TALII NA TEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA MILIMA YA MAHALE

Mkoani kigoma magharibi mwa jamhuri ya muungano wa Tanzania

Chanzo Cha Chimbuko Halisia Kimaelezo Na Ubunifu (Mwalimu Edgardo Kabulwa Welelo

Ukweli Wa Mambo Kuhusiana Na Hifadhi Ya Taifa Ya Milima Ya Mahale Mkoani Kigoma Magharibi Mwa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania; Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale inapatikana kijiografia mkoani kigoma katika upande wa magharibi mwa Jamhuri ya Muungano yaTanzania. Uwapo mkoani Kigoma Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale inapatikana katika upande wa Mashariki wa mwambao wa Ziwa Tanganyika takribani umbali wa kilometa 150 Kusini mwa Mji wa Kigoma kupitia usafiri wa majini katika Ziwa Tanganyika. Hifadhi hii ilianzishwa rasmi mnamo mwaka wa 1985.

Ushauri kwa watalii raia wa Tanzania katika kujiandaa na kujipanga kimaandalizi na kikamilifu kwa safari utalii

Fedha zinahitajika katika maandalizi ya usafiri ili kuwezesha na kufanikisha matembezi yenu hifadhini. Je bajeti ya fedha zilizotengwa zinawawezesha kutembelea na kutalii hifadhini au hapana?

Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale ipatikanayo mkoani Kigoma ilitangazwa na kuanzishwa rasmi kupitia katika gazeti la serikali Namba 262 la tarehe 14 mwezi Juni mnamo mwaka wa 1985. Kihistoria Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale ni makazi asilia ya jamii ya watu wa makabila ya Watongwe na Waholoholo. Tangu mnamo mwaka wa 1961, watafiti wa Kijapani wametafiti maeneo mbalimbali katika mwambao wa Ziwa Tanganyika, kusini mwa mji wa Kigoma. Mnamo mwaka wa 1965, walianzisha kambi ya kudumu ya utafiti katika eneo la Kansyana na kuanza kuwazoesha sokwe kwa shughuli za utafiti lakini pia waweze kuangaliwa na watu bila ya uwoga wowote ule. Toka nyakati hizo utafiti wao umeendelea mpaka leo hii kwa kipindi cha zaidi ya miaka 50 bila ya kusimama.

Ukubwa wa eneo la Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale mkoani Kigoma ina jumla ya ukubwa wa kilometa za mraba 1613, ambapo ni sawa na maili za mraba 623. Kilometa za mraba 1517 ni sehemu ya eneo la nchi kavu katika hizo kilometa za mraba za eneo lote ambazo ni 1613, wakati ambapo kilometa za mraba 96 ni sehemu ya eneo la maji ndani ya Ziwa Tanganyika. Jina la Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale limetokana na safu za Milima yenye kuwa na urefu wa kilometa 50 ambazo zinakatisha ndani ya Hifadhi kutokea katika upande wa kaskazini magharibi kuelekea katika upande wa kusini mashariki. Milima hii ina kilele cha Nkungwe chenye kuwa na mwinuko wa mita takribani 2462 kutoka usawa wa bahari na ambacho ndicho kilele kirefu zaidi kinachopatikana pembezoni mwa Ziwa Tanganyika.

Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale mkoani Kigoma inafikika kwa njia ya kutumia usafiri wa aina mbalimbali kama vile; · Usafiri wa Anga; Shirika la ndege nchini Tanzania (Air Tanzania) hufanya safari zake za anga kila siku isipokuwa tu siku ya Jumanne kutokea jijini Dar es – Salaam hadi Kigoma. Vilevile pia panapatikana mashirika ya ndege ndogo za kukodisha ambazo huruka moja kwa moja zikitokea Kigoma mjini, Mwanza, Arusha au Dar es – Salaam kuja Mahale. Ndege hizi ndogo ni za makampuni ya ndege kama vile Zantas Air, Air Excel pamoja na Tanganyika Flight. Ndege hizi hutua katika uwanja wa ndege mdogo wa Kalolwa ambao unapatikana takribani kilometa nne kutokea makao makuu ya Hifadhi. · Usafiri wa Majini; Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale pia inafikika kwa njia ya usafiri wa majini kupitia Ziwa Tanganyika. Meli ya MV Liemba hufanya safari zake angalau mara mbili katika kila mwezi ikitokea Kigoma mjini kuelekea Zambia. Safari hii kawaida hutumia saa 9 mpaka 10 kufika katika kituo cha Lagosa kilichopo katika kijiji cha Mgambo. Kutoka katika kijiji cha Mgambo/ Lagosa unaweza kukodisha au kupanga usafiri wa boti ya Hifadhi ili kuweza kufika Mahale. Kutoka katika kituo cha Lagosa – Mgambo kunapatikana takribani umbali wa kilometa 30 kaskazini mwa Hifadhi na vilevile inachukua muda wa dakika 30 kufika katika makao makuu ya Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale. · Usafiri wa njia ya Barabara; Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale pia inafikika kwa njia ya usafiri wa barabara. Usafiri wa magari unapatikana ukitokea Kigoma mjini kuelekea upande wa kusini mwa mji wa Kigoma kupitia katika kijiji cha Simba kupitia mto Malagarasi hadi katika kijiji cha Kapalamsenga takribani zaidi ya kilometa 150 wakati wa kipindi cha nyakati za kiangazi au kilometa 122 kupitia katika kijiji cha Sigunga ambapo mtalii atahitajika kukodisha boti ya Hifadhi. Kijiografia Hifadhi hii inapatikana upande wa Mashariki mwa mwambao wa Ziwa Tanganyika takribani kilometa 150 Kusini mwa Mji wa Kigoma. Ni sawa na saa 3 mpaka 4 kwa njia ya usafiri wa boti zinazotumia Injini.

ziwa tanganyika, safu ya milima, bonde la ufa la ukanda wa magharibi, pamoja na misitu.

Hali ya hewa kutoka usawa wa bahari ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale inaanzia mita 2000 mpaka 2462. Majira ya kiangazi huanza katikati ya 84 - nyakati za kipindi cha mwezi Mei hadi kufikia mwezi wa Oktoba ambapo kiwango cha juu cha joto hufikia nyuzi joto 31. Kipindi cha nyakati cha msimu wa mvua huanzia mwezi Oktoba na kumalizikia katikati ya mwezi Mei. Katika vipindi vyote hivi viwili hali ya joto hubadilika mara kwa mara hususani nyakati za kipindi cha usiku.

 

  1. Viumbe hai ndege wa aina mbalimbali.
  2. Fukwe za Ziwa Tanganyika.
  3. Maporomoko ya maji ya Ntale pamoja na Lubugwe.
  4. Makundi makubwa ya Sokwemtu.
  5. Milima na misitu.  

Ziwa Tanganyika jenyewe ni mojawapo ya kivutio kikubwa barani Afrika na duniani kwa ujumla wake katika misingi ya kwamba ndilo ziwa nambari moja kwa kuwa na urefu mrefu zaidi duniani kuliko maziwa yote takribani umbali wa urefu wa kilometa 673 kutokea upande wa kaskazini kuelekea kusini. Vilevile pia Ziwa Tanganyika ni ziwa nambari moja barani Afrika kwa kuwa na kina kirefu zaidi kuliko maziwa yeyote yale barani Afrika na pia ni nambari mbili duniani kwa kuwa na kina kirefu zaidi baada ya ziwa Baikal nchini Urusi (Siberia). Kina cha Ziwa Tanganyika ni takribani mita 1470. Ziwa Tanganyika lina zaidi ya aina mbalimbali za viumbe hai samaki takribani 350 ambao kimsingi hawapatikani sehemu yeyote ile duniani.

  • Matembezi ya safari utalii wa boti ndani ya Ziwa Tanganyika kuelekea katika
    kuwaona mammalia viboko, viumbehai vinavyotambaa kama vile mamba bila kusahau
    viumbe hai samaki.
  •  Matembezi ya safari utalii wa miguu katika utazamaji na utambuzi wa viumbe hai
    ndege.

  • Utalii wa upigaji makasia wa takribani saa tatu.
  • Utalii wa uvuvi katika utumiaji wa ndoano au ndoana.
  • Utalii wa uogeleaji.
  • Matembezi ya safari utalii wa miguu ndani ya msitu wa KASOGE ya muda mrefu na
    pia muda mfupi chini ya usimamizi na uongozaji wa askari wa wanyamapori. Shughuli
    nyinginezo ni pamoja na kupanda kilele cha Mlima Nkungwe kwa takribani saa 7 mpaka
    9. Kilele cha Mlima Nkungwe ni takribani urefu wa mita 2,462 juu ya usawa wa bahari.
  • Safari utalii wa matembezi ya miguu kwenda kujionea makundi makubwa ya
    Sokwemtu katika msitu wa KASOGE.

