TALII NA TEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA MLIMA KILIMANJARO

Mkoani Kilimanjaro (wilayani Moshi vijijini pamoja na wilayani Rombo) katika kanda wa kaskazini mwa Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Chanzo Cha Chimbuko Halisia Kimaelezo Na Ubunifu (Mwalimu Edgardo K.Welelo)

Ukweli Wa Mambo Kuhusiana Na Hifadhi Taifa ya Mlima Kilimanjaro (Mkoani Kilimanjaro) Katika Ukanda Wa Kaskazini Mwa Jamhuri Ya Muungano Ya Tanzania Pamoja Na Historia Yake; Ukweli halisia wa mambo ni ya kwamba Mkoa wa Kilimanjaro upatikanao kijiografia katika ukanda wa Kaskazini - Mashariki mwa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania umejipatia jina “Kilimanjaro” kutokana na Mlima KILIMANJARO kama nembo ya mkoa huu, ambao ndio ulio Mlima mrefu zaidi kuliko yote barani AFRIKA kama paa la Afrika na vilevile nchini kwetu Tanzania katika mita 5,895 kutoka usawa wa Bahari na pia ndio Mlima pekee zaidi duniani uliosimama huru peke yake wenyewe ambao una vilele vitatu ambavyo ni KIBO (Uhuru) katika futi 19,341 au mita 5,895, MAWENZI katika futi 16,900 au mita 5,150, pamoja na SHIRA katika futi 12,936 au mita 3,962. Kwa mujibu wa maelezo ya kabila wenyeji asilia la Wachagga wa Mkoa huu waishio kuzunguka maeneo haya ya Mlima Kilimanjaro ni ya kwamba neno au jina “Kilimanjaro” ni neno asilia kabisa la kabila la Wachagga ikimaanisha “Kilema Kyaro”. ‘Kilema’, ikimaanisha Mlima. “Kyaro”, inamaanisha Safari. Tafsiri rahisi hapa ina maana ya kwamba safari ya matembezi kuelekea kupanda kilele cha Mlima Kilimanjaro kilikuwa kikiwashinda watu wengi waliojaribu kupanda mlima na hii ilikuwa wakati wa kipindi cha nyakati hizo za miaka ya zamani. Leo hii hali hiyo haipo tena kwasababu wengi wa watalii kutoka nje ya nchi na ndani ya nchi hufika kileleni mwa Mlima Kilimanjaro pasipo shida yeyote ile. Hata hivyo ni vema na busara ikumbukwe na ieleweke ya kwamba neno au jina ‘KILIMANJARO’ limeelezewa kuwa na maana zaidi ya moja kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya vitabu na waandishi wake.

Ushauri kwa watalii raia wa Tanzania katika kujiandaa na kujipanga kimaandalizi kwa safari utalii

Utalii ni burudani na vilele ni sehemu ya mafunzo ya kielimu. Hivyo basi, kwa njia yeyote ile iwe au isiwe, fedha zinahitajika katika maandalizi ya kupanda mlima. Ufanisi wa kufanikisha maandalizi ya matembezi ya mguu katika kupanda mlima utategemea zaidi jinsi fedha zitakavyotumika na mpangilio wa bajeti ya fedha hizo.

Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro katika mkoa wa Kilimanjaro ilianzishwa rasmi mnamo mwaka wa 1973.Hifadhi hii ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro ina ukubwa wa eneo takribani kilometa za mraba 1,712, na vilevile ilitangazwa rasmi na taasisi ya kimataifa ya umoja wa mataifa inayojihusisha na elimu, sayansi na utamaduni (UNESCO) kama urithi wa dunia mnamo mwaka wa 1987 na pia maajabu asilia ya bara la Afrika katika mwaka 2013. ◦UFIKAJI HIFADHINI MLIMA KILIMANJARO NA UPATIKANAJI WAKE KIJIOGRAFIA Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro inafikika kwa njia ya usafiri wa barabara umbali wa kilometa takribani 48 kutokea Mji wa Moshi ambao ndio makao Makuu ya Mkoa wa Kilimanjaro kufikia katika kijiji cha Marangu ambayo ndio yaliyo makao makuu ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro. Vilevile hifadhi hii inafikika umbali wa kilometa 128 kutokea Mkoani Arusha. Inachukua mwendo wa dakika 50 kutoka Moshi Mjini, vilevile ni mwendo wa saa 1 kutoka katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Kilimanjaro (KIA). Hali kadhalika ni saa 2.30 kutoka mkoani Arusha.

Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro inafikika kwa njia ya usafiri wa barabara umbali wa kilometa takribani 48 kutokea Mji wa Moshi ambao ndio makao Makuu ya Mkoa wa Kilimanjaro kufikia katika kijiji cha Marangu ambayo ndio yaliyo makao makuu ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro. Vilevile hifadhi hii inafikika umbali wa kilometa 128 kutokea Mkoani Arusha. Inachukua mwendo wa dakika 50 kutoka Moshi Mjini, vilevile ni mwendo wa saa 1 kutoka katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Kilimanjaro (KIA). Hali kadhalika ni saa 2.30 kutoka mkoani Arusha.

Ni pamoja na kanda 5 za mazingira ya makazi na mojawapo ya hizi kanda ni pamoja na mandhari nzuri yenye kupendeza ya uoto wa msitu wa kitropiki wa mlimani (Montane Forest), vilele vitatu vya Mlima Kilimanjaro ambavyo ni Shira, Kibo (Uhuru) na Mawenzi.

Ina anzia mita 1829 katika lango la kuingilia la Marangu mpaka mita 5895 katika
kilelele cha Kibo (Uhuru).

