TALII NA TEMBELEA HIFADHI YA TAIFA KITULO (BUSTANI YA MUNGU)
Mkoani Jombe pamoja na mkoani mbeya katika kanda ya nyanda za juu kusini mwa jamhuri ya muungano wa Tanzania (Southern highlands region)
Chanzo Cha Chimbuko Halisia Kimaelezo Na Ubunifu (Mwalimu Edgardo Kabulwa Welelo)
Ukweli Wa Mambo Kuhusiana Na Hifadhi Ya Taifa Kitulo (Bustani Ya Mungu) Mkoani Njombe Na Mkoani Mbeya (Nyanda Za Juu Kusini) Mwa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania; Hifadhi ya Taifa Kitulo (Bustani Ya Mungu) ipatikanayo kijiografia katika Nyanda za Juu Kusini (Southern Highlands Region) Mkoani Mbeya katika wilaya za Rungwe na Mbeya vijijini pamoja na Mkoani Njombe katika wilaya ya Makete ina jumla ya ukubwa wa eneo lenye kuwa na kilometa za mraba takribani 465 nukta 4 na vilevile inapatikana katika mwinuko wa mita 2500 mpaka 3000 kutoka usawa wa bahari.
Ushauri kwa watalii raia wa Tanzania katika kujiandaa na kujipanga kimaandalizi na kikamilifu kwa safari utalii
Iwe usafiri binafsi au usafiri wa kukodi ni lazima fungu la fedha litengwe pembeni ili kufanikisha safari ya utalii na matembezi hifadhini Kitulo. Mambo muhimu ya kujiuliza je ni vitu gani ambavyo ni muhimu vinavyohitajika na vitu gani visivyohitajika ni suala la utafiti wa kuangalia na kupata maelezo ya kina kuhusiana na sehemu hii mnayokusudia kutalii na kuitembelea. Taarifa na maelezo ni mambo muhimu na yanayohitajika kupewa kipaumbele cha hali ya juu kabisa.
Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba historia ya eneo hili la Kitulo ilianzia mnamo mwaka wa 1870 wakati ambapo mpelelezi ajulikanaye kwa majina ya Fredrick Elton alipotembelea na kuipatia jina lake mwenyewe kama ELTON. Mnamo mwaka wa 1960 eneo kubwa la Kitulo lilichukuliwa na Shirika La Umoja Wa Mataifa linalojishughulisha na chakula na pia kilimo (FAO) kwa ajili ya mradi wa majaribio ya kilimo cha ngano pamoja na kondoo wa sufi. Hatahivyo, baadaye eneo hili la Kitulo lilibadilishwa na kufanywa kuwa shamba la kufugia ng’ombe. Kutokana na maoni ya taasisi za uhifadhi na wadau mbalimbali wa mazingira, sehemu ya shamba, hifadhi ya misitu ya milima ya Livingstone na bonde la Nhumbe vikatangazwa rasmi mnamo tarehe 16 mwezi wa Septemba mwaka wa 2005 kupitia gazeti la serikali namba 279 na kuwa Hifadhi ya Taifa Kitulo.
Ukubwa wa eneo la Hifadhi ya Taifa Kitulo ni takribani kilometa za mraba 465 nukta 4. Na uwepo wake kijiografia katika Nyanda za Juu Kusini kunapelekea hifadhi hii kuwa na hali yake ya hewa ya baridi na mwezi wa Juni na Agosti inakuwa ni baridi sana. Mvua ni nyingi na joto kawaida ni la chini.
Kwa njia ya usafiri wa barabara, hifadhi hii inafikika kutokea jijini Dares – Salaam – Makambako – Njombe – Makete – Kitulo, takribani umbali wa kilometa 963. Dares – Salaam – Chimala – Matamba – Kitulo, takribani umbali wa kilometa 836, na vilevile Mbeya mjini – Isyonje – Kitulo, takribani kilometa 67, na pia Mbeya mjini – Chimala – Kitulo, takribani kilometa 103. Kwa usafiri wa njia ya reli au treni ni kupitia vituo vya Makambako, Chimala na Iyunga Mbeya. Kwa usafiri wa njia ya anga ni kupitia katika uwanja wa kimaifa wa ndege Songwe, kupitia Isyonje ni takribani umbali wa kilometa 88 na vilevile kupitia Chimala ni takribani kilometa 125.