Wanyamapori jamii ya nyani (primates) kama vile mbega wenye kuwa na rangi nyeupe na nyeusi, nyani wenye rangi ya kijivu na manjano, tumbili pamoja na kima. Wanyamapori wengineo ukiachana na jamii ya nyani ni pamoja na Funo, Isha, Nguchiro, Mkia mweupe, nguchiro mraba, chui, nyati au mbogo, simba na wengineo wengi.

Uoto wa asili wa misitu katika tambarare, uoto wa misitu wa milimani mchanganyiko pamoja na mianzi, na vile vile asilimia 75 ya uoto wa asili ni wa mimea ya miti ya Miombo.

Wakati mzuri na ulio bora wa kutembelea na kutalii Hifadhi hii ya Taifa ya Milima ya Mahale ni wakati wa kipindi cha nyakati za kiangazi kinachoanzia mwezi Mei (Tano) mpaka kufikia katikati ya mwezi Oktoba (Kumi) kwa matembezi ya utalii wa miguu katika msitu. Katika nyakati cha kipindi hiki hupatikana uwezekano mkubwa wa kuwaona sokwe mtu wakiwa katika makundi makubwa. Kitu kinachofurahisha zaidi hasahasa kwa wale watalii ambao wanaweza kupata bahati ya kujionea tabia mbalimbali za sokwe mtu kama vile uwindaji wa wanyamapori wengineo jamii ya nyani sambamba na mammalia wengineo wadogowadogo kawaida huwa ni katika kipindi cha nyakati hizi.

Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba Hifadhi hii ya milima ya Mahale inapatikana mbali sana kijiografia na inashauriwa kwa Watanzania watalii wa ndani wajiandalie vyakula vyao wenyewe vya kujipikia katika siku kadhaa watakapokuwepo hifadhini kimatembezi.

Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale ina jumla ya mabanda matano (5) ambayo yana huduma za choo kwa ndani na kila banda lina vyumba viwili na kila chumba kina vitanda viwili ambapo kwa ujumla wake yanaweza kulaza wageni watalii wanne (4) kwa kila banda. Pia panapatikana huduma ya jiko pamoja na vifaa vya jikoni kwa ajili ya kujipikia chakula binafsi. Maeneo ya kupiga kambi za kutumia mahema zinapatikana katika hifadhi, nyumba za kulala wageni hifadhini. Lakini inashauriwa na kusisitizwa kujibebea mahema kwa ajili ya malazi kuliko kutegemea ya hifadhini

Kunapatikana kimsingi kambi tatu za wawekezaji kama vile; kambi ya GREYSTOKE – NOMAD ambayo inamilikiwa na NOMAD TANZANIA LTD na ina uwezo wa kulaza wageni kumi na nne; KAMBI YA MBALIMBALI iko chini ya usimamizi na umiliki wa 86 - HILLTOP/MBALIMBALI inayopatikana Kigoma mjini katika eneo la Sinsiba ambako ni jirani na kusini mwa mabanda ya Shirika la Hifadhi za Taifa yanayopatikana katika eneo la Kasiha. Kambi hii ina uwezo wa kuwa na vitanda 20; KAMBI YA FLYCATCHER – kambi hii iko chini ya usimamizi na umiliki wa FLYCATCHER SAFARIS. Inapatikana takribani kilometa tatu hivi kaskazini mwa mabanda ya Shirika la Hifadhi za Taifa katika eneo la Kasiha. Uwezo wake ni takribani vitanda 12.

Elimu itolewe kwa Watanzania watalii wa ndani kabla ya matembezi hifadhini na vile vile popote pale wanapokuwa hifadhini katika masuala ya mambo muhimu yanayohusiana na usalama wao wenyewe na mambo mengineyo muhimu kama vile kuzifahamu sheria za Hifadhi za Taifa.

Mambo muhimu ya kufanya na kuzingatia
(kanuni na taratibu ndani ya hifadhi)

Safari utalii yenu ya matembezi hifadhini inachukua siku ngapi? Je fedha zenu kibajeti zinakidhi gharama za kuendelea kuwepo hifadhini au hapana? Haya yote ni masuala ya msingi katika kujiuliza. Matembezi ya utalii hifadhini ni fedha.   

zingantiaji na ufuatiliaji wa umakini wa kanuni na taratibu zake hifadhini. 

TARATIBU ZA KUANGALIA SOKWEMTU

Lazima ubaki umbali wa mita kumi kutoka kwenye kundi la Sokwemtu wakati wote kwani hii inapunguza hatari ya wewe mtalii kuwaambukiza au kuambukizwa vijududu na virusi vya magonjwa baina ya Sokwemtu na binadamu.

