AINA ZA UTALII TANZANIA

MALIKALE TANZANIA

Utalii wa Malikale Tanzania

  • Dondoo;

Eneo  lenye utajiri  mkubwa  wa  kumbukumbu  za  kale na  utamaduni wa  kisasa.

  • Mkoa; Arusha  (Kanda ya kaskazini)
  • Wilaya: Ngorongoro (Mamlaka ya Hifadhi  Ngorongoro)
  • Umuhimu wake: Fuvu la binadamu wa Kale (Zinjanthropus boisei) kuweza kuishi duniani lenye kuwa na umri wa miaka takribani milioni 1. 75 lililovumbuliwa na Hayati DK. Mary Leakey katika ndani ya eneo la Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro.  Umuhimu mwingine upatikanao katika bonde la Oldupai ni pamoja na nyayo za zamadamu  wa Laetoli au Mwanadamu wa kale zenye kuwa na umri wa miaka takribani million 3.6. Vilevile umuhimu mwingine  ni  pamoja  na  jengo la makumbusho ya Bonde la Oldupai (OLDUPAI MUSEUM).
  • Dondoo;

 Mapango ya miamba ya chokaa yaliyotapakaa katika pwani ya Afrika ya Mashariki.

  • Mkoa: Tanga
  • Wilaya: Tanga Mjini

Umuhimu wake: Mapango ya Jiolojia makubwa ya miamba ya chokaa katika pwani ya Afrika ya Mashariki. Haijulikani idadi ya umri wa miaka yake. Tafiti bado zinaendelea.

 Dondoo;
Magofu ya Tongoni Mkoani Tanga ni ushuhuda wa makazi na utamaduni wa waswahili wa
karne ya 14 hadi 15 katika eneo hili. Kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo, Vasco Da Gama,
msafiri wa majini maarufu wakati wa enzi za kale, alitembelea eneo la Tongoni Tarehe 6
Aprili 1498.
 Mkoa: Tanga
 Wilaya: Tanga Mjini
 Umuhimu wake: Ushahidi wa makazi na utamaduni wa waswahili na uislamu. Magofu ya
Tongoni mkoani Tanga umri wake ni katika karne ya 13 hadi ya 15.

Dondoo:
Makumbusho ya Caravan Serai ni ushuhuda wa kumbukumbu za utumwa katika
Makumbusho ya Caravan Serai. Mfanya biashara Said Magram Awadh alijenga jengo hili
katika miaka ya mwanzo ya 1870 kama Hoteli kwa ajili ya kufikia misafara ya wafanyabiashara
za watumwa na meno ya Tembo kutoka bara kwenda katika soko la watumwa visiwani
Zanzibar. Eneo hili ndio asili ya neno Bwagamoyo (Bagamoyo) likiwa na maana ya
kupumzisha moyo baada ya safari ndefu.
 Mkoa: Pwani
 Wilaya: Bagamoyo
 Umuhimu wake: Makumbusho yanayoonyesha historia na matokeo ya biashara ya utumwa
katika njia ya kati ya biashara ya utumwa na vipusa. Makumbusho ya Caravan Serai yana
umri katika karne ya 19

  • Dondoo:
    Mji Mkongwe Bagamoyo ni mahali ambapo panapatikana majengo mazuri ya enzi za utawala
    wa Kijerumani. Ndani ya Mji Mkongwe Bagamoyo panapatikana Boma la Kijerumani
    lililojengwa mnamo mwaka wa 1897 na pia jengo la LIKU ambalo lilikuwa makao makuu ya
    utawala wa Kijerumani. Vilevile shule ya kwanza Tanzania iliyojengwa katika karne ya 19 kwa
    ajili ya wanafunzi kutoka jamii zote kama vile wazungu, wahindi na waafrika. Pia katika eneo
    la ufukweni, panapatikana jengo la forodha la enzi za utawala wa Kijerumani lililojengwa
    mnamo mwaka wa 1895. Pia Bandari ya Bagamoyo na soko la samaki. Katika upande wa
    Kusini, kunapatikana Jengo la ngome kongwe iliyojengwa katika karne ya 19 na kutumiwa na
    Sultan Seyyid Said wa visiwani Zanzibar kwa ajili ya kuhifadhi watumwa kwa muda wakiwa
    safarini kuelekea katika soko la watumwa visiwani Zanzibar.
     -Mkoa: Pwani
    -Wilaya: Bagamoyo.
    -muhimu wake: Jengo lililotumiwa na watumwa kuondoka Tanzania bara (zamani
    Tanganyika) kuelekea soko la watumwa visiwani Zanzibar. Jengo hili umri wake ni katika
    karne ya 19

Dondoo:
Magofu ya Kaole Bagamoyo ni ushuhuda wa historian a ushahidi wa makazi ya washirazi
katika pwani ya Afrika Mashariki katika karne ya 13.
 Mkoa: Pwani
 Wilaya: Bagamoyo
 Umuhimu wake: Ushahidi wa makazi na maisha ya waswahili katika Pwani ya Afrika ya
Mashariki katika karne ya 13.