Uoto wa asili, mandhari nzuri yenye kupendeza ya milima, pamoja na uoto wa asili wa milimani.
Ni takribani mita 2600 baina ya vilele vya milima Kipengere, Mporoto na Livingstone. Tabia nchi huathiriwa na mambo mawili kama vile mwinuko kutoka usawa wa bahari pamoja na Ziwa Nyasa (Ziwa Malawi). Kiwango cha juu cha hali ya hewajoto kwa siku ni baina ya nyuzi joto 14 nukta 5 na nyuzi joto 18, na kiwango cha chini kabisa ni kati ya nyuzi joto 7 na 8 baina ya mwezi Desemba pamoja na mwezi Aprili. Wakati 94 - mwingine hutokea kushuka kwa joto na kufikia nyuzi joto takribani 0 nukta 5 (kuanzia mwezi wa Juni hadi mwezi wa Agosti, kipindi ambacho huwepo kwa theluji). Wastani wa mvua kwa mwaka ni takribani milimita 1600 ikitofautiana pia kati ya milimita 1500 na milimita 1700. Msimu wa mvua huwa ni kati ya mwezi wa Oktoba mpaka mwezi wa Mei.
Ni pamoja na maua ya porini, mimea mikuu, aina kadhaa za viumbe hai ndege, vipepeo, vinyonga, mijusi pamoja na vyura. Kwa ujumla wake vivutio vikuu vya utalii Hifadhini Kitulo inaweza kuelezewa kama ifuatavyo;
1. Bonde La Nhumbe; Bonde la Nhumbe lina vijito vidogo pembezoni mwa vilima ambavyo hutiririka na pia kutengeneza maporomoko ya maji yenye kuwa na maji yenye kufikia urefu wa zaidi ya mita 100, ambayo chanzo chake ni cha mto Nhumbe. Mto Nhumbe ni mkondo mkuu wa mto RUAHA. Bonde lake limetawaliwa na miti aina ya Mitarakwa na ni miongoni mojawapo ya miti mirefu Afrika ya Mashariki ambayo hufikia urefu wa takribani mita 50.
2. Safu Za Milima; Milima ya Livingstone imepambwa na misitu ya mianzi na miti ya asili. Pia hupatikana Mitulunga, Mitarakwa na Mikangazi.
3. Uoto Wa Asili; Hifadhi ya Taifa Kitulo ina jumla za aina za mimea takribani 350. Miinuko hiyo ni eneo muhimu kijiografia kwa aina za mimea ipatikanayo hasahasa katika ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika. Pia ni maarufu kwa kuwa na aina mbalimbali za mimea ambazo ni adimu kupatikana katika maeneo mengineyo ya uhifadhi nchini Tanzania.
4. Maua; Hifadhi ya Taifa Kitulo ni miongoni mwa maeneo mazuri ya maua ya asili duniani, ambayo kati ya hayo, kunapatikana zaidi ya aina 40 za maua ya mimea ya kikanda, ambapo aina 31 zinapatikana pekee nchini Tanzania, aina 16. Hifadhi ya Taifa Kitulo na milima ya Uporoto zinapatikana aina 3 za mimea yenye kuwa na upekee tofauti. Maua haya huchanua na kujitandaza mithili ya bustani yenye kuwa na rangi mbalimbali za maua kuanzia mwishoni mwa mwezi Novemba hadi Aprili.
5. Mandhari Ya Eneo Lenye Kupendeza; Hifadhi ya Taifa Kitulo ina eneo kubwa lenye kuwa na mwinuko ambao ni uwanda wa nyasi, milima inayoizunguka mbuga, maporomoko ya maji, mito, pamoja na ziwa la kreta (crater lake).