Muda wote wa kuangalia Sokwemtu unatakiwa uvae kichuja hewa au barakoa ambayo hufunika pua na mdomo. Kifaa hiki utapatiwa na muongozaji wageni watalii anayewaongoza katika safari utalii yenu ya matembezi ya miguu katika kuwaona Sokwemtu pale ambapo mtakapowasogelea Sokwemtu takribani umbali wa mita 50.

Usile wala kunywa kitu chochote kile wakati mtakapokuwa karibu na Sokwemtu. Inafaa kula au kunywa kitu chochote kile pale ambapo utakapokuwa umbali wa takribani mita 250.

Beba vifaa vyako vyote wakati wote kwasababu baadhi ya vifaa vyako vinaweza kuambukiza maradhi au magonjwa kwa wanyamapori Sokwemtu na kama itatokea ya kwamba unahitaji msaada wa kubebewa vifaa vyako basi bila shaka muongozaji wageni watalii anayewaongoza na kuwasimamia atakuwa wa kwanza kutoa msaada wa kuwabebea vifaa vyenu. 

Usitupe taka hovyo ndani ya Hifadhi kwasababu ni hatarishi kwa afya na maisha ya wanyamapori na vilevile inaweza kuambukiza magonjwa au maradhi kwa Sokwemtu. 

Jitahidi kujizuia kupiga chafya na kutema mate uwapo ndani ya Msitu na endapo kama itatokea unapiga chafya au kukohoa basi bila shaka tafadhali ziba au funika mdomo wako ili kupunguza uwezekano wa wewe katika kueneza virusi vya magonjwa kwa wanyamapori Sokwemtu. 

Epuka kujisaidia ndani ya Msitu na kama inashindikana basi bila shaka jaribu kusogea umbali wa takribani mita 250 kutoka pale walipo Sokwemtu na pia umjulishe muongozaji wageni watalii uliyenaye ili akusaidie kuchimba shimo la walau sentimeta 30. 

Hairuhusiwi kwenda au kushiriki matembezi ya miguu katika kuwaona Sokwemtu kama wewe ni mgonjwa au una maradhi au magonjwa ya kuambukiza na ni vema na busara ukapatakuweza kuwasiliana na meneja wa kambi au muongozaji wageni watalii uliyenaye kama itatokea ya kwamba haujisikii vizuri kiafya kama tahadhari muhimu kwa upande wako. 

Watoto wenye kuwa na umri wa chini ya miaka 12 hawaruhusiwi kabisa kuingia ndani ya msitu katika matembezi ya miguu na kutalii katika kuwaona Sokwemtu. Hii ni kwa ajili ya usalama wa watoto wenyewe na vilevile pia kwa afya ya Sokwemtu kwasababu ni rahisi sana kwa watoto wa binadamu kueneza magonjwa ya kuambukiza. 

Haitakiwi kabisa kuzidi watu 6 pamoja na muongozaji wageni watalii mmoja ambao kimsingi wanaruhusiwa kushiriki matembezi ya miguu na kutalii katika kujionea wanyamapori Sokwemtu kwa wakati mmoja.

Muda wa kuwatazama Sokwemtu ni saa moja tu katika siku. Iwapo Sokwemtu ikatokea wanatembea na kukawa na muingiliano wakati wa kuwaangalia basi bila shaka muda utasimamishwa mpaka Sokwemtu watakapokuwa wameonekana vizuri na kutulia. Hairuhusiwi kabisa kuendelea kuwafuata kwa zaidi ya saa 3 kama imefanikiwa kuwaona kwa mara moja hata kama muda wa saa moja wa kuwaona Sokwemtu haujaisha au kutamatika. Hii inasaidia kupunguza usumbufu kwa Sokwemtu na wanyamapori wengine wa msituni.

Vifaa muhimu vya kuchukua katika safari utalii hifadhini

Mambo yote muhimu ambayo yamekwishaelezewa kwa Watanzania watalii wa ndani wanaojiandaa na matembezi hifadhini.

Huduma za mahitaji mengineyo

Mambo ya ziada ya mahitaji yanayojitokeza na upatikanaji wake katika sehemu husika ambapo Watanzania watalii wa ndani walipo.

Maelezo ya huduma za habari utalii wa ndani.

MAWASILIANO MENGINEYO MAKAO MAKUU (TANAPA)

+255 272508216

info@domestictourismsafaris.c  info@domestictourismsafaris.co.tz