TALII NA TEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA VISIWA VYA RUBONDO (RUBONDO ISLAND NATIONAL PARK)

Mkoani Mwanza (Mwanza Region) katika Ukanda wa Ziwa Victoria/N yanza (Lake Victoria/Nyanza Region Zone) mwa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania (The United Republic of Tanzania)

Chanzo Cha Chimbuko Halisia Kimaelezo Na Ubunifu (Mwalimu Edgardo Kabulwa Welelo)

Ukweli Wa Mambo Kuhusiana Na Hifadhi Ya Taifa Ya Visiwa Vya Rubondo (Rubondo Island National Park) Mkoani Mwanza (Mwanza Region) Katika Ukanda Wa Ziwa Victoria (Lake Victoria/Nyanza Region Zone) Mwa Jamhuri Ya Muungano Ya Tanzania (The United Republic of Tanzania); Hifadhi ya Taifa ya Visiwa vya Rubondo (Rubondo Island National Park) ni mojawapo ya hifadhi pekee ‘’Nchini Kwetu Tanzania’’ na ‘’Barani Afrika’’ kwa ujumla wake ipatikanayo katika makazi ya maji ya ‘’Ziwa Victoria/Nyanza’’ (Lake Victoria). Kijiografia,hifadhi hii inapatikana ndani ya ‘’Ziwa Victoria/Nyanza (Lake Victoria/Nyanza) katika upande wa ‘’Kaskazini Mwa Ghuba ya Emini Pasha’’ (Emin Pasha Gulf), Mkoani Mwanza (The Rock City). Hifadhi hii ya ‘’Taifa ya Visiwa vya Rubondo’’(Rubondo Island National Park) ilianzishwa rasmi mnamo ‘’Tarehe 18 ya Mwezi Januari’’ ya ‘’Mwaka wa 1977’’. Ukubwa wa eneo la ‘’Hifadhi ya Taifa ya Visiwa vya Rubondo’’(Rubondo Island National Park) ni takribani kilometa za mraba 457, ambapo kilometa za mraba takribani 237 ni eneo la nchi kavu na takribani kilometa za mraba 220 ni eneo la makazi ya maji ya ‘’Ziwa Victoria/Nyanza’’(Lake Victoria/Nyanza). Ni hifadhi ambayo kimsingi imezungukwa na visiwa kadhaa kama vile visiwa vya ‘’Mizo’’, ‘’Nyamitundu’’, ‘’Chitende’’, ‘’Rubiso’’, ‘’Chitebe’’, ‘’Kalera’’, ‘’Iroba’’, ‘’Chambuzi’’, ‘’Manyila’’, ‘’Makosi’’ pamoja na ‘’Izilambuba’’. Ni hifadhi ya Taifa nchini kwetu Tanzania ambayo kimsingi inatoa fursa kadhaa za kipekee zenye kupendeza na kuvutia kwa watalii wa ndani na nje ya nchi. Ikumbukwe na ifahamike ya kwamba kina cha maji cha ‘’Ziwa Victoria/Nyanza’’(Lake Victoria/Nyanza) kinapatikana katika eneo la ‘’Irumo’’, ndani ya ‘’Hifadhi hii ya Taifa ya Rubondo’’(Rubondo Island National Park). Kwa ufupisho, ‘’Hifadhi ya Taifa ya Visiwa vya Rubondo’’(Rubondo Island National Park) inapatikana kijiografia katika upande wa ‘’Kusini – Magharibi’’ mwa kona ya ‘’Ziwa Victoria/Nyanza’’(Lake Victoria/Nyanza Corner) Mkoani Mwanza (Mwanza Region).’’Makao makuu’’ ya ‘’Hifadhi ya Taifa ya Visiwa vya Rubondo’’ (Rubondo Island National Park Headquarters) yanapatikana katika eneo la ‘’Kageye’’. Ikumbukwe na ifahamike ya kwamba ‘’Hifadhi ya Taifa ya Visiwa vya Rubondo’’(Rubondo Island National Park) ina urefu wa eneo unaokadiriwa takribani kilometa 31 na upana wake ni eneo linalokadiriwa kuwa na takribani kilometa 3 mpaka 10. Ndani ya ‘’Hifadhi ya Taifa ya Visiwa vya Rubondo’’ (Rubondo Island National Park) panapatikana ‘’Miamba 2 Mikubwa (2 Rocky Hills/Rocky Outcrops/Kopjes) ambayo imefunikwa na uoto wa asili wa ‘’Misitu Minene’’(Dense Forests) sambamba na vichaka vilivyofungamana na maeneo ya wazi yaliyotawaliwa na uoto wa asili wa mimea nyasi. Kisiwa pekee ambacho kinapatikana katika mwinuko wa juu zaidi kutoka katika usawa wa bahari, ‘’Lwamtola Hills’’ ni takribani mita 351.