6. Uwanda Wa Juu; Uwanda wa juu una aina kuu tatu za uoto wa asili; mosi, nyika kavu kwenye udongo wa Volkano wenye kuwa na aina mbalimbali za mimea; pili, ardhi oevu (wetland) ya 95 - kudumu na pia yenye kuwa na aina nyingi za mimea kimsimu; na tatu, miinuko iliyopambwa na miamba geu pamoja na mimea mbalimbali.
7. Viumbe Hai Ndege; Hifadhi ya Taifa Kitulo ni mojawapo ya maeneo nchini Tanzania katika upatikanaji wa aina mbalimbali za viumbe hai ndege kama vile ndege wahamao kutokea bara Ulaya na maeneo ya bara la Afrika. Kwa mfano Korongo Mayobwe na Korongo Mweupe ambao hufika hifadhini Kitulo wakitokea barani Ulaya. Pia hifadhini Kitulo ni makazi na mazalia ya mbayuwayu wa rangi ya bluu na Tandawala Machaka. Baadhi ya ndege wakazi (resident birds) wa Kitulo ni kama vile Kestreli wadogo pamoja na ndege wawindaji (raptors/birds of prey), na pia Njombe cisticola, na wengineo wengi.
8. Wanyamapori; Hifadhi ya Taifa Kitulo ina wanyamapori wa aina mbalimbali kama vile Tohe Mlima, Mbweha, Sungura, Mbega wenye kuwa na rangi nyeupe na nyeusi, Minde, Pundamilia na Mbuzi Mawe. Pia panapatikana wanyamapori jamii ya nyani (primates) aliyegunduliwa katika miaka ya hivi karibuni anayefahamika (Rungwecebus kipunji) pamoja na wanyamapori wengineo wadogo na wa kati. Vivutio vinginevyo nje ya hifadhi ni kama vile fukwe za matema, daraja la asili la Kiwira, Ziwa Ngozi, Ziwa Masoko, maporomoko ya maji – Kimani, kimondo cha Mbozi, na kadha wa kadhalika.
Ni pamoja na utalii wa kutumia magari (vehicle game viewing), utalii wa matembezi ya miguu (walking safaris) – masafa mafupi takribani saa 1 mpaka 4, masafa marefu takribani zaidi ya saa 4, utalii wa kupiga kambi kwa kutumia mahema (camping sites), utalii wa utazamaji viumbe hai ndege (birds watching), utalii wa upigaji picha na kadha wa kadhalika. Pia panapatikana huduma ya utalii wa kiutamaduni (cultural tourism) wa makabila makubwa yanayoishi na kuizunguka Hifadhi ya Taifa Kitulo kama vile makabila ya Wakinga, Wawanji, Wasafwa na Wanyakyusa ambayo yanaishi maisha yao ya kawaida. Makabila haya yanajishughulisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi kama vile kilimo na ufugaji. Ni vema ukapata muda wa kutembelea jamii hizi ili kujifunza mila na desturi zao.
Wanyamapori ni wachache sana ukilinganisha na hifadhi nyinginezo nchini Tanzania. Wanyamapori wapatikanao zaidi ni kama vile Tohe mlima na Pofu, Pundamilia, na wengineo wadogo wadogo na wa kati. Hifadhi ya Taifa Kitulo ni eneo muhimu kwa aina mbalimbali za viumbe hai ndege, wahamao (migratory birds) kutokea barani Ulaya na maeneo mengineyo ya Afrika. Kwa mfano Korongo Mayobwe na Korongo Mweupe 96 - hufika hifadhini Kitulo wakitokea barani Ulaya. Hali kadhalika pia Hifadhi ya Taifa Kitulo ni makazi na mazalia ya mbayuwayu wa bluu na Tandawala Machaka. Baadhi ya ndege wakazi (resident birds) wa Kitulo ni kama vile Kestreli wadogo, Njombe cisticola na ndege wawindaji (raptors/birds of prey).