Ni pamoja na mandhari nzuri yenye kupendeza ya uoto wa asili wa msitu wa kitropiki wa mlimani (Montane Forest), vilevile vilele 3 vya Mlima Kilimanjaro ambavyo ni Shira (mita 3,962), Mawenzi (mita 5,150) na Kibo (Uhuru) katika mita 5,895). Kunapatikana takribani njia 7 za kupanda Mlima Kilimanjaro ambazo ni Rongai, 24 - Machame, Londorosi, Lemosho, Kilema, Mweka, pamoja na Umbwe.Vivutio vya utalii vinginevyo ni kama vile sura ya mandhari ya eneo; maeneo ya kitamaduni ya kabila la Wachagga (Kifinika), mapango na vilevile shimo la lava katika mlima (Maundi crater), maporomoko ya maji ya Lauwo.

Wanyamapori jamii ya nyani (primates) kama vile mbega wenye rangi nyeusi na nyeupe, nyani, kima na ngedere.Wengineo ni pamoja na Tembo (ndovu), Mbuzi mawe, Funo, Tohe mlima, Twiga, Kuro, Ngiri , Chui, Kindi, Pimbi, Pofu, Nyegere na wengineo wengi. Vilevile kunapatikana aina mbalimbali za viumbe hai ndege. Kwa ujumla wake, hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro ina zaidi ya spishi za mammalia (mammals) takribani 140, kwa mfano, wanyamapori jamii ya nyani (primates) spishi 7, jamii ya walaji wa nyama (carnivores) takribani spishi 25, jamii ya swala (antelopes) spishi takribani 25, popo aina 24, na ndege spishi 179. ◦UOTO WA ASILI HIFADHINI MLIMA KILIMANJARO Katika maeneo matano ya kanda za uoto wa asili nchini Tanzania (Phytogeographical regions), hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro inaangukia katika eneo la uoto wa asili wa misitu wa kitropiki wa milimani (Afro – Montane forest) ambavyo vilevile ikihusisha pia na uoto wa asili wa misitu wa Milima ya Tao la Mashariki (Eastern Arc Mountains ) kama vile Milima ya Usambara Mashariki na Magharibi na vilevile Milima ya Upare Kusini na Kaskazini, na kadhalika.

Katika maeneo matano ya kanda za uoto wa asili nchiniTanzania (Phytogeographical regions), hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro inaangukia katika eneo la uoto wa asili wa misitu wa kitropiki wa milimani (Afro Montane forest) ambavyo vilevile ikihusisha pia na uoto wa asili wa misitu wa Milima ya Tao laMashariki (Eastern Arc Mountains ) kama vile Milima ya Usambara Mashariki na Magharibi na vilevile Milima ya Upare Kusini na Kaskazini, na kadhalika.

Mwezi wa Desemba mpaka Februari. Vilevile pia mwezi wa Julai mpaka mwezi wa  Septemba.

Kwa Mlima Kilimanjaro ni suala la lazima kuwa na mpishi wenu na vilevile kubeba vyakula vyenu wenyewe kwa siku zote mtakazo kuwa mlimani. 

Kwa Mlima Kilimanjaro kuna vibanda vya kupiga kambi mlimani (Mountain huts) na vilevile ni lazima kubeba mahema yenu wenyewe binafsi kwa ajili ya zoezi zima la kupiga kambi na kulala.

Gharama zote za usafiri zitakamilika na kufahamika baada ya kuzingatia na kufuatilia mambo muhimu ya kimsingi kama vile maandalizi ya usafiri, huduma za chakula, malazi au kulala na mahitaji mengineyo muhimu yatakayojitokeza.

Kabla ya kupanda Mlima Kilimanjaro ni lazima kama ikibidi kuwa na mazoezi fulani ya kutembea. Vilevile suala la huduma ya kwanza kama vile sanduku la huduma ya kwanza ni muhimu kabisa.

Mambo ya kufanya na kuzingatia (kanuni na taratibu ndani ya hifadhi);

Utaratibu maalumu unahitajika katika suala zima la matembezi hifadhini Kilimanjaro katika kupanda mlima. Je Kampuni ya utalii mtakayoitumia kupanda mlima Kilimanjaro ina kibali cha utalii kupandisha watalii mlimani?Afya husika za watu katika kupanda Mlima Kilimanjaro zinaruhusu au hapana?Mambo mengineyo muhimu ni pamoja na kuhakikisha ya kwamba kunapatikana vifaa vya kupandia mlima Kilimanjaro. Utekelezaji na ufuatiliaji wa kanuni na taratibu hifadhini. Hizi taratibu na kanuni zake ndio mwongozo wa shughuli zote ndani ya hifadhi. Kwa maelezo zaidi soma vepeperushi vya hifadhi husika.

Vifaa vya kuchukua katika safari utalii hifadhini

Vifaa vyote muhimu vinavyohusiana na safari utalii na matembezi hifadhini katika kupanda mlima kilimanjaro . viongozi wenu katika kikundi chenu cha watalii wa ndani watawajulisheni au kampuni husika itakayowahudumia katika kupanda mlima kilimanjaro itawajulisheni.

Huduma za mahitaji mengineyo

 Mambo ya ziada ya mahitaji yanayojitokeza na upatikanaji wake katika sehemu husika watanzania watalii wa ndani waliopo.

Maelezo ya huduma za habari utalii wa ndani.

MAWASILIANO MENGINEYO MAKAO MAKUU (TANAPA)

+255 272508216

info@domestictourismsafaris.c  info@domestictourismsafaris.co.tz