TALII NA TEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA KISIWA CHA SAA NANE (SAANANE ISLAND NATIONAL PARK)

Mkoani Mwanza katika ukanda wa ziwa Victoria/nyanza) mwa jamhuri ya muungano ya Tanzania (The united republic of Tanzania

Chanzo Cha Chimbuko Halisia Kimaelezo Na Ubunifu (Mwalimu Edgardo Kabulwa Welelo), Master of the Game.

Ukweli Wa Mambo Kuhusiana Na ‘Hifadhi Ya Taifa Ya Kisiwa Cha Saa Nane’ (Saanane Island National Park); Hii ndio ‘Hifadhi ya Taifa’ (National Park) iliyo ndogo kuliko zote nchini kwetu Tanzania na ‘Afrika Mashariki’. Jina la ‘Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saa Nane’ (Saanane Island National Park) kinachopatikana katika ‘Ziwa Victoria (Nyanza)’ katika ‘Mkoa wa Mwanza’ kimetokana na raia mtanzania mwenyeji asilia wa eneo hili ambaye alikuwa mvuvi na mmiliki wa kisiwa hiki aliyejulikana kwa majina kama ‘Mzee Saa Nane Chawandi’ ambaye aliachia eneo hili la kisiwa kwa ‘Serikali yetu ya Tanzania’ kwa ajili ya kupisha ‘uhifadhi endelevu wa eneo hili’ baada ya yeye mwenyewe ‘Mzee Saa Nane Chawandi’ kufidiwa gharama za eneo lake na ‘Serikali ya Tanzania’’ mnamo miaka ya 1960. Hatimaye mara moja ‘Serikali ya Tanzania’ ikalianzisha eneo hili la kisiwa kama ‘Bustani ya Wanyamapori’ (Wildlife Zoo) ya kwanza kabisa nchini kwetu Tanzania katika mwaka wa 1964. Malengo ya ‘Serikali’ ya wakati wa kipindi kile ilikuwa ni kuendeleza uhifadhi endelevu wa eneo lenyewe pamoja na kuhamasisha na kuelimisha elimu ya utalii na mazingira kwa raia watanzania wenyewe na wageni kutoka nje ya nchi lakini vilevile ilikuwa na pia kutoa burudani kwa wakazi wa ‘Mji na Mkoa wa Mwanza’ na sehemu nyinginezo za nchi yetu ya Tanzania.

Historia ya hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Saanane (Saanane island national park)

Kati ya mwaka ‘1964 mpaka 1966’, shirika la ‘Hifadhi za Taifa nchini Tanzania’ (Tanzania National Parks Authority) liliwasafirisha na kuwaleta wanyamapori wa aina mbalimbali katika ‘Kisiwa hiki cha Saanane’ kutoka katika maeneo mbalimbali ya uhifadhi nchini kwetu Tanzania.Wanyamapori hawa ilikuwa ni pamoja na Nyati/Mbogo (African/Cape/Savanna Buffalo) ,Pongo (Bushbuck),Digidigi au Saruya(Kirk’s dikdik),Tembo/Ndovu (African/Bush/Savanna Elephant),Pofu (East African Eland/ Patterson Eland), Swala Pala (Impala),Faru (Black Rhinos), Nyamera (Topi) ,Ngiri (Common Warthog) pamoja na Nyumbu (White – Bearded Wildebeest).Wanyamapori wengineo ni pamoja na Pundamilia(Plains/Burchell’s/Common Zebra) ,Nyani (Olive/Savanna Baboon) ,Twiga (Maasai/ Kilimanjaro Giraffe,Nungunungu (Ground Crested Porcupine) pamoja na mamba (Nile Crocodile).Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba hii ndio ‘Hifadhi ya Taifa’ (National Park) ya pili inayopatikana katika ziwa ‘Victoria (Nyanza)’ katika ‘Mkoa wa Mwanza’ baada ya ‘Hifadhi ya Taifa ya visiwa vya Rubondo’ (Rubondo Island National Park) ambavyo navyo pia vinapatikana katika ‘Mkoa wa Mwanza’