Uoto wa asili wa milimani pamoja na maua ya porini. Hifadhi ya Taifa Kitulo ina jumla ya aina mbalimbali za mimea takribani spishi 350.
Watanzania watalii wa ndani wapendeleao kutazama uoto wa asili wa maua pori ni kuanzia mwezi wa Desemba na Aprili. Kwa wanaopendelea upandaji wa milima ni kuanzia mwezi wa Septemba na Novemba pale panapokuwepo mwanga wa jua. Kwa usafiri wa anga ni kupitia lango la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe – kupitia Isyonje ni takribani umbali wa kilometa 88 na vilevile kupitia Chimala ni takribani kilometa 125. Kwa njia ya usafiri wa barabara ni kupitia jijini Dares – Salaam – Makambako – Njombe – Makete – Kitulo ni takribani kilometa 963, na vilevile kupitia jijini Dares – Salaam – Chimala – Matamba – Kitulo ni takribani umbali wa kilometa 836. Kutokea Mbeya Mjini – Isyonje – Kitulo ni umbali wa takribani kilometa 67, Mbeya Mjini – Chimala – Kitulo ni umbali wa kilometa takribani 103. Kwa usafiri wa reli au treni – ni kupitia vituo vya Makambako, Chimala na Iyunga Mbeya.
Huduma za chakula hifadhini na nje ya hifadhi zinapatikana. Lakini inashauriwa na kupendekezwa kwa Watanzania watalii wa ndani watokao mbali wakawa wamejiandaa kikamilifu wakiwa na vyakula vyao wenyewe vya kujipikia.
Huduma za malazi hifadhini zinapatikana kama vile kambi za Jumuiya (public campsites). Inashauriwa na kupendekezwa kwa watanzania watalii wa ndani wakajibebea mahema yao wenyewe ya malazi kwa ajili kupiga mahema. Nje ya hifadhi vile vile kuna huduma zinazopatikana za malazi kama vile nyumba za kulala wageni za mji mdogo wa Matamba (Kitulo God’s Garden, Zebra Guest, Eden Motel, Mama Izengo Guest, Mtanganyika Lodge, na Rena Bluemen), bila kusahau jiji la Mbeya.
Ni masuala ya pamoja kiujumla wake yanayohusiana na maandalizi ya usafiri utalii na matembezi hifadhini Kitulo, huduma za chakula, malazi au kulala na mengineyo yaliyo muhimu. Tozo ni kama vile;
1. Tozo ya kuingia ndani ya Hifadhi kwa mtu mmoja (umri wa miaka 16 na zaidi, umri kati ya miaka 5 na 15, na umri chini ya miaka 5).
2. Tozo ya Magari (uzito hadi 2000, uzito kati ya kilo 2000 mpaka 3000, uzito kati ya kilo 3001 mpaka 7000, na uzito zaidi ya kilo 7001).
3. Tozo ya Kambi ya jumuiya (public campsites) - umri wa miaka 16 na zaidi, umri kati ya miaka 5 na 15, na umri chini ya miaka 5).
4. Tozo ya Kambi maalumu (special campsites) – umri wa miaka 16 na zaidi, umri kati ya miaka 5 na 15, na umri chini ya miaka 5).
5. Tozo ya uongozaji wageni watalii (Tour guiding fees) – tozo ya uongozaji safari utalii wageni, tozo ya muongozaji wageni maalumu.
6. Tozo ya safari utalii wa matembezi ya miguu kwa muda mfupi na muda mrefu (matembezi ya miguu ya muda mfupi takribani saa 1 mpaka 4 kwa mtu mzima, matembezi ya miguu ya muda mfupi takribani saa 1 mpaka 4 kwa mtoto mwenye umri zaidi ya miaka 12, matembezi ya miguu ya muda mrefu takribani zaidi ya saa 4 kwa mtu mzima, na matembezi ya miguu ya muda mrefu takribani zaidi ya saa 4 kwa mtoto zaidi ya miaka 12).