Ushauri kwa watalii raia wa Tanzania katika kujiandaa na kujipanga kimaandalizi kwa safari utalii

awe (260 of 266)

Ni pamoja na upatikanaji wa rasilimali fedha ambazo zitatumika katika kuwezesha na kufanikisha safari utalii za matembezi hifadhini.

Hifadhi ya Taifa ya Visiwa vya Rubondo (Rubondo Island National Park) ilianzishwa rasmi mnamo tarehe 18 ya ‘’Mwezi Januari’’ ya mwaka wa 1977.

Ukubwa wa eneo la ‘’Hifadhi ya Taifa ya Visiwa vya Rubondo’’ (Rubondo Island National Park) ni takribani kilometa za mraba 457, wakati ambapo kilometa za mraba takribani 237 ni eneo la nchi kavu na pia kilometa za mraba takribani 220 ni eneo la makazi ya maji ya ‘’Ziwa Victoria/Nyanza’’ (Lake Victoria/Nyanza).

’Hifadhi ya Taifa ya visiwa vya Rubondo’’ (Rubondo Island National Park) inafikika kwa njia ya utumiaji wa usafiri wa barabara kutokea ‘’Jijini Mwanza’’ (Mwanza City) kwa kutumia magari katika uelekeo wa kuelekea ‘’ Barabara ya Mwanza Sengerema – Geita – Nzera – Nkome’’. Ni sawa na mwendo wa takribani saa 5 mpaka 6. Kutokea ‘’Nkome’’, kunahitajika tena takribani mwendo wa saa 2 kwa utumiaji wa usafiri wa majini wa ‘’BOTI’’(Boat) zenye injini zinazotumia mafuta kuweza kufika hifadhini Rubondo. Njia nyingineyo mbadala ya ufikaji katika ‘’Hifadhi ya Taifa ya visiwa vya Rubondo’’(Rubondo Island National Park) ni kutokea katika upande wa magharibi. Kutokea ‘’Jijini Mwanza’’(Mwanza City) kunapatika pia njia ya kupitia ‘’Kivuko cha Busisi’’(Busisi Ferry) ambapo kwa hivi sasa mradi wa ‘’daraja la Busisi’’ umekamilika, ambapo njia hii inaelekea katika uelekeo wa ‘’Sengerema – Geita’’, na baadaye tena katika ‘’Barabara Kuu’’(Highway) inayoelekea ‘’Bukoba’’, na nchi ya ‘’Rwanda’’, ‘’Chato’’, na ‘’Muganza’’. Ni sawa na mwendo wa takribani saa 9 kutokea ‘’Jijini Mwanza’’(Mwanza City) kufika ‘’Muganza’’, na pia kutokea hapo hadi kufikia ‘’Hifadhi ya Taifa ya Visiwa vya Rubondo’’(Rubondo Island National Park) kwa kutumia usafiri wa majini unaotumia ‘’Boti’’(Boat) zenye injini zinazotumia mafuta ni sawa na mwendo wa takribani dakika 30 kupitia ‘’Kituo cha Askari wa Wanyamapori cha Mlaga’’(Mlaga Ranger Post). Pia vilevile panapatikana huduma ya Kiwanja kidogo cha ndege’’(Airstrip) karibu kabisa na lango la kuingilia ‘’Makao makuu - Kageye’’ ya Hifadhi ya Taifa ya visiwa vya Rubondo’’(Rubondo Island National Park - Kageye Headquarters).