Dondoo:
Michoro ya miambani ya Kolo – Kondoa katika Mkoa wa Dodoma ni ushuhuda wa kipekee
wa milenia kadhaa za uwindaji, uokotezaji na ukulima.
 Mkoa: Dodoma
 Wilaya: Kondoa
 Umuhimu wake: Njia zilizotumika kuhifadhi kumbukumbu za taarifa na matukio kabla ya
ugunduzi wa maandishi. Michoro ya miambani ya Kolo katika wilaya ya Kondoa, Mkoani
Dodoma umri wake ni takribani miaka 5000.

Dondoo:
Tembe la Dkt Livingstone, kwihara mkoani Tabora ni ushuhuda wa kumbukumbu za biashara
ya utumwa na safari ya mwisho ya Dkt. Livingstone kupitia njia ya kati ya biashara utumwa
na vipusa katika karne ya 19 akiambatana na wasaidizi wake waaminifu – SUSI na CHUMA.
 Mkoa: Tabora
 Wilaya: Tabora Mjini
 Umuhimu wake: Kumbukumbu ya biashara ya utumwa kupitia njia ya kati ya biashara ya
utumwa na vipusa katika karne ya 19.

 Dondoo:
Makumbusho ya kumbukizi ya Dkt Livingstone – Ujiji Kigoma ni ushuhuda wa kumbukumbu
za harakati za kupinga biashara haramu ya utumwa iliyokuwa ikifanyika kupitia njia ya kati ya
biashara haramu ya utumwa na vipusa katika karne ya 19 ikiwa ni pamoja na maneno
maarufu yaliyosemwa na H.M. STANLEY – Dr. Livingstone I PRESUME!!!
 Mkoa: Kigoma
 Wilaya: Kigoma mjini
 Umuhimu wake: kumbukumbu ya biashara ya utumwa katika karne ya 19.

Dondoo:
Kimondo cha Mbozi ambacho ni cha nane kwa ukubwa duniani kinapatikana katika kijiji cha
Ndolezi wilayani Mbozi katika mkoa mpya wa Songwe na kinakadiriwa kuwa na uzito wa tani
12 ambacho kwa ukubwa ni cha pili katika Afrika.
 Mkoa: Songwe
 Wilaya: Mbozi
 Umuhimu wake: Kimondo chenye uzito wa tani 12 na umri wake bado haujulikani. Tafiti
bado zinaendelea.

Dondoo:
Muhula wa zama za mawe ISIMILA mkoani Iringa ni eneo lenye kuwa na zana za muhula wa
Mawe za Acheulean pamoja na nguzo za miamba ya jiolojia zinazovutia sana
zilizosababishwa na mmomonyoko wa udongo.
 Mkoa: Iringa
 Wilaya: Iringa vijijini
 Umuhimu wake: Ushahidi wa matumizi ya zana za mawe takribani miaka 10,000 mpaka
40,000.

Dondoo:
Magofu ya Kilwa kisiwani na Songo mnara, mkoani Lindi ni ushuhuda jinsi ambavyo ni
namna gani Kilwa ilivyokuwa jiji maarufu la kibiashara katika karne ya 19.
 Mkoa: Lindi
 Wilaya: Kilwa
 Umuhimu wake: Ushahidi wa makazi ya mwanzo mnamo karne ya 9 kama vile msikiti mkuu
wa karne ya 11 hadi 15. Vilevile jumba la kifalme la makutani na msikiti mdogo wenye
madungu juu pamoja na jumba la kifalme la Husuni kubwa na Husuni ndogo.