7. Tozo ya kurekodi kwa siku kwa mtu mmoja.
8. Tozo ya mpagazi (porter) raia wa Tanzania inajumuisha viingilio vya kuingilia na malazi kambini.
9. Tozo ya utalii wa kula chakula porini.
10. Tozo kwa wanafunzi na wanachuo kutoka katika taasisi za kielimu za ndani ya nchi kwa wenye kuwa na vibali.
11. Kibali cha mwaka cha mkurugenzi wa wakala wa utalii.
12. Tozo ya kambi za kuhamahama.
13. Faini ya kuzidisha mwendo kasi kwa magari yote. Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba TOZO zinaweza kubadilika wakati wowote ule.
Je mtalala hifadhini au je hamtalala ndani ya hifadhi? Haya maswali ndio yatakayowapeni muongozo wa maamuzi yenu mtakayoafiki yafanyikeje.
Mambo muhimu ya kufanya na kuzingatia
(kanuni na taratibu ndani ya hifadhi)
Ni vizuri wana vikundi katika safari utalii na matembezi hifadhini kupeana na kuelimishana elimu inayohusiana na huduma ya kwanza na jinsi ya kukabiliana na majanga yeyote yawezayo kujitokeza hifadhini. Kanuni na taratibu ndani ya Hifadhi ni kama vile;
1. Tumia barabara au njia, au alama ndani ya Hifadhi zilizoruhusiwa na uongozi wa Hifadhi.
2. Usitupe taka hovyo Hifadhini.
3. Ni marufuku kabisa kupiga kelele au kupiga honi ndani ya Hifadhi.
4. Ni marufuku kabisa kuendesha gari katika mwendo kasi zaidi ya kilometa 50 kwa saa.
5. Usiwashe au kusababisha moto ndani ya Hifadhi.
6. Ni marufuku kabisa kuwasumbua na vilevile kuwapatia na kuwalisha chakula wanyamapori ndani ya Hifadhi.
7. Usiingize mnyama yeyote yule afugwaye majumbani na binadamu ndani ya Hifadhi, au kuingia ndani ya Hifadhi na silaha ya aina yeyote ile.
8. Usiogelee katika mito au maporomoko ya maji.
9. Muda wa kuwa ndani ya Hifadhi ni kati ya saa 12;30 Asubuhi na saa 1;00 jioni.
Vifaa muhimu vya kuchukua katika safari utalii hifadhini
Ni kama vile vitabu viongozi (guide books) mbalimbali vya kielimu vya mambo ya hifadhini vya mimea, wanyamapori, ndege na kadhalika. Vile vile vifaa kama vile viona mbali (Binoculars), kamera na vinginevyo muhimu.
Vifaa vyote muhimu katika safari utalii yenu ya matembezi hifadhini. Mfano hai ni kama vile mahema (tents) kama mtalala ndani ya hifadhi, vyombo vyenu wenyewe vya kujipika na maji ya kunywa. Orodha ni ndefu na inategemea na mtakavyojipanga kwa mujibu wa bajeti yenu kifedha wenyewe ndugu watanzania.
Huduma za mahitaji mengineyo
Haya ni mambo ya ziada ya mahitaji yanayojitokeza na upatikanaji wake katika
sehemu husika ambayo watanzania watalii wa ndani walipo.
Maelezo ya huduma za habari utalii wa ndani.
Kampuni ya Uelimishaji,Uratibu,Uandaaji,Uhamasishaji, na Uwezeshaji Utalii wa Ndani
Follow us:
MAWASILIANO MENGINEYO MAKAO MAKUU (TANAPA)
- Juma tatu - Ijumaa
- 8:00 Asubuhi - 4:30 Jioni
+255 272508216
info@domestictourismsafaris.c info@domestictourismsafaris.co.tz



