TEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA MIKUMI (MIKUMI NATIONAL PARK

Mkoani Morogoro katika ukanda wa Mashariki (Eastern zone) mwa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania (The United Republic of Tanzania);

Chanzo Cha Chimbuko Halisia Kimaelezo Na Ubunifu (Mwalimu Edgardo Kabulwa Welelo)

Ukweli Wa Mambo Kuhusiana Na ‘’Hifadhi ya Taifa ya Mikumi’’ (Mikumi National Park) katika ‘’Ukanda wa Mashariki’’ (Eastern Zone) mwa Jamhuri ya Muungano Ya Tanzania (The United Republic of Tanzania); ‘’Hifadhi ya Taifa ya Mikumi’’ (Mikumi National Park) inapatikana kijiografia katika ‘’Mkoa wa Morogoro’’. Ni mojawapo kati ya ‘’Hifadhi za Taifa’’ (National Parks) ‘’nchini kwetu Tanzania’’ zinazopatikana kijiografia katika ukanda wa upande wa ‘’Mashariki Mwa Nchi’’ (Eastern Zone).Ni sawa na umbali wa takribani kilomita 295 kutokea katika upande wa ‘’Magharibi mwa Jiji la Dar – es - Salaam’’ kuweza kufika katika ‘’Hifadhi hii ya Taifa ya Mikumi (Mikumi National Park).Vilevile ‘’Hifadhi hii ya Taifa ya Mikumi’’ (Mikumi National Park) inapatikana baina ya ‘’Vijiji vya Doma na Mikumi’’ katika ‘’Barabara Kuu ya Dar es Salaam – Tunduma’’. Ukweli wa mambo ni ya kwamba ‘’Hifadhi ya Taifa ya Mikumi’’ (Mikumi National Park) kimsingi inaangukia katika ukanda wa eneo la ‘’Milima Ya Tao la Mashariki’’ (The Eastern Arch Mountains) ambayo asili na chimbuko lake imeanzia kusini mwa ‘’nchi ya Kenya’’ katika ‘’Milima ya Taita’’ (Taita Hills) kuelekea na kutawanyika kuja katika uelekeo wa upande wa ‘’Kaskazini Mashariki mwa nchi yetu ya Tanzania’’ kupitia ‘’Milima ya Pare Kaskazini na Kusini (North and South Pare Mountains),Usambara Mashariki na Magharibi (Eastern and Western Usambara Mountains), Milima ya Nguu, Nguru,Ukaguru,Uluguru,Rubeho,Malundwe,Mahenge,Livingstone,Udzungwa, mpaka Makambako na nchi jirani ya Malawi. Makao makuu ya ‘’Hifadhi ya Taifa ya Mikumi’’ (Mikumi National Park) yanapatikana kutoka usawa wa bahari mita 549. Ikumbukwe na ifahamike ya kwamba ‘’Hifadhi ya Taifa ya Mikumi’’ (Mikumi National Park) ilianzishwa rasmi mnamo mwaka wa 1964 na ilipata jina lake hilo kutoka katika ‘’Mji wa Mikumi’’ ambapo kiasili na uhalisia wa jina hili ‘’Mikumi’’ limetokana na mimea ya miti ya ‘’jamii ya minazi’’ (Palms) ijulikanayo katika lugha ya ‘’Kiswahili’’ kama ‘’Mchapa’’.Katika jamii ya makabila mengineyo ‘’nchini kwetu Tanzania’’ kama vile ‘’Wasukuma na Wanyamwezi’’ mmea huu wa mti unajulikana kama ‘’Muhama’’

Ushauri kwa Watalii Raia wa Tanzania katika kujiandaa na kujipanga kimaandalizi kwa Safari Utalii

Kabla ya kufanya maamuzi ya kutalii na kutembelea hifadhini ni vema na busara maandalizi ya safari utalii ya kutalii na matembezi hifadhini yakapewa kipaumbele cha kwanza ikizingatiwa ya kwamba gharama za usafiri hupanda na kubadilika mara kwa mara ‘’nchini kwetu Tanzania’’.