Ni pamoja na ‘’Ziwa Victoria/Nyanza’’ (Lake Victoria/Nyanza), ‘’Visiwa 11 vinavyozunguka ‘’Hifadhi ya Taifa ya Visiwa vya Rubondo (Rubondo Island National Park) ambavyo visiwa hivi ni pamoja na ‘’Izilambuba’’, ‘’Makosi’’, ‘’Manyila’’, ‘’Chambuzi’’, ‘’Iroba’’, ‘’Kalera’’, ‘’Chitebe’’, ‘’Rubiso’’, ‘’Chitende’’, ‘’Nyamitundu’’, na ‘’Mizo’’. Vivutio vikuu vinginevyo vipatikanavyo hifadhini Rubondo ni pamoja na ‘’Miamba Miwili Mikubwa’ ’(2 Rocky Outcrops/Kopjes) ndani ya ‘’Ziwa Victoria/Nyanza’’ (Lake Victoria/Nyanza) moja katika upande wa ‘’Kaskazini’’ na jingine katika upande wa ‘’Kusini’’, pamoja na ’’Hifadhi ya Msitu (Forest Reserve).

Msimu wa kipindi cha mvua (Rainy Season) kawaida huanzia katika ‘’Mwezi Oktoba’’ mpaka ‘’Mwezi Mei’’, ambapo kimsingi hupatikana misimu miwili, msimu mmoja huanzia ‘’Mwezi Desemba’’, na msimu mwingine ni katika ‘’Mwezi Aprili na Mwezi Mei’’. Msimu wa kipindi cha kiangazi ni baina ya ‘’Mwezi Juni’’ na ‘’Mwezi Septemba’’. Kwa mujibu wa rekodi inaonyesha ya kwamba wastani wa mvua kwa mwaka ni takribani miririta 1200. Kwa ujumla wake na ukweli wa mambo ni kuwa ‘’Hifadhi ya Taifa ya Visiwa vya Rubondo (Rubondo Island National Park) ina hali ya hewa ya joto la wastani ambapo karibia mwaka mzima ni nyuzi joto 26 katika kiwango cha hali juu na pia kiwango cha chini cha joto ni nyuzi joto takribani 16. Hali ya hewa kutoka katika mwinuko wa usawa wa bahari ni takribani mita 1,134.

Ndege Wahamao(Migratory Birds),Fukwe(The Beach), ‘’Idadi Kubwa Ya Tai Walao Samaki(Fish Eagles)’’,’’Swala Nzohe’’(Sitatunga Antelopes), pamoja na idadi kubwa ya ‘’Viumbe Hai Vipepeo (Butterflies). Viumbe hai wanaotambaa (Reptiles) kama vile ‘’Kenge’’(Monitor Lizards), na ‘’Nyoka Chatu’’(Pythons). Ni vema na busara ikakumbukwa na kufahamika ya kwamba katika ‘’Hifadhi ya Taifa ya Visiwa vya Rubondo’’(Rubondo Island National Park) hakuna rekodi yeyote ile ya uwepo wa upatikanaji wa mammalia wakubwa wawindaji walao nyama (Mammalian Predators) kama vile ‘’Simba’’, ‘’Chui’’, ‘’Fisi’(Hyenas), na kadha wa kadhalika.

