Nchi Ya Tanganyika (Leo hii ikijulikana kama ‘’Tanzania Bara’’)
Tanganyika (Tanzania Bara) ilijipatia uhuru wake kamili wa madaraka wa kujitawala wenyewe mnamo tarehe 9 Desemba ya mwaka wa 1961, chini ya uongozi wa waziri mkuu wa kwanza ‘’Hayati Baba Wa Taifa’’ na vilevile ‘’Muasisi’’ wa ‘’Taifa Letu Mama Tanzania’’, ‘’Mwalimu Julius Kambarage Nyerere’’ na mnamo mwaka wa 1962, Tanganyika (Tanzania Bara) ikawa Jamhuri na ‘’Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akawa Rais’’.
Hapo Awali Zamani Kale (Miaka ya Zamani) Katika ‘’Nchi Ya Tanganyika’’ (Tanzania Bara)
Kwa takribani zaidi ya miaka 40 iliyopita mpaka mwishoni kabisa mwa ‘’Vita Vya Kwanza Vya Dunia’’ (World War One) ambavyo kimsingi vita hivi vilifanyika na kupigwana mnamo baina ya miaka ya ‘’1914 mpaka 1918’’, ‘’Nchi Ya Tanganyika’’ (Tanzania Bara) ilikuwa chini ya uongozi na uthibiti wa himaya ya ‘’Kampuni Ya Wajerumani Ya Afrika Mashariki’’ (German East Africa Company) na baadaye tena katika ‘’Dola Ya Watawala Wakoloni Wajerumani’’. Baadaya vita vya kwanza vya dunia (World War One) kumalizika kati ya mwaka ‘’1914 – 1918’’, udhibiti na mamlaka ya ‘’Nchi Ya Tanganyika’’ (Tanzania Bara) ukawa ‘’Chini Ya Utawala Na Uongozi Wa Watawala Wakoloni Waingereza’’, kuanzia mnamo mwaka wa 1919 mpaka mnamo tarehe 9 Desemba ya mwaka wa 1961, pale ambapo ‘’nchi ya Tanganyika’’ ilipojipatia uhuru wake rasmi wa kujitawala na kujiongoza chini ya Hayati Baba wa Taifa, ‘’Mwalimu Julius Kambarage Nyerere’’. Hivyo basi ‘’Mkoloni Muingereza’’ alitawala ‘’Nchi ya Tanganyika’’ (Tanzania Bara) kwa takribani miaka 42. Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba ‘’Watawala WakoloniWaingereza’’ vilevile walivitawala ‘’Visiwa Vya Nchi Ya Zanzibar ‘’ ambavyo kimsingi vilikuwa chini ya utawala wa kimla na usimamizi wa ‘’Sultan Wa Kiarabu , Sultan Jamshid bin Abdullah’’, lakini chini ya ‘’Himaya Ya Waingereza’’ tangu mnamo wa miaka ya 1890.
Baba Wa Taifa – ‘’Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere’’
Baba wa ‘’Taifa Mama Tanzania’’, Hayati Mwalimu ‘’Julius Kambarage Nyerere’’, ambaye pia ni ‘’Muasisi’’ wa kwanza wa ‘’Taifa Letu Sote Tanzania’’ (Tanganyika na Zanzibar), aliitawala Tanzania katika mfumo wa ‘’Chama Kimoja Cha Siasa’’(Single Party Political System) akiwa madarakani tangu mnamo mwaka wa 1961 mpaka alipojiuzulu na kung’atuka kutoka madarakani na katika uongozi wa nchi yeye mwenyewe binafsi mnamo mwaka wa 1985. ‘’Chama Tawala Cha Mapinduzi (CCM)’’ cha Mwalimu ‘’Julius Kambarage Nyerere’’, tokea kuasisiwa na kuanzishwa kwake mnamo wa ‘’Tarehe 5 Mwezi Februari’’ ya mwaka wa 1977, kimekuwepo madarakani katika uongozi wa nchi kwa kipindi kirefu sana na kuweza kushinda katika ‘’Uchaguzi wa mfumo wa vyama vingi vya siasa (Multi – Party Political System) kwa takribani mara 4 tokea kuasisiwa na kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa (Multi – Party Political System) nchini ‘’kwetu Tanzania’’ tangu mnamo mwaka wa 1995’’. Marais wengineo waliowahi kutawala na kuongoza ‘’nchini kwetu Tanzania’’ (Tanganyika pamoja na visiwa vya Zanzibar) baada ya Baba wa Taifa, ‘’Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere’’, ni pamoja na ‘’Mheshimiwa Hayati Ali Hassan Mwinyi’’ (mnamo mwaka wa 1985 mpaka 1995 katika mfumo wa chama kimoja cha siasa), ‘’Mheshimiwa Hayati Benjamin William Mkapa’’, katika mfumo wa vyama vingi vya siasa (mnamo mwaka wa 1995 mpaka 2005), ‘’Mheshimiwa Daktari Jakaya Mrisho Kikwete’’, mnamo mwaka wa 2005 mpaka 2015), ‘’Mheshimiwa Hayati Daktari John Pombe Joseph Magufuli’’, mnamo mwaka wa 2015 mpaka 2021), na hivi sasa ‘’Mheshimiwa Daktari Samia Hassan Suluhu’’, mnamo mwaka wa 2021 mpaka 2025), na pia ni mgombea urais tena kupitia tiketi ya ‘’Chama Chake Cha Mapinduzi /CCM’’ katika ‘’Uchaguzi Mkuu Wa Urais, Wabunge na Madiwani’’ uliofanyika mnamo tarehe 29 Oktoba ya mwaka wa 2025, na kuweza kufanikiwa kuchaguliwa na kushinda tena kiti cha urais wa kuingoza nchi ya Tanzania kwa kipindi kingine kijacho cha miaka mitano.