Dondoo;
Makumbusho ya nyumba ya Mwalimu nyerere ,Magomeni, Dares salaam ni ushuhuda wa
kumbukumbu za maisha ya Hayai Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere katika karne ya 20 wakati
wa harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Dondoo; Mji wa kihistoria wa mikindani mkoani Mtwara unapatikana kusini mashariki mwa Tanzania, takribani kilometa 546 kutoka Dares-salaam katika pwani ya bahari ya Hindi. Kuanzia karne ya 9, historia ya Mikindani inaonyesha mwingiliano baina ya watu kutoka mataifa ya Uarabuni, Ureno, Ujerumani na Uingereza hivyo kuwepo kwa mchanganyiko wa tamaduni, majenzi na mapishi. Mji huu pia ulikuwa ni kituo cha utawala wa Kijerumani na pia kituo cha biashara haramu ya watumwa kwenda visiwa vya REUNION, USHELISHELI na COMORO. Vilevile kilikuwa ni kituo cha mwisho cha safari ya Dkt Livingstone kuelekea Afrika ya kati.

Dondoo: Magofu ya Kunduchi mkoani Dares Salaam yanapatikana umbali wa kilometa 22 kutoka katika jiji la Dares Salaam. Magofu haya ni ushahidi usio na shaka kuhusiana na maendeleo ya waswahili na uislamu yaliyokuwa yamefikiwa katika ukanda huo kuanzia karne ya 18 hadi ya 19.

Dondoo: Magofu ya Kunduchi mkoani Dares Salaam yanapatikana umbali wa kilometa 22 kutoka katika jiji la Dares Salaam. Magofu haya ni ushahidi usio na shaka kuhusiana na maendeleo ya waswahili na uislamu yaliyokuwa yamefikiwa katika ukanda huo kuanzia karne ya 18 hadi ya 19.

MAKUMBUSHO YA TAIFA TANZANIA

Utalii wa Makumbusho ya Taifa Tanzania.

  • Dondoo:
    Makumbusho ya kumbukizi ya vita vya majimaji yamejengwa na yanapatikana katika eneo
    ambalo mashujaa wa vita walizikwa baada ya kunyongwa na utawala wa wakoloni
    wajerumani mnamo tarehe 27/10/1906, mjini Songea katika mkoa wa Ruvuma. Makumbusho
    ya kumbukizi ya vita vya majimaji yalifanywa rasmi kuwa makumbusho ya Taifa mnamo
    mwaka wa 2010.
  • Dondoo:
    Kijiji cha makumbusho kinapatikana katika eneo la Kijitonyama katika barabara ya Ali Hassan
    Mwinyi, mkoani Dares Salaam. Kijiji cha makumbusho kilianzishwa na kufunguliwa rasmi kwa
    umma wa wananchi wa Tanzania mnamo mwaka wa 1967 kwa ajili maalumu ya kuhifadhi
    utamaduni wa asili wa Tanzania na hasa mitindo ya ujenzi wa nyumba za asili za jamii ya
    makabila mbalimbali nchini Tanzania.

Dondoo:
Makumbusho ya Azimio la Arusha yanapatikana katika mtaa wa Kaloleni karibu kabisa na
Mnara wa Mwenge Mkoani Arusha. Makumbusho haya ya Azimio la Arusha yalianzishwa
mnamo mwaka wa 1967 mara tu baada ya uhuru wa Tanganyika. Makumbusho ya kumbukizi
na kielelezo cha Azimio la Arusha na Siasa ya ujamaa na kujitegemea.

Dondoo:
Makumbusho ya Mwalimu J.K.Nyerere ni makumbusho yanayohifadhi kumbukumbu na urithi
wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na historia ya maisha yake na
uongozi wake. Makumbusho haya yanapatikana Butiama katika wilaya ya Musoma mkoani
Mara. Makumbusho ya Mwalimu Nyerere yalijengwa tangu mwaka wa 1987 na kufunguliwa
rasmi mnamo mwaka wa 1999.

  • Dondoo:
    Makumbusho haya yanapatikana mtaa wa Shaaban Robert mkabala na chuo cha usimamizi
    wa fedha (IFM). Ikumbukwe na ifahamike ya kwamba makumbusho haya yalianza kama
    kumbukumbu na heshima kwa mfalme George V wa Uingereza aliyefariki katika mwaka 1936.
    Makumbusho haya yalifunguliwa rasmi kwa jamii mwaka wa 1940 na baada ya uhuru
    ilifanywa kuwa makumbusho ya Taifa mnamo mwaka wa 1963.

Maelezo ya huduma za habari utalii wa ndani.

MAWASILIANO MENGINEYO MAKAO MAKUU (TANAPA)

+255 272508216

info@domestictourismsafaris.c  info@domestictourismsafaris.co.tz