Kilicho cha kipekee na cha umuhimu wa aina yake tofauti kabisa na maeneo mengineyo ya uhifadhi ‘’nchini kwetu Tanzania’’ ni upatikanaji wa wanyamapori jamii ya swala wanaopendelea makazi ya maji ambao wanafahamika kama ‘’Swala Nzohe’’(Sitatunga Antelopes) ambao mojawapo ya maeneo mengineyo huweza kupatikana na kuonekana ni pamoja na ‘’Hifadhi ya Taifa ya Nyerere (Nyerere National Park) na Mto Malagarasi’’. Wengineo ni kama vile ‘’Nyani’’(Savanna/Olive/Anubis Baboon),’’Mbega wenye kuwa na rangi mchanganyiko ya weusi na weupe’’(Black – and White Colobus Monkeys), ‘’Kima’’(Blue/Syke’s Monkeys),‘’Nyati/Mbogo’’(Savanna/Cape/African Buffalo),’’Nguruwe Mwitu’’(Bushpigs),’’Pongo/Mbawala(Bushbucks),’’Sokwe Mtu’’(Chimpanzees),’’Digidigi/Saruya’’(Kirk’s Dikdik), ‘’Tembo/Ndovu’’(African/Bush/Savanna Elephant),’’Twiga’’(Maasai/Kenyan/Kilimanjaro Giraffe), ‘’Viboko’’(Common/East African Hippopotamus), ‘’Pimbi’’(Hyrax), ‘’Faru’’(Rhinos), ‘’, ‘’Kindi’’(Squirrel), ‘’Ngiri’’(Common Warthog),’’Kuro’’(Common Waterbuck),’’Tumbili/Ngedere’’(Black – Faced Monkey/Vervet Monkeys), ‘’Kanu Mkubwa Madoadoa’’(Large – Spotted Genet), ‘’Fisi Maji Madoa Shingoni’’(Spot – Necked Otter),’’Nguchiro Maji’’(Marsh Mongoose), ‘’Panya Walaji Miwa’’(Cane Rats), na bila kusahau viumbe hai wanaotambaa (Reptiles) aina ya ‘’Mamba’’(Nile Crocodile). Ni vema na busara ikakumbukwa na ikaeleweka ya kwamba ‘’Hifadhi ya Taifa ya Visiwa vya Rubondo’’(Rubondo Island National Park) imeripotiwa na kurekodiwa kitafiti na kisayansi kuwepo zaidi ya ‘’Spishi 200’’, za viumbe hai ndege wanaopatikana na kuishi ndani ya hifadhi, ambapo baadhi yao ni pamoja na ‘’Ndege Wahamao’’(Migratory Birds) wakitokea ‘’Afrika Mashariki, Magharibi na Kati’’. ‘’Hifadhi ya Taifa ya Visiwa vya Rubondo’’(Rubondo Island National Park) imebarikiwa sana pia kwa kuwa na idadi kubwa sana ya ‘’Ndege Korongo’’(Herons), ‘’YangeYange’’(Egrets), ‘’Storks’’, ‘’Ibises’’, ‘’Mnandi’’(Cormorants), ‘’Kingfishers’’, na bila kusahau ‘’Ndege Wawindaji Walao Nyama na Mizoga’’(Raptors/Birds of Prey). Ina aminika ya kwamba ‘’Hifadhi ya Taifa ya Visiwa vya Rubondo’’(Rubondo Island National Park) ina utajiri wa hali ya juu ya upatikanaji wa aina ya ndege wanaofahamika kama ‘’Tai Walao Samaki’’(Fish Eagles) duniani. Ni rahisi sana na wala hakuna ugumu wowote au changamoto yeyote ile kutoweza kuwaona aina hii ya viumbe hai ndege mara punde unapotembelea hifadhi hii. Kilicho cha muhimu na cha kipekee katika hifadhi hii ni ya kwamba yenyewe ni njia au lango la kuingilia ‘’Ndege Wahamao’’ (Birds Migratory Route) wanaotokea ‘’Barani Ulaya’’(Europe), ‘’Afrika ya Kati, Mashariki, na Magharibi’’(Central, East & West Africa). Miongoni mwao ni pamoja na ‘’Pin – Tailed Whydah’’, ‘’Red – Capped Robin Chat’’, ‘’Emerald – Spotted Wood Dove’’, ‘’Yellow – Billed Stork’’, ‘’Fire Finch’’, ‘’Saddle – Billed Stork’’, ‘’Marabou Stork’’, ‘’White Stork’’, ‘’Spoonbill Stork’’, ‘’Open – Billed Stork’’,’’White Pelican’’, ‘’Sacred Ibis’’, na ‘’Hadada Ibis’’.

Uoto wa asili unaopatikana hifadhini ni ‘’Uoto wa Asili wa Maeneo ya Kanda ya ‘Ziwa Victoria/Nyanza’’, unaofahamika kiutalamu kama (Lake Victoria Region Vegetation). Hata hivyo, kunapatikana aina kadhaa za uoto wa asili kama vile ifuatavyo;

1. ‘’Uoto wa Asili wa Maeneo ya Ardhi Oevu Pamoja na Uoto wa Nyasi KandoKando ya Ziwa (Papyrus Swamp & Lake – Edge Grassland). Katika eneo hili la uoto wa asili ni kuwa mimea iliyotawala na kutalamaki ni pamoja na mimea ya ‘’Koo’’ (Genus) ‘’Cyperus’’. Koo nyinginezo ni kama vile ‘’Phoenix’’, ‘’Panicum’’, ‘’Hemarthria’’, ‘’Mimosa’’, ‘’Cynodon’’, na ‘’Setaria’’.

