green turtle, pamoja na Fungu Buyuni Coral Reef. Hifadhi hii inapatikana kijiografia baina ya Mkoa wa Tanga na Pwani

Ushauri kwa watalii raia wa tanzania katika kujiandaa na kujipanga kimaandalizi na kikamilifu kwa safari utalii

Ni pamoja na kufahamu gharama za jumla za safari utalii yenu ya matembezi na kutalii hifadhini Saadani. Ufahamu wa maandalizi haya yazingatie mambo muhimu ya kimsingi kama vile aina ya usafiri mtakayoimudu kwa mujibu wa uwezo wenu kifedha na kiuchumi, sehemu za huduma za chakula, malazi au kulala na mengineyo yatakayojitokeza. Baada ya haya yote kutekelezwa kwa ukamilifu na umakini mkubwa kitakachofuatilia ni mpango mkakati wa fedha za maandalizi zilizopatikana. Mwisho kabisa ni bajeti ya fedha za maandalizi kuandaliwa jinsi zilivyopangiliwa.

Hifadhi ya Taifa Saadani ilianzishwa na kutangazwa rasmi mnamo mwaka wa 2005, ikiwa na eneo lenye kuwa na kilometa za mraba takribani 1,178. Tangu mnamo miaka ya 1960, eneo hili la Saadani ilikuwa ni moja ya maeneo ya pori la akiba la wanyamapori. Hifadhi ya Taifa Saadani inapatikana kwa ukaribu katika miji ya kihistoria ya Bagamoyo, Pangani na Zanzibari ambayo kimsingi wake ilishamiri sana kwa nyakati zake wa kipindi cha biashara ya watumwa.

Ukubwa wa eneo la Hifadhi ya Taifa Saadani ni jumla ya ukubwa wa eneo lenye kuwa na kilometa za mraba 1,178. Nchi kavu inachukua ukubwa wa kilometa za mraba 1,148 ambapo kilometa za mraba 30 ni eneo la maji ya bahari ya Hindi.

Hifadhi ya Taifa Saadani inapatikana kijiografia kando kando ya pwani ya bahari ya Hindi katika mikoa ya Tanga na Pwani ndani ya wilaya za Bagamoyo, Pangani na Handeni. Hifadhi inapatikana kijiografia Kaskazini mwa miji ya Dar es Salaam na Bagamoyo takribani umbali wa kilometa 220 kwa kupitia Chalinze, Msata Mandera hadi Miono. Vilevile inafikika umbali wa kilometa 50 kutoka visiwa vya Zanzibari kupitia mkondo wa Zanzibari na inachukua takribani saa 3 kwa njia ya usafiri wa majini wa kutumia ngalawa na vilevile ni dakika takribani 40 kwa njia ya usafiri wa majini wa kutumia boti. Vilevile ni sawa na umbali wa kilometa 45 kutoka mji mkongwe wa kihistoria wa Bagamoyo (dakika 40) na Dar es Salaam ni kilometa 100 ambapo ni sawa na mwendo wa kawaida wa gari takribani saa mbili. Muda mzuri na bora wa kutembelea na kutalii Hifadhi ya Saadani ni mwezi wa Januari na Februari na vilevile mwezi Juni mpaka Agosti.

Tambarare za pwani, vilima vidogo vidogo, mlima kiono unaohifadhi msitu wa asili wa Zaraninge kwa upande wa Kusini Magharibi. Upande wa Kaskazini wa Mkwaja una mandhari nzuri yenye kupendeza ya makazi ya vilima vya hapa na pale. Kwa upande wa kusini ni Bonde la Mto Wami.

Hali ya hewa ya Hifadhi ya Taifa Saadani ni ile ambayo ni ya ukanda wa Pwani ya Afrika Mashariki ambapo hupatikana misimu miwili ya mvua katika kiwango cha takribani milimita 800 mpaka 1000 kwa mwaka. Hali ya hewa kutoka usawa wa bahari inaanzia 0 mpaka 350. Hifadhi hupata misimu miwili ya mvua na kiangazi kama kwaida ya ukanda wa pwani. Mvua za masika huanza mwezi Machi hadi Mei na za vuli huanza Novemba hadi Desemba. Kiangazi huanza mwezi Juni hadi Oktoba na kurudia tena mwezi Januari hadi Machi. Wageni watalii na Watanzania watalii wanashauriwa kutembelea na kutalii hifadhi ya Saadani wakati wa msimu wa kiangazi ambapo ni mwezi Juni hadi Oktoba pamoja na Januari hadi Machi. Hata hivyo, hifadhi ya Saadani inaweza pia kutembelewa katika nyakati zote katika mwaka kutokana na kuwa na mvuto wake wa kipekee. Februari na Julai ni miezi mikame zaidi yenye kuwa na kiwango cha juu zaidi cha joto kinachofikia takribani nyuzi joto 29.