‘’Hifadhi ya Taifa ya Mikumi’’ (Mikumi National Park) ilianzishwa rasmi mnamo mwaka wa 1964. Hifadhi hii ya ‘’Taifa ya Mikumi’’ (Mikumi National Park) ilijipatia jina lake hilo kutoka katika ‘’Mji wa Mikumi’’, ambapo kimsingi asili ya jina hili pia limetokana na uoto wa asili wa mimea miti ya ‘’jamii ya minazi’’ (Palms) inayostawi maeneo haya kiasilia

Ukubwa wa eneo la ardhi ya ‘’Hifadhi ya Taifa ya Mikumi’’ (Mikumi National Park) ni takribani kilomita za mraba 3,230.

Hifadhi ya Taifa ya Mikumi’’ (Mikumi National Park) inafikika kwa njia ya usafiri wa barabara umbali wa takribani kilomita 295 kutokea ‘’Jijini Dar – es - Salaam’’ na vile vile ni sawa na umbali wa takribani kilomita 330 kutokea ‘’Hifadhi ya Taifa ya Ruaha’’ (Ruaha National Park). Ni sawa na takribani saa 3 mpaka 4 kutokea ‘’ Jijini Dar – es – Salaam na vilevile ni sawa na saa 5 mpaka 6 kutokea ‘’Hifadhi ya Taifa ya Ruaha’’ (Ruaha National Park).

Ni pamoja na ‘’Ardhi Tambarare’’ zilizofurika maji za ‘’Mto Mkata’’ (Mkata Floodplains), ‘’Maeneo yenye kuwa na Ardhi Oevu’’ (Swamps) na vile vile ‘’Uoto wa Asili wa Mimea Miti ya Miombo (Miombo Woodland/Zambezian Vegetation Region).

Kawaida inaanzia mita 500 mpaka 2,270 kutoka katika usawa wa Bahari. Kimsingi na cha kipekee kabisa ‘’Hifadhini Mikumi’’ ni ya kwamba kiwango cha mvua kinachonyesha hutofautiana baina ya miririta 508 katika ‘’Makao Makuu’’ ya hifadhi, wakati ambapo katika sehemu ya ‘’Chamgore’’, takribani kilomita 24, yenyewe kawaida ni wastani wa miririta 635. Katika vilima vipatikanavyo ndani ya hifadhi yenyewe ni wastani wa miririta 1,067. Mvua za vuli au mvua fupi (Short Rainy Season) kimsingi hunyesha katika ‘’Mwezi Novemba na Mwezi Desemba’’, ambapo ‘’Mvua ndefu za masika’’ (Long Rainy Season) zenyewe huanza kunyesha kuanzia ‘’Mwezi Machi mpaka Mwezi Mei’’. Hivyo basi kwa ufupi mvua zinazonyesha ndani ya hifadhi ya Taifa ya Mikumi hutofautiana kwa mujibu wa kanda mbalimbali hifadhini humo.

Ni pamoja na ‘’Ardhi Tambarare’’ zilizofurika na maji za ‘’Mto Mkata’’ (Mkata Floodplains),Wanyamapori kama vile Tembo/Ndovu(Savanna/African/Bush Elephant),Twiga(Maasai/Kilimanjaro Giraffe),Mbwa Mwitu(African Hunting Dog) na wengineo walio wengi wa aina mbalimbali, viumbe hai ndege wahamao(Migratory birds) na bila kusahau maeneo ya kiutamaduni.