2. ‘’Uoto wa Asili wa Mimea Nyasi Loudetia’’(Loudetia Grassland); Aina hii ya uoto wa asili ni maalum na asilia katika maeneo yenye kuwa na kina cha chini cha kuta katika udongo na kawaida mimea nyasi iliyotawala na kutalamaki katika kustawi ni aina ya mimea nyasi inayofahamika katika jina lake la kisayansi na kibotania kama ‘’Loudetia simplex’’. Hata hivyo, pia hupatikana aina nyinginezo za ‘’Koo’’ (Genera) za mimea nyasi kama vile, ‘’Acolanthus’’, ‘’Vernonia’’, ‘’Sporobolus’’, ‘’Eragrostis’’, na ‘’Andropogon’’.

3. ‘’Uoto wa Asili wa Mimea Miti ya Migunga Unaostawi Katika Mabonde’’ (Acacia Valley Open Woodland);

Aina hii ya uoto wa asili ya mimea miti ya migunga katika ‘’Koo’’(Genus) inayofahamika kama ‘’Acacia’’, leo hii kama ‘’Achelia), hupendelewa zaidi na wanyamapori ‘’Twiga’’(Maasai/Kilimanjaro Giraffe). Hata hivyo, pia hupatikana na aina nyinginezo za ‘’Koo’’(Genera) za mimea miti kama vile, ‘’Markhamia’’, ‘’Antidesma’’, ‘’Combretum’’, na kadha wa kadhalika. Pia katika ukanda wa eneo hili hupatikana tabaka la uoto wa mimea nyasi katika ‘’Koo’’(Genera) kama vile ‘’Loudetia’’, ‘’Perotis’’, na ‘’Hyparrhenia’’.

4 . ‘’Uoto wa Asili wa Mimea Miti ya Misitu Mchanganyiko pamoja na Maeneo Wazi ya Uoto wa Mimea Nyasi’’(Forest Grassland Mixture); Katika aina hii ya uoto wa asili, pia hupatikana aina kadhaa za jamii za mimea inayostawi katika tabaka la chini la ardhi yenye kuwa na kichanga. Maeneo wazi ya uoto wa mimea nyasi kawaida inahusisha aina za ‘’Koo’’ (Genera), kama vile; ‘’Loudetia’’, ‘’Perotis’’, na ‘’Hyparrhenia’’.

5.’’Uoto wa Asili wa Mimea Miti ya Mapori Mchanganyiko na Misitu’’(Woodland Areas & Forest Patches). Katika ukanda huu wa eneo hupatikana ustawi wa uoto wa mimea miti ya mapori mchanganyiko na misitu kama vile ‘’Koo’’ (Genera) zinazofahamika kama ‘’Parinari’’, ‘’Annona’’, ‘’Combretum’’, ‘’Croton’’, ‘’Albizia’’, ‘’Bersama’’, na ‘’Ficus’’(Mikuyu).

6. ‘’Uoto wa asili wa mimea miti ya misitu na jamii ya vichaka’’(Forest Thicket Communities); Hapa hupatikana kawaida ustawi wa miti mirefu ya misitu yenye kuwa na mizizi mirefu zaidi kwenda ardhini kama vile ‘’Koo’’(Genera) zinazofahamika kama ‘’Justicia’’ na ‘’Aframomum angustifolium’’, ‘’Lianas’’, ‘’Epiphytes’’, na kadha wa kadhalika. Koo za mimea miti iliyo mirefu kitabia (Canopy Trees) ni pamoja na ‘’Haplocodum’’, ‘’Ficus’’(Mikuyu), ‘’Albizia’’, ‘’Vitex’’, na ‘’Croton’’. Koo nyinginezo za mimea miti ya misitu ni kama vile, ‘’Acalypha’’, ‘’Carissa’’, ‘’Tedea’’, ‘’Chlorophora’’, ‘’Albizia’’, ‘’Rhus’’, ‘’Vangueria’’, ‘’Maytenus’, na pia ‘’Trema’’. Kwa ufupi, aina hii mbalimbali ya uwepo wa aina za uoto wa asili hifadhini Rubondo, huweza kukidhi na kusaidia ustawi wa maisha ya viumbe hai halisia wanaopatikana na kuishi katika hifadhi hii kama vile,’’Swala Nzohe’’(Sitatunga Antelopes),‘’Pongo/Mbawala’’(Bushbucks), ‘’Tumbili/Ngedere’’(Vervet/Black – Faced Monkeys), ‘’Viboko’’(Common/East African Hippopotamus), ‘’Mamba’’(Nile Crocodile),’’Panya Walao Miwa’’(Cane Rats), ‘’Fisi Maji Madoadoa Shingoni’’(Sport – Necked Otter), ‘’Kanu Mkubwa Madoadoa’’(Large – Spotted Genet), na wengineo kadhaa ambao kimsingi hupatikana katika idadi kubwa.