Ushauri kwa watalii raia wa Tanzania katika kujiandaa na kujipanga kimaandalizi na kikamilifu kwa safari utalii

Mipango na utaratibu wa safari utalii ya matembezi ya kutembelea ‘Hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Saa Nane’(Saanane Island National Park) kwa njia ya usafiri wa majini wa boti zenye injini huandaliwa kwa kuwasiliana na kupata taarifa kutoka katika ‘Makao Makuu ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saa Nane’ yanayopatikana ‘Capri Point’ katika wilaya ya ‘Nyamagana’.

hifadhi hii ya ‘taifa ya kisiwa cha saa nane’ (saanane island national park) ilianzishwa rasmi mnamo mwaka 2012 baada ya kupitishwa na kudhibitishwa na sheria za ‘bunge la tanzania’ katika mwezi oktoba, 2012.

Mpaka hivi sasa ‘hifadhi hii ya taifa ya kisiwa cha saa nane’ (saanane island national park) ina ukubwa wa eneo lenye kuwa na kilomita za mraba ‘ 0 nukta 7’ ambapo inajumuisha kwa pamoja eneo la nchi kavu na majini.lakini hata hivyo kuna mipango na mikakati ya baadaye ya kuliongeza eneo hili ukubwa wake wa eneo ambapo itahusisha visiwa viwili vidogo vya ‘chankende kubwa’ na ‘chankende ndogo’ katika upande wa kusini kijiografia na kulifanya eneo hili la ‘kisiwa cha saa nane’ kufikia ukubwa wa eneo la kilomita za mraba takribani ‘1nukta 32’. ikumbukwe na ieleweke ya kwamba hii ndio ‘hifadhi ya taifa’ (national park) pekee iliyo ndogo nchini kwetu tanzania na afrika ya mashariki mpaka wakati huu.

ufikaji hifadhini katika ‘hifadhi ya taifa ya kisiwa cha saa nane’(saadani island national park) hufanyika kupitia katika ‘makao makuu ya hifadhi’ yanayopatikana ‘capri point’ katika ‘wilaya ya nyamagana’.

Mandhari nzuri yenye kupendeza na kuvutia ya maumbile ya kijiografia ya ‘Mji wa Mwanza’, ‘Ziwa Victoria (Nyanza)’ pamoja na ‘Miamba ya Ardhini katika Uso wa Ardhi’(Rocky Outcrops/Kopjes) na vilevile ‘Uoto wa Asili wa Mimea wa Ukanda wa Ziwa Victoria/Nyanza’ (Lake Victoria Vegetation Zone).

Ni pamoja na ‘Utazamaji Viumbe Hai Ndege na Wanyamapori’ katika mwambao wa ‘Ziwa Victoria’,upandaji katika ‘Miamba ya Ardhini katika Uso wa Ardhi’ (Rocky Outcrops/Kopjes), mapumziko au mandale (picnic site).

Ni pamoja na viumbe hai ‘Jamii ya Nyani (Primates)’ kama vile Tumbili /Ngedere(Vervet Monkeys/ Black – Faced Monkeys), De-Brazzas Monkeys. Wengineo ni pamoja na paka pori (Wild Cat), Pimbi(Hyraxes) ,Swala Pala (Impala).Viumbe hai watambaao (Reptiles) ni pamoja na Kenge (Monitor Lizard) ,Koromondo (Agama Lizards) ,Nyoka (Snakes), Mamba (Nile Crocodiles), na Kobe (Tortoises).

Maelezo ya huduma za habari utalii wa ndani.

MAWASILIANO MENGINEYO MAKAO MAKUU (TANAPA)

+255 272508216

info@domestictourismsafaris.c  info@domestictourismsafaris.co.tz