  1. Mila na desturi za wakazi wenyeji wa makabila ya ukanda wa Pwani.
  2.  Maeneo mazuri ya mabaki ya kihistoria.
  3. Misitu ya mikoko na ile ya ukanda wa Pwani. 
  4. Takribani zaidi ya spishi 200 za viumbe hai ndege wakiwemo ndege wahamaji kama vile Heroe pamoja na mazalia ya kasa.
  5. Aina mbalimbali za wanyamapori kama vile ndovu, simba, nyati, kiboko, nyani, ngiri, na wengineo lukuki bila kusahau viumbe hai wanaotambaa kama vile mamba.
  6. Fukwe nzuri zenye uasilia wake halisi.
  7.  Maji ya bahari yanayokutana na maji ya mto (Estuaries).
  8. Mto Wami maarufu kwa upatikanaji wake wa aina mbalimbali za wanyama na ndege.
    ○ Aina mbalimbali za viumbe hai wa baharini na fungu la mchanga Mafui.
    ○ Mandhari nzuri yenye kupendeza na kuvutia ya muunganiko wa nyika na Bahari.
    ○ Misitu minene ya Pwani ya Afrika Mashariki katika eneo la Zaraninge

Safari utalii wa utazamaji wanyamapori nyakati za mchana na usiku.
i. Utazamaji ndege pamoja na utambuaji wake.

ii. Safari utalii wa matembezi ya miguu katika msitu wa asili wa Zaraninge.

  1. iii.Utazamaji vivutio katika safari utalii wa utumiaji magari.
    iv. Safari utalii wa utumiaji mitumbwi pamoja na boti katika mto Wami.
    v.  Safari utalii wa matembezi ya miguu ndani ya hifadhi sanjari na kubarizi ufukweni katika bahari ya Hindi.
    ○ Michezo mbalimbali ya ufukweni katika Bahari ya Hindi.
    ○ Shughuli za safari za boti baharini na kutembelea fungu la mchanga Mafui.
    ○ Ushuhudiaji wakati halisi Kasa wa kijani wanapoanguliwa.
    ○ Mapumziko katika fukwe safi za Bahari ya Hindi.

Hifadhi ya Saadani imerekodi kwa kuwa na takribani aina mbalimbali za ndege 200. Wanyapori hifadhini ni pamoja na Tembo (ndovu), Viboko, Twiga, Nyati (mbogo), nguruwe mwitu, Funo wa rangi nyekundu, Kongoni aina ya Lichtensteins, Pundamilia, ngiri na wanyamapori jamii ya nyani (primates).

Hifadhi ya Taifa Saadani inaangukia katika eneo la uoto wa asili wa kanda ya Mashariki wa maeneo ya Pwani na Zanzibari (Zanzibar – inhambane region) wenye kuhusisha uoto wa asili wa misitu ya Pwani, Mapori na vichaka. Misitu asilia ni Pugu, Zaraninge na Ngezi.

Kuanzia kipindi cha msimu wa mwezi wa Januari na Februari. Vile vile pia mwezi Juni na Agosti. Saadani inafikika kwa urahisi kwa kutumia; 35 - · Usafiri wa barabara (kutokea Dar es Salaam na kuanzia Njia panda Chalinze – Mandera – Miono – Saadani) – kuingilia lango la Mwave ni takribani kilometa 95. Vilevile kuanzia mkoani Arusha – Kilimanjaro – Segera – Tanga, Pangani – Saadani. Na pia kuanzia Dar es – Salaam – Bagamoyo – Saadani kupitia Makurunge – kuingilia lango la Gama ni takribani kilometa 116. Kutokea mkoani Tanga – Pangani – Mkwaja – kuingilia lango la Madete ni takribani kilometa 97. · Usafiri wa Anga (kunapatikana ndege ndogo za kukodi za makampuni ya usafirishaji kutoka Dar es Salaam, Tanga, Zanzibari pamoja na Arusha hadi kwenye viwanja vya ndege Mkwaja na Saadani. · Usafiri wa treni au gari moshi (reli ya uhuru kutokea Dar es Salaam hadi Arusha hupitia hifadhini Saadani na kituo kimoja cha kushushia abiria cha Wami. · Usafiri wa Majini (unaweza kufika hifadhini Saadani kwa kutumia mtumbwi au boti za kukodi kutokea miji ya Dar es Salaam, Tanga, Bagamoyo, Pangani pamoja na Zanzibari.

Swali la kujiuliza hapa kwa watalii wa kitanzania. Je mtabeba vyakula vyenu wenyewe vya kujipikia au mtapata huduma hiyo katika sehemu nyinginezo ambazo zinajulikana? Haya ni mambo ya kimsingi katika kuyaangalia na kuyazingatia kwa umakini mkubwa sana.

Je mtabeba vifaa vyenu wenyewe vya kupiga kambi kama vile mahema katika safari utalii yenu ya matembezi hifadhini? Au mtalala katika nyumba za wageni ndani ya hifadhi au nje ya hifadhi? Haya ni mambo ya kimsingi ya kujiuliza watanzania watalii wa ndani. Pamoja na hayo yote ndani ya Hifadhi ya Saadani kunapatikana nyumba ya kupumzika wageni (Tourist Cottages (Bandas) na Rest House sanjari na mabanda yanayomilikiwa na kusimamiwa na Hifadhi. Vilevile pia panapatikana maeneo ya kupiga mahema yenye kuwa na huduma ya jiko, vyoo na bafu. Kwa mfano, mojawapo ya maeneo haya ya kupiga mahema yenye kuwa na huduma ya jiko, vyoo na bafu ndani ya hifadhi ni (Kinyonga & Beach). Maeneo maalum ya kupiga mahema ambayo yapo katika uhalisia wake ni (Kiwandi & Tengwe). Saadani Safari Lodge (www.saadanilodge.com) ni kambi pekee ya mwekezaji ambayo ipo ndani ya Hifadhi. Nje ya Hifadhi kunapatikana vilevile kambi mbalimbali za kitalii pamoja na nyumba za kulala wageni katika vijiji vya Mkwaja na Saadani. Kwa mfano, Tent with a view (www.tentwithaview.com), Barry’s Beach Resort (www.barrysbeachresort.com),Tanganyika Coastal Campsite and Lodge (www.kenzanluxurycamp.com).

Ni baada ya zoezi zima kukamilika linalohusiana na maandalizi ya usafiri, huduma za chakula, malazi au kulala na mahitaji mengineyo kukamilika. Tozo huhusisha maeneo yafuatayo kama vile; ·

1. Kuingia Ndani ya Hifadhi; ·

2. Kupiga Mahema kama vile maeneo ya kambi ya jumla (public campsite).

· 3. Kupiga Mahema kama vile maeneo ya kambi maalumu (special campsite).

· 4. Nyumba za kupumzika wageni.

 5. Mabanda ya wageni.

6. Utalii katika eneo la Funguni. ·

7. Utalii wa nyakati za usiku (Night Game Drive). 

8. Gharama za Waongozaji Wageni Watalii (Safari Guides)

9. Chakula/ Maakuli (Bush lunch/ dinner).

10. Safari utalii wa Boti. · 11. Kukodisha Boti. 

12. Viingilio vya magari yaliyofungwa uzani wa gari. Magari ya wazi hutakiwa kulipa asilimia 50 zaidi ya tozo za kawaida. 

13. Viingilio vya Ndege. 

14. Tozo za kupiga picha kibiashara bila kujali uraia. 

15. Tozo za ajali ndani ya Hifadhi. Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba endapo utafanya kosa lolote ndani ya Hifadhi kama kutembea na gari nje ya barabara maalumu kwa ajili ya utalii wa utumiaji gari, au kupiga honi au kupigia kelele wanyamapori utatozwa faini. Vilevile endapo utasababisha ajali ndani ya Hifadhi bila kujali nani aliyesababisha au kukosea pia kuna faini yake. Kitu cha msingi na chenye kupewa kipaumbele ni kukumbuka ya kwamba malipo yote hufanyika kwa kutumia kadi za kieletroniki za kibenki kama vile TANAPA pay Card au VISA/MASTER Credit & Debit Cards, MPesa, TigoPesa, Airtel Money. Vibali vya kuingia bila malipo ni kwa watu wenye kuwa na ruhusa maalum. Wageni wakazi (Expatriates) wanaruhusiwa kulipa kwa kutumia pesa ya Tanzania. Fedha zikishalipwa hazirudishwi. Tozo zinaweza kubadilika wakati wowote ule. 

Chaguo la Kampuni ya utalii itakayowahudumieni ninyi katika safari yenu ya matembezi hifadhini, je inatambulika na imesajiliwa? Je wana uzoefu wowote ule na huduma za utalii hifadhini? Au ni utaratibu upi mtakaoutumia ili safari utalii yenu ya matembezi hifadhini isije ikagonga mwamba. Hata hivyo raia wa Tanzania na usafiri wake binafsi anaruhusiwa kufanya utalii wa ndani na sio lazima kupitia kampuni za utalii zilizosajiliwa na kutambulika na mamlaka husika na hii zaidi ni kwa wageni watalii wan nchi za nje.

Mambo ya kufanya na kuzingatia (kanuni na taratibu ndani ya hifadhi);

Wageni watalii wan nje ya nchi ya Tanzania sambamba na watalii wa kitanzania mnakumbushwa ya kwamba ni marufuku na pia ni kosa kisheria; Þ Kusumbua na kubughuzi wanyamapori ndani ya Hifadhi. Þ Kupiga honi na kelele yeyote ile ndani ya Hifadhi. Þ Kusababisha usumbufu na bughuza kwa wageni watalii wengineo ndani ya Hifadhi. Þ Kung’oa, kuchuma, kukata au kuharibu mmea au sehemu yake. Þ Kutupa takataka hovyo, vishungi vya sigara au njiti za kiberiti holela. Þ Kusababisha miito ya moto hifadhini. Þ Kuendesha chombo cha moto kama vile gari katika mwendo kasi mkubwa takribani kilometa 50 kwa saa. Þ Kuendesha chombo chako cha moto nje ya utaratibu malumu wa barabara ndani ya hifadhi maalumu kwa ajili ya safari utalli wa utazamaji wanyamapori (off road drive). Þ Kutoka au kushuka nje ya chombo chako cha moto kama vile gari isipokuwa kuwa tu katika maeneo ambayo yameruhusiwa na mamlaka ya hifadhi husika. Þ Kuingia na silaha na mnyama wa nyumbani kama vile mbuzi. Þ Ni marufuku na vilevile pia hairuhusiwi kulisha wanyamapori ndani ya Hifadhi. · Mengineyo ya ziada ni kwa watanzania watalii wa ndani katika safari utalii wanazoziandaa kuhakikisha angalau wanapata kwa pamoja mazoezi na mafunzo ya kielimu ya huduma ya kwanza katika kukabiliana na changamoto zinazowezajitokeza pasipokutarajia kama vile kupata na kufahamu namna na jinsi ya kukabiliana na dharura ambazo zinazoweza kujitokeza. Au namna gani jinsi vifaa vya huduma ya kwanza vinavyotumika panapotokea dharara kama vile ajali au mtu kuumwa na nyoka kama mfano.

       Kanuni na taratibu zote hifadhini ni kama vile;
1. Ni marufuku kabisa kusumbua au kunyanyasa wanyamapori ndani ya Hifadhi
kwasababu nao pia wana haki ya njia.
2. Ni marufuku kabisa kuleta au kusababisha usumbufu wa aina yeyote ile kwa wageni watalii ndani ya Hifadhi.
3. Ni marufuku kabisa kuchuma au kung’oa mmea wa aina yeyote ile ndani ya Hifadhi.
4. Ni marufuku kabisa kutupa takataka ndani ya Hifadhi.
5. Usizidishe mwendokasi zaidi ya kilometa 50 kwa saa.
6. Ni marufuku kabisa kuwapatia na kuwalisha chakula wanyamapori pamoja na ndegendani ya Hifadhi.

7. Usiteremke nje ya chombo chako cha usafiri isipokuwa tu katika maeneo yaliyoruhusiwa na uongozi wa Hifadhi katika maeneo kama vile kambi za jumuiya (public campsites) pamoja na maeneo ya mapumziko ya muda mfupi (picnic sites).
8. Usiendeshe nje ya barabara.
9. Ni marufuku kabisa kuingia na silaha ndani ya Hifadhi. Unapokuwa una silaha unawajibika kuwasilisha nyaraka halali za umiliki na silaha kwa askari wa wanyamapori katika lango la kuingilia.
10. Usipige kelele wala honi ya gari Hifadhini.

Vifaa muhimu vya kuchukua katika safari utalii hifadhini

Vifaa vyote muhimu katika safari ya matembezi hifadhin kwa mujibu wa aina ya utalli husika. Kwa mfano mahitaji ya milimani ni tofauti na safari za mbugani.

Huduma za mahitaji mengineyo

Mambo ya ziada ya mahitaji yanayojitokeza na upatikanaji wake katika sehemu husika
watanzania wazalendo watalii wa ndani walipo.

Maelezo ya huduma za habari utalii wa ndani.

MAWASILIANO MENGINEYO MAKAO MAKUU (TANAPA)

+255 272508216

info@domestictourismsafaris.c  info@domestictourismsafaris.co.tz