Ni katika kipindi cha msimu wa kiangazi (Dry – Season) ambao kimsingi huanzia ‘’Mwezi Juni’’ na kumalizikia ‘’Mwezi Agosti’’. Kwa utalii wa utazamaji maua pori na vipepeo ni katika kipindi cha msimu wa mvua za masika (Rainy/Wet Season) ambapo kawaida huwa ni katika ‘’Mwezi Novemba’’ na kuendelea mpaka ‘’Mwezi Machi’’. Kwa utazamaji wa viumbe hai ndege wahamao (Migratory Birds) ni katika ‘’Mwezi Desemba’’ mpaka ‘’Mwezi Februari’’.

inashauriwa na kupendekezwa kwa ‘’watanzania watalii’’ wa ndani watembeleao hifadhini wakajibebea vyakula vyao wenyewe vya kujipikia na mambo mengineyo yaliyo ya kimsingi ya kiuhitaji wa kibinadamu kama vile maji ya kunywa na kupikia, karatasi za chooni (toilet papers), na kadha wa kadhalika.

 

‘’Watanzania’’ watalii wa ndani wanaotembelea na kutalii hifadhini ‘’RUBONDO’’ wanashauriwa wakajiandaa kwa kujibebea vifaa vyao wenyewe vya malazi kama vile ‘’Mahema’’(Tents) na vifaa vinginevyo vilivyo vya muhimu vya kupiga kambi. Ndani ya ‘’Hifadhi ya Taifa ya Visiwa vya Rubondo’’(Rubondo Island National Park), pia hupatikana huduma za ‘’Kambi za Jumuiya’’(Public Campsites) kwa wageni watalii wanaohitaji huduma hii.

Ni jumla ya mambo muhimu na ya kimsingi kiutendaji ya maandalizi ya usafiri, huduma za chakula, malazi au kulala na mengineyo yaliyo muhimu. Hii ndio sehemu ya dira ya safari utalii ya matembezi na utalii hifadhini.

Haya ni mambo ya ziada ya mahitaji yanayojitokeza na upatikanaji wake katika sehemu husika watanzania watalii wa ndani wanapokuwepo.

Mambo muhimu ya kufahamu na kujiuliza

Elimu ya uelimishaji na mafunzo ya huduma ya kwanza ni ya muhimu sana na ya kimsingi kupeana miongoni mwetu sisi watanzania watalii wa ndani. Kanuni na taratibu ndani ya hifadhi kuzingatiwa ni pamoja na utekelezwaji wa sheria mama za mambo ya utunzaji wa mazingira katika hifadhi na sheria nyinginezo kwa ujumla wake.

Mkomazi4

Vifaa muhimu vya kuchukua katika safari utalii hifadhini

Vifaa vyote vilivyo vya muhimu katika safari utalii yenu ya matembezi hifadhini kama vile
Kamera, Video Kamera, Vitabu vya viongozi Vifaa vyote vilivyo vya muhimu katika safari utalii yenu ya matembezi hifadhini kama vile
Kamera, Video Kamera, Vitabu vya viongozi (Guide books) vya mimea, wanyamapori na ndege, Kalamu na madaftari madogo madogo ya kujiandikia na kujiwekea kumbukumbu zenu wenyewe.(Guide books) vya mimea, wanyamapori na ndege, Kalamu na madaftari madogo madogo ya kujiandikia na kujiwekea kumbukumbu zenu wenyewe.

Huduma za mahitaji mengineyo

Haya ni mambo ya ziada ya mahitaji yanayojitokeza na upatikanaji wake katika sehemu husika ambapo ‘’Watanzania’’ watalii wa ndani watakapokuwepo.

Maelezo ya huduma za habari utalii wa ndani.

MAWASILIANO MENGINEYO MAKAO MAKUU (TANAPA)

+255 272508216

info@domestictourismsafaris.c  info@domestictourismsafaris.co.tz