Ni pamoja na wanyamapori jamii ya nyani (primates) kama vile nyani wenye rangi ya manjano (Yellow Baboon), Tumbili/Ngedere(Vervet Monkey/Black – Faced Monkey), Kima (Blue Monkey/Sykes Monkey),Simba(Lion), Pundamilia(Plains/Common/Burchell’s Zebra(Grant’s Zebra), Pofu (Patterson/East African Eland), Mbogo/Nyati(Savanna/African/Cape Buffalo), Tandala wakubwa(Greater Kudus), Pongo(Bushbucks), Kuro(Common Waterbuck), kongoni aina ya ‘’Lichtensteins’’(Lichtenstein Hartebeest) na wengineo walio wengi sana. Ikumbukwe na ifahamike ya kwamba ‘’Hifadhi ya Taifa ya Mikumi’’ (Mikumi National Park) ina takribani spishi za viumbe hai ndege zaidi ya 450 kuweza kurekodiwa na kuripotiwa kisayansi na kitafiti.

Ni pamoja na ‘’Uoto wa Asili wa Mimea ya Miti ya Miombo’’(Miombo Woodland), ‘’Uoto wa Asili wa Mimea katika ‘’ Ardhi Tambarare zilizofurika maji za ‘’Mto Mkata’’(Mkata River Floodplain), na pia sehemu iliyosalia ni ya ‘’Miti ya Miba ya Migunga, Mpingo, Mibuyu na Vichaka’’. Kwa ujumla wake ni vema na busara ikakumbukwa na kufahamika ya kwamba ‘’Hifadhi ya Taifa ya Mikumi’’ (Mikumi National Park) ina takribani aina 6 za uoto wa asili kama ifuatavyo;

1. ‘’Uoto wa Asili wa Misitu ya Kitropiki ya Milimani (Afromontane Forest); Uoto huu unahusisha vipande vya sehemu ya safu za milima yenye kutawaliwa na misitu ya milimani kama vile ‘’Milima ya Malundwe’’ katika sehemu ya katikati ya hifadhi. Milima ya ‘’Malundwe’’ ni mojawapo ya sehemu ya ‘’Milima ya Tao la Mashariki’’ (The Eastern Arch Mountains).

2. ‘’Uoto wa Asili wa Msitu unaostawi kufuata Mkondo wa Mto’’(Riverine/Gallery Forest); Uoto huu wa asili pia unahusisha vichaka vinene vilivyofungamana na misitu kandokando ya mito.

3. ‘’Uoto wa asili wa mimea katika ‘Ardhi Tambarare zilizofurika maji ya ‘’Mto Mkata’’

4. ‘’Uoto wa Asili wa Mapori mchanganyiko na uoto wa nyasi’’ (Wooded Grassland).

5. ‘’Uoto wa Asili wa Mapori yaliyo wazi’’ (Open Woodland) 6. ‘’Uoto wa Asili wa miti ya Mapori iliyofungamana au ‘’Uoto wa asili wa miti ya Miombo (Miombo Woodland) upatikanao kimtawanyiko katika vilele vya milima na kadha wa kadhalika.

Wakati wa kipindi cha msimu wa kiangazi (Dry – Season) kuanzia Mwezi
Septemba mpaka Mwezi Machi.

Katika ‘’Hifadhi hii ya Taifa ya Mikumi’’ (Mikumi National Park) inawezekana kwa watanzania watalii wa ndani kuweza kujibebea vyakula vyao wenyewe vya kujipikia kama safari utalii yao kwa mujibu wa ratiba zao zinaruhusu kulala na kupiga kambi na vilevile huduma hizo za chakula zinapatikana pasipo shida yeyote ndani na nje ya hifadhi.

Ni pamoja na ‘’Hoteli ya Mikumi’’ (Mikumi Wildlife Lodge) ambayo hapo zamani ilikuwa chini ya milki na udhibiti wa ‘’Serikali ya Jamhuri ya Muungano Ya Tanzania’’ kupitia shirika la utalii kwa kipindi hicho cha zamani (Tanzania Tourist Corporation) kabla ya kubinafsishwa. Hoteli au Lodge hii imejengwa katika mwinuko ikitazama bonde kutoka katika usawa wa bahari wa mita 762 na pia ina jumla ya vitanda takribani 150 vya kulaza wageni pamoja na bwawa la kuogelea wageni (swimming pool). Pia panapatikana huduma ya kituo cha mafuta (Petrol Station) kwa huduma zaidi. Karibu na lango la kuingilia ‘’Hifadhi ya Taifa ya Mikumi’’(Mikumi National Park) pia panapatikana ‘’Kambi ya kudumu ya kupiga mahema’’ inayofahamika kama ‘’Mikumi Wildlife Tented Camp’’ ambayo hutoa fursa ya utazamaji wa ardhi tambarare pamoja na bonde kwa chini sambamba na wanyamapori kwa watalii wa ndani na nje wanaopiga kambi sehemu hii. Kambi hii ya mahema ya ‘’Mikumi Wildlife Tented Camp’’ ina takribani vitanda 40 vya kulaza wageni ingawa kuna mipango ya baadaye ya kuongeza vitanda vya kulaza wageni watalii. Pia panapatikana huduma binafsi ya kampuni ya utalii ya kupiga mahema chini ya usimamizi na uongozi wa kampuni ya utalii ya ‘’FOX’’ ambao wanamiliki kambi ya ‘’Fox Safari Tented Camp’’ yenye kuwa na vitanda takribani 24 vya kulaza wageni. Huduma nyinginezo binafsi ni pamoja na ‘’Vuma Hill Tented Camp’’ yenye kuwa na vitanda vya kulaza wageni takribani 32, na bila kusahau ‘’Live Safaris Tented Camp’’ yenye kuwa na vitanda vya kulaza wageni watalii takribani 40. Huduma ya ‘’HOSTELI’’ pia ipo inapatikana chini ya usimamizi na uangalizi wa uongozi wa ‘’Hifadhi ya Taifa ya Mikumi’’ (Mikumi National Park). Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba huduma hii ya ‘’HOSTEL’’ ni maalumu kwa ajili ya wanafunzi na wanachuo na ina jumla ya vitanda vya kulaza wageni takribani 60, ingawa kuna uwezekano wa mipango ya baadaye kuongeza idadi ya vitanda vya kulaza wageni ili iweze kufikia takribani 120 kwa ajili ya wanafunzi na wanachuo. Huduma za ‘’Kambi za Jumuiya’’ (Public Campsites) na pia ‘’Kambi Maalumu’’ (Special Campsites) pia zinapatikana karibia maeneo yote ndani ya ‘’Hifadhi ya Taifa ya Mikumi’’ (Mikumi National Park). Mojawapo ya mifano hai ya ‘’Kambi za Jumuiya’’ (Public Campsites) ni pamoja na; 1. Public Campsite No 1 (Eneo Kikoboga) 2. Public Campsite No 2 (Eneo Kisungura) 3. Public Campsite No 3 (Eneo Vuma Hill) 4. Public Campsite No 4 (Eneo Vuma Hill) 5. Special Campsite (Eneo Chogawale) 6. Special Campsite (Eneo Kitangawizi) 7. Special Campsite (Eneo Korongo la Maziku) 8. Premium Campsite (Eneo Vuma Hill) 9. Premium Campsite (Eneo Ngolwe) 10. Satellite Campsite (Eneo Chamgore) 11. Satellite Campsite (Eneo Mayawili). Zaidi ya hizi huduma pia panapatikana maeneo kadhaa ya mapumziko ya muda mfupi (Picnic Sites) ndani ya hifadhi wakati ambapo shughuli mbalimbali zinapoendelea ndani ya hifadhi. Hata hivyo, nje ya hifadhi ya ‘Taifa ya Mikumi’’ (Mikumi National Park) pia huduma za malazi na chakula pia hupatikana katika ‘’Mji wa Mikumi’’ (Mikumi Township). Mojawapo ya hayo maeneo ni pamoja na;

1. ‘’Impala Guest House’’.

2. ‘’Kilimanjaro Guest House’’.

3. ‘’White House Guest House’’.

4. ‘’Green Park Hotel’’.

5. ‘’Sanene Hotel’’.

6. ‘’TanSwiss Hotel’’.

7. ‘’HalfWay Guest House’’.

8. ‘’Genesis Motel’’.

9. ‘’Melela Nzuri Campsite, na kadha wa kadhalika.

10. Premium Campsite (Eneo Ngolwe) 10. Satellite Campsite (Eneo Chamgore)

11. Satellite Campsite (Eneo Mayawili). Zaidi ya hizi huduma pia panapatikana maeneo kadhaa ya mapumziko ya muda mfupi (Picnic Sites) ndani ya hifadhi wakati ambapo shughuli mbalimbali zinapoendelea ndani ya hifadhi. Hata hivyo, nje ya hifadhi ya ‘Taifa ya Mikumi’’ (Mikumi National Park) pia huduma za malazi na chakula pia hupatikana katika ‘’Mji wa Mikumi’’ (Mikumi Township). Mojawapo ya hayo maeneo ni pamoja na; 1. ‘’Impala Guest House’’. 2. ‘’Kilimanjaro Guest House’’. 3. ‘’White House Guest House’’. 4. ‘’Green Park Hotel’’. 5. ‘’Sanene Hotel’’. 6. ‘’TanSwiss Hotel’’. 7. ‘’HalfWay Guest House’’. 8. ‘’Genesis Motel’’. 9. ‘’Melela Nzuri Campsite, na kadha wa kadhalika.

Gharama za usafiri wote pamoja na tozo ni matokeo ya ukamilishaji wa mambo muhimu ya safari utalii kama vile maandalizi ya usafiri, huduma za chakula, malazi, viingilio ndani ya hifadhi na dharura za hapa na pale zitakazojitokeza.

Je mpangilio wa ratiba wa safari utalii yenu ya kutalii na matembezi hifadhini ni ya siku moja au zaidi ya siku moja? Haya ndiyo mambo muhimu kabisa yatakayotoa picha halisi na dira ni namna gani fedha itakavyotumika kuanzia mwanzo wa safari utalii yenu mpaka mwisho wa safari utalii yenyewe.

Mambo muhimu ya kufanya na kuzingatia
(kanuni na taratibu ndani ya hifadhi)

Kila safari utalii yeyote ile ya kutalii na matembezi hifadhini ni lazima izingatie ya kwamba usalama wa ‘’Afya za Watu’’ ni muhimu pamoja na kinga zake. Inashauriwa na kuhamasishwa kubeba boksi la huduma ya kwanza. Kanuni na taratibu ndani ya hifadhi ni pamoja na uzingatiaji wa zile sheria mama za uhifadhi wa mazingira ambazo kimsingi zinafahamika ili kuepuka adhabu ambazo hazistahili kuzipata kwa wageni watalii wa ndani.

Vifaa muhimu vya kuchukua katika safari utalii hifadhini

Ni pamoja na ‘’Vitabu vya Viongozi’’ hifadhini (Guide books) kama vile vitabu vyenye kuwa na maelezo elekezi vya ‘’Hifadhi za Taifa’’(National Parks Field Guide Books), vitabu vya mimea, ndege na viongozi vya vitabu vinginevyo. Viona mbali (Binoculars) na Kamera, ingawa leo hii katika ulimwengu wa utandawazi ‘’Simu Janja’’ (Smart Phones) pia ni mojawapo ya vifaa muhimu sana katika kujiwekea kumbukumbu.

Huduma za mahitaji mengineyo

Mambo ya ziada ya mahitaji yatakayojitokeza na upatikanaji wake katika sehemu husika mlipo katika safari yenu ya matembezi hifadhini.

Maelezo ya huduma za habari utalii wa ndani.

MAWASILIANO MENGINEYO MAKAO MAKUU (TANAPA)

+255 272508216

info@domestictourismsafaris.c  info@domestictourismsafaris.co.tz