TALII NA TEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA ARUSHA
Arusha(wilayani Arumeru) katika kanda ya Kaskazini Mwa Jamhuri ya muungano wa Tanzania
Chanzo Cha Chimbuko Halisia Kimaelezo Na Ubunifu (Mwalimu Edgardo Kabulwa Welelo)
Ukweli Wa Mambo Kuhusiana Na Hifadhi Ya Taifa Ya Arusha (Wilayani Arumeru); Hifadhi ya Taifa ya Arusha (Wilayani Arumeru) pamoja na Mkoa wa Arusha kwa
ujumla wake umepata majina yake kiasilia kutoka katika kabila la Waarusha (Wamaasai wakiwaita kama Larusa). Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba kabila la Wamaasai pamoja na Waarusha wanasikilizana sana katika mawasiliano ya uongeaji wao na pia kuwa na mahusiano ya kindugu. Makabila mengineyo asilia yapatikanayo ya Mkoa wa Arusha ni pamoja na Wameru, Wamburu (Wairakwi), Wahadzabe (Hadza), Wasonjo, Wandorobo, Wabarabeigi, Wambugwe, na makabila mengineyo mengi madogo madogo. Kihistoria, makabila ya Wamaasai, Wameru, Waarusha, Wachagga na Wamaasai hapo zamani miaka ya nyuma kabla ya kupisha uhifadhi yaliishi maeneo haya yanayozunguka Hifadhi ya Taifa ya Arusha kwa miaka mingi sana kupita ya Mababu na Mabibi zao.Hifadhi ya Taifa ya Arusha ilianzishwa rasmi mnamo mwaka wa 1960, mwaka mmoja kabla ya Uhuru wa Tanganyika (Tanzania bara) na ndio iliyo hifadhi pekee nchini kwetu Tanzania ambayo imepata kutokea kubadilishwa majina yake takribani mara tatu. Mwanzoni kabisa wa uanzishwaji wake kihistoria ilikuwa ikijulikana kwa jina la Hifadhi ya Taifa ya Bonde la Ngurdoto (Ngurdoto Crater National Park) kutokana na bonde la Ngurdoto kama mojawapo ya maeneo ya maumbile asilia ya kijiografia hifadhini yenye kuwa na kivutio cha kipekee chenye kuvutia na kupendeza. Baadaye tena jina hili la Ngurdoto likabadilishwa na kuitwa Hifadhi ya Taifa ya Crater ya Mlima Meru (Meru Crater National Park) na hatimaye mnamo mwaka wa 1967 jina la Hifadhi ya Taifa ya Arusha likatumika rasmi mpaka hadi leo hii. Ni mojawapo ya Hifadhi za Taifa kongwe nchini kwet Tanzania. Hivyo basi, ndugu Mtanzania na raia wa Mama Tanzania hamasika na pata nafasi ya kuitembelea hifadhi hii unapokuwepo mkoani Arusha katika harakati zako binafsi za kimaisha.
Ushauri kwa watalii Raia wa Tanzania katika kujiandaa na kujipanga kimaandalizi na kikamilifu kwa safari utalii
Mambo ya kuzingatiwa na kupewa kipaumbele cha hali ya juu kabisa ni maandalizi ya usafiri kama vile gharama za usafiri hifadhini kwenda na kurudi iwe usafiri 18 – binafsi au wa kukodi, huduma za malazi au kulala, chakula pamoja na mahitaji mengineyo yatakayojitokeza. Haya yote yanahitaji fedha na namna ambavyo hizo fedha jinsi zitakavyotumika. Fedha hizo zinahitaji kutengenezewa bajeti ya matembezi hifadhini.
Hifadhi ya Taifa ya Arusha ilianzishwa rasmi mnamo mwaka wa 1960.
Mpaka hivi sasa ukubwa wa eneo la Hifadhi ya Taifa ya Arusha ni takribani kilometa za mraba 552. Hii ni baada ya eneo la hifadhi hii kuongezwa ukubwa wa eneo la msitu wa asili wa akiba wa Mlima Meru kama mojawapo ya sehemu ya uhifadhi kimikakati tangu mnamo mwaka wa 2004. Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba hifadhi ya Taifa ya Arusha ilipoanzishwa mnamo mwaka wa 1960 ilikuwa na ukubwa wa eneo la kilometa za mraba 137 (ambayo ni sawa na maili za mraba 53).
Hifadhi ya Taifa ya Arusha inafikika kirahisi kabisa kwa njia ya usafiri wa barabara umbali wa takribani kilomita 35 mpaka 40 katika upande wa Mashariki mwa Mji wa Arusha. Vilevile ni sawa na umbali wa takribani kilomita 130 kutoka katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro katika Mkoa wa Kilimanjaro na vilevile pia ni sawa na mwendo wa dakika 50 kutoka Arusha Mjini na saa 1 mpaka 2 kutoka Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro. Vilevile ni sawa na takribani kilomita 60 kutoka katika kiwanja cha kimataifa cha ndege Kilimanjaro.
Mlima Meru ambao ndio mlima wa pili kwa urefu nchini kwetu Tanzania baada ya Mlima Kilimanjaro upatikanao mkoani Kilimanjaro, ambapo mlima Meru wenyewe una urefu wa mita takribani 4566, au sawa na futi 14,990. Maziwa ya maji yenye kuwa na magadi ya Momella (Alkaline Momella Lakes).Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Arusha kunapatikana takribani maziwa 7, ambayo ni pamoja na ziwa dogo la Momella (Small momella lake), ziwa kubwa la Momella (Big momella lake),ziwa Kusare,ziwa Rishateni,ziwa Tulusia,ziwa Lekandiro,pamoja na ziwa El Kekhotoito. Ziwa pekee hifadhini Arusha linalotambulika kuwa na maji baridi (Fresh water) badala ya kuwa na magadi ni ziwa Longil. Maumbile mengineyo ya asili kijigrafia hifadhini Arusha ni kama vile mabonde katika vilele vya mlima Meru, Bonde la Ngurdoto (Ngurdoto Crater), misitu, pamoja na maporomoko ya maji kama vile maporomoko ya maji ya Tululusia na Maio.
Inaanzia mita 1525 katika maziwa ya Momella mpaka mita 4566 katika kilele cha
Mlima Meru kutoka katika usawa wa bahari.
Ni pamoja na Bonde la Ngurdoto (Ngurdoto Crater), Crater ya Mlima Meru na vilele vyake (Meru Crater & Cone), maziwa ya maji yenye kuwa na magadi ya Momella 19 - (Alkaline/Saline Momella Lakes), pamoja na Mlima Meru wenyewe (Mount Meru) na mbega wenye kuvutia na kupendeza wa rangi ya weusi na weupe (Black and White Colobus Monkeys), Twiga (Maasai/Kilimanjaro Giraffes) na bila kusahau maporomoko ya maji ya Tululusia na Maio. Ukiachana na vivutio vikuu, pia Hifadhi ya Taifa ya Arusha ina vivutio vinginevyo vidogo vidogo kama vile Serengeti Ndogo (Mini Serengeti/Little Serengeti), Ujambo wa Mbogo (Buffaloe’s Glade), Mti wa Mkuyu wenye kuwa na shimo kubwa katikati yake (Fig Tree Arch), Makumbusho ya Ngurdoto (Ngurdoto Museum), bila kusahau Msitu wa Asili wa Ngurdoto (Ngurdoto Nature Forest). Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba Hifadhi ya Taifa ya Arusha ni paradiso kwa wageni watalii wapendao viumbe hai ndege (Bird Enthusiasts), ambapo Hifadhi hii ya Taifa ya Arusha ina jumla ya zaidi ya spishi 400 kuweza kurekodiwa na kuripotiwa kiutafiti. Miongoni mwa ndege wapatikanao Hifadhini Arusha ni pamoja na ndege wa makazi ya misitu (Forest Dwellers), ndege wawindaji na walaji wa nyama (Raptors/Birds of Prey), ndege wa makazi ya maji (Water Birds) na ndege wahamaji (Migratory Birds) watokao hususani uzio wa kaskazini (Northern Hemisphere) ikimaanisha mstari wa Ikweta (Equator) kaskazini. Baadhi ya viumbe hai ndege maarufu ni pamoja na ndege Heroe (Flamingos), Tai Mla Samaki (African Fish Eagle), Kinega – Kifua Marungi (Cinnamon – Chested Bee – Eaters), Bata – Bukuni (Egyptian Geese), Mwari Mweupe (Great White Pelican), na kadhalika.
Ni kama vile Mbega wenye kuwa na rangi nyeusi na nyeupe (Black and White Colobus Monkeys),Nyati/Mbogo (Savanna/African Buffalo), Funo (Harvey Red Duikers), Pongo (Bushbucks), Digidigi/Saruya (Kirk’s DikDik), Ngiri (Common Warthog), Paa (Suni), Tembo/Ndovu(Bush/Savanna/AfricanElephant),Kuro(CommonWaterbuck), Tohe(BohorReedbuck),Twiga(Kilimanjaro/MaasaiGiraffes),Pundamilia(Common/Burch ell’s/Plains Zebra),Fisi Madoadoa (Spotted Hyenas) na wengineo walio wengi. Kunapatikana zaidi ya spishi 450 za viumbe hai ndege hifadhini Arusha. Mfano mzuri ni pamoja na ndege heroe (Flamingos) katika ziwa kubwa la Momella (Big Momella Lake) na ziwa Rishateni, ndege Marabu (Marabou Stork), ndege Fundi Chuma (Hammerkop), ndege Korongo Majoka (Black – Headed Heron), ndege Taji/Korongo – Taji (Grey Crowned Crane) na wengineo walio wengi. Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba hakuna wanyamapori simba kabisa katika hifadhi hii. Wanyamapori wengineo ambao hawapatikani kabisa hifadhini Arusha ni kama vile swala tomi, taya, swala pala na kongoni. Sababu ya kimsingi ya kutopatikana wanyamapori hawa ni makazi ya kimazingira hifadhini Arusha yenyewe jinsi yalivyo ambayo si ya makazi ambayo wanyamapori hawa huyahitaji, pamoja na tabia zao jinsi zilivyo. Kwa sababu ya hifadhi hii ya Taifa Arusha kutawaliwa kwa kiasi fulani kuwa na makazi ya uoto wa asili wa misitu ya hapa na pale, wanyamapori kama vile jamii ya nyani (primates),kima,tumbili na mbega wenye kuwa na rangi nyeupe na nyeusi hupatikana 20 - na kuonekana pasipo shida yeyote ile. Vilevile wanyamapori chui hupatikana na kuonekana.
Hifadhi ya Taifa ya Arusha inaangukia katika uoto wa asili wa misitu wa kitropiki wa milimani (Montane Forest). Vilevile hifadhi hii ya Taifa ya Arusha pia ina maeneo ya mazingira ya makazi yenye kutofautiana na pia yenye kuwa na hali ya hewa tofauti kutoka katika usawa wa bahari na vilevile jiografia yake ya maeneo kutofautiana. Kwa mfano hai, hali ya hewa kutoka katika usawa wa bahari (mita 1700 mpaka 1800) uoto wa asili wake katika Mlima Meru umetawaliwa na msitu wa kijani kibichi uliotawaliwa na mimea asilia kama vile mimea miti Marumbayi (Croton), Loliondo (Olea), Mfumu au Mkuyu (Ficus) na mingineyo iliyo mingi ya aina mbalimbali. Katika ukingo wa bonde la Ngurdoto (Ngurdoto Crater) uoto wa asili wa mlimani uliotawala ni pamoja na Cussipourea malossana. Hali ya hewa kutoka katika usawa wa bahari ya hali ya juu mlimani inayoanzia takribani (mita 1800 mpaka 2100) uoto wa asili wa mimea miti ni pamoja na Daragwai (Juniperus) na Podo (Podocarpus). Wakati ambapo hali ya hewa kutoka katika usawa wa bahari ya hali ya kati mlimani unanzia (mita 1440 mpaka 1700) uoto wa asili ni kama vile mimea miti Msamvu (Diospyros) na Loliondo (Olea).Uoto mwingineo upatikanao hifadhini Arusha ni pamoja na uoto wa asili wa mimea nyasi katika maeneo ya vivutio kama vile Ujambo wa Mbogo au Nyati (Buffaloe’s Glade), na Serengeti ndogo ( Little Serengeti/ Mini Serengeti).
Ni katika wakati wowote ule karibia mwaka mzima. Wakati mzuri na ulio bora wa
kutembelea na kutalii Hifadhini Arusha ni mwezi wa Oktoba mpaka Februari
Kama kuna ulazima wa kubeba vyakula vyenu wenyewe mnaweza kufanya hivyo. Kama hakuna ulazima basi utaratibu mwingineo unaweza kuratibiwa.
Kama safari utalii yenu ya matembezi hifadhini ni zaidi ya siku moja kama vile kupanda Mlima Meru ni lazima kubeba vyakula vyenu wenyewe. Kama mtalala ndani ya hifadhi kwa ajili ya kupiga kambi ni muhimu kubeba mahema yenu wenyewe ingawa utalii ndani ya hifadhi hii ya Arusha huweza kukamilika katika siku moja tu (Day –trip).Nyumba za kulala wageni watalii ni za kutosheleza ndani ya hifadhi yenyewe na vile vile nje ya hifadhi hususani katika mji mdogo wa USA – RIVER na maeneo mengineyo yaliyo karibu jirani na hifadhi yenyewe.
Ni pamoja na mambo muhimu na ya kimsingi kama vile maandalizi ya usafiri, huduma za chakula, malazi au kulala na mengineyo yanayoweza kujitokeza. Hii ndio sehemu ya dira ya safari utalii yenu ya matembezi hifadhini.
Utaratibu maalumu uandaliwe wa kuelimishana na kupeana mafunzo yanayohusiana na huduma ya kwanza miongoni mwa wananchi watalii wa ndani. Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba dharura hutokea katika safari utalii za matembezi hifadhini.
Mambo muhimu ya kufanya na kuzingatia
(kanuni na taratibu ndani ya hifadhi)
Hii ni sehemu muhimu sana na iliyo makini ya kujiuliza maswali ambayo ni ya msingi ili kupata ufumbuzi wa jibu la safari utalii na matembezi hifadhini. Je, mtalala ndani ya hifadhi au hapana? Kama mtalala ndani ya hifadhi basi ni lazima mbebe mahema yenu wenyewe kwa ajili ya kupiga kambi. Ufuatiliaji na utekelezaji wa kanuni na taratibu hifadhini. Kwa mfano usitupe takataka
hovyo, sigara na vitu vinginevyo. Vipeperushi vya hifadhini vinaelezea haya yote.
Vifaa muhimu vya kuchukua katika safari utalii hifadhini
Kamera, viona mbali (Binoculars), video kamera, vitabu mbalimbali vya mafunzo ya
kujielimisha kielimu ya viumbe hai mimea, wanyamapori pamoja na mazingira ya makazi yao
(Viongozi vya vitabu/ Guide books)
Huduma za mahitaji mengineyo
Haya ni mambo au masuala ya ziada ya mahitaji yanayojitokeza na upatikanaji wake katika sehemu husika watalii wa ndani walipo
Maelezo ya huduma za habari utalii wa ndani.
Kampuni ya Uelimishaji,Uratibu,Uandaaji,Uhamasishaji, na Uwezeshaji Utalii wa Ndani
Follow us:
MAWASILIANO MENGINEYO MAKAO MAKUU (TANAPA)
- Juma tatu - Ijumaa
- 8:00 Asubuhi - 4:30 Jioni
+255 272508216
info@domestictourismsafaris.c info@domestictourismsafaris.